Polisi Masasi, ni wakati wa kuwaonesha maovu yenu

Sesimba

Senior Member
Dec 20, 2016
189
382
Wanajukwaa Salaam!

Naomba niwaeleze snario iliyopo Polisi Wilaya ya Masasi Mkoa wa MTWARA.

Iko Hivi, tarehe 27 oct 2021 kulitokea tukio la kukamatana masuala ya ugoni.

Bwana J ndiye Mwenye Mke ambaye baada ya kumuona mkewe amebadilika kitabia na mienendo yake mibaya aliamua kumfuatilia kwa ukaribu. Hivyo katika kufuatilia aliweka mitego yake na ndipo siku 40 za mwizi zilitimia.

Baada ya mtego kukamilika aliwachukua ndugu zake 7 ambapo walifika kwenye guest wakawakuta. Mgoni aliambiwa waende polisi lakini kabla ya kufika hatua ya kwenda polisi mgoni aliomba msamaha na kutaka wayamalize.

Jamaa akaagiza kwa kijana wake amletee fedha pale alipokuwepo. Kweli ililetwa ambapo Mwenye mke alikuwa analazimisha waende polisi lakini mgoni alikataa na kutaka wayamalize.

Mgoni alipoletewa fedha alimtaka Mwenye Mke aweze kupokea fedha kiasi cha Milioni 5! Kweli ndugu wa jamaa Mwenye mke walimsihi wayamalize kwa mtindo huo na kumfichia aibu mkewe kwa kuwa tayari yameshatokea.

Hoja yangu siyo kueleza hayo Bali Ni matukio baada ya Jambo Hilo kumalizika kule guest.

Ndugu zangu Wana jamii! Baada ya tukio, yule aliyeshikwa Alikwenda polisi na kugeuza kesi kwamba amekabwa na kutekwa na Yule Mwenye mke na kwamba wamlazimisha amtume mwanaye kuleta fedha.

Polisi walichofanya wakamkamata Mwenye mke na mkewe na mmoja wa ndugu yake wakawaweka ndani toka tarehe 28/10 Hadi leo tarehe 07 Nov 2021 Ni siku ya 11 wapo selo ya polisi Wilaya na hawajapekwa japo mahakamani.

Kumbe jamaa amewalipa fedha polisi na kuwaambia wahakikishe wanamkomesha Mwenye mke anarudisha fedha. Na Mwenye mke amesema hatarudisha fedha Ila Kama kweli mgoni wake alichowaeleza Ni kweli wakamalize mahakamani.

Suala sasa limebakia hapo na sasa Mgoni hapokei simu na hata akipigiwa simu anakata na anazima simu.

Ndugu wamekwenda Hadi kwa DC na DC alimuagiza OCD awaachie lakini OCD amekaidi. Ukweli kunapoendelea Ni kubaya baina ya familia hii na Jeshi la Polisi na kwa taarifa kunafanyika organization watu wanataka kuandamana Kama walivyofanya wakati wa gesi ya Mtwara na kwa mnaokumbuka ilileta madhara makubwa mno na ikumbukwe chanzo hasa kilikuwa Ni hao polisi kupitia kwa traffic mmoja.

Waziri Simbachawene tambua hili.
Waziri Mwambe Jofrey na (Mb) wa Jimbo la Masasi tambua hili.

Polisi MASASI wanafanya Jambo la hatari Sana.
 
Nachoona wanachofanya polisi nisahihi kabsa mtu wamekubaliana na mkeo wanalalana halaf Bdo mnahangaishana mpaka polisi Ili iweje ingekua kubaka Sawa na ningependa waendelee kuwashikilia shenz kabsa watu wanageuza wake zao Kama mtaji
 
Polisi wanahusika nini kwenye ugoni? Polisi wanahusika kwenye ubakaji, mahakama ndiyo inahusika na ugoni.
Unajua point ya mtoa mada? Au baada ya kukurupushwa na notification basi ukasoma hata hijaelewa ukajikuta umemjibu? Anacholaani huyu mtoa mada Ni kwa Nini polisi watumike kwa kununuliwa na mtu?

Maana Kama wamewakamata watu Leo siku ya 12 Sasa bila kupelekwa mahakamani Ni Nini lengo lao na familia hiyo? Maana Kama wameona hiyo familia Ina makosa basi wawapandishe kizimbani ili sheria ifuate mkondo wake
 
Pointi yangu ni kwamba ukifumaniwa kataa kwenda polisi, polisi hawahusiki kwenye fumanizi, umefumaniwa mwambie twende mahakamani, kwanini alikubali kwenda polisi?
 
Polisi wanahusika nini kwenye ugoni? Polisi wanahusika kwenye ubakaji, mahakama ndiyo inahusika na ugoni.
Ukweli ni huo walipaswa kuwapeleka mahakamani lakini wamewaweka ndani siku ya 12 leo. Lakini jamaa kwa kuwa ana jina kwa hiyo kinachoonekana Ni kwamba wanataka rushwa.
 
Hizo ni shobo za ndoa kwa ufupi polisi awanaga shobo nazo ni pasua kichwa sana
Jamaa wamepuliziwa mtonyo kwa ili kukubali uongo wa mgoni kwamba eti amevamiwa wakati uongo.

Hebu fikiria Kuna Mtendaji alikuwepo kwenye tukio alipokwenda polisi kuwaeleza kwamba hao waliowaweka ndani hawana hatia. Wakamuweka ndani siku ya pili wakamtoa na kumuonya asijuhusushe na kesi hamhusu. Je Hadi hapo hujaona Kama Kuna Jambo linatengenezwa?
 
Pointi yangu ni kwamba ukifumaniwa kataa kwenda polisi, polisi hawahusiki kwenye fumanizi, umefumaniwa mwambie twende mahakamani, kwanini alikubali kwenda polisi?
Aliataa ndiyo maana aliomba wayamalize na kuficha aibu. Lakini wahusika walipokubali yeye akaeageuka na kwenda polisi kueleza kwamba kavamiwa na kulazimishwa kutoa fedha Jambo ambalo Ni uongo.
 
Hii kali sema tu nikitoka hapo mahakamani ntatumia njia yeyote kuhakikisha Mgoni anaelekea futi 6 chini!

Katika njia yeyote iwe mzizioloji au planned assasination. Yani namfatilia kimya kimya ipo siku ataishia kubaya.
 
Nachoona wanachofanya polisi nisahihi kabsa mtu wamekubaliana na mkeo wanalalana halaf Bdo mnahangaishana mpaka polisi Ili iweje ingekua kubaka Sawa na ningependa waendelee kuwashikilia shenz kabsa watu wanageuza wake zao Kama mtaji
Ndugu acha nijusamehe Sana
Hebu fanya kwamba wewe ndiyo umemkuta mkeo analiwa na jamaa umeamua kusamehe kwa nmna fulani Halafu u akamatwa Tena wewe , mkeo na Ndugu yako mnawekwa ndani ungejisikiaje?

Tusiongee tu kwa kuwa yamemkuta mwenzio.
 
Unajua point ya mtoa mada? Au baada ya kukurupushwa na notification basi ukasoma hata hijaelewa ukajikuta umemjibu? Anacholaani huyu mtoa mada Ni kwa Nini polisi watumike kwa kununuliwa na mtu?

Maana Kama wamewakamata watu Leo siku ya 12 Sasa bila kupelekwa mahakamani Ni Nini lengo lao na familia hiyo? Maana Kama wameona hiyo familia Ina makosa basi wawapandishe kizimbani ili sheria ifuate mkondo wake
Kweli Kaka wewe unaelewa.
 
Hii kali sema tu nikitoka hapo mahakamani ntatumia njia yeyote kuhakikisha Mgoni anaelekea futi 6 chini!

Katika njia yeyote iwe mzizioloji au planned assasination. Yani namfatilia kimya kimya ipo siku ataishia kubaya.
Ndicho kitakachomkuta jamaa...watu 12 kuwaweka ndani Ni uhuni....
 
Ndugu acha nijusamehe Sana
Hebu fanya kwamba wewe ndiyo umemkuta mkeo analiwa na jamaa umeamua kusamehe kwa nmna fulani Halafu u akamatwa Tena wewe , mkeo na Ndugu yako mnawekwa ndani ungejisikiaje?

Tusiongee tu kwa kuwa yamemkuta mwenzio.
Mke Mpaka anaamua kut0mbw@ nje ( hajabakwa Hapo) tyari ni red card hapo hawezi badilika ipo siku atagongwa tu tena Sasa ndugu utagombana na wangap inamaana Si utakua unaonekana punguani Sasa daily Wew na kugombana na wagoni
 
Back
Top Bottom