POLISI: Marufuku Kulipua Mafataki Mkesha wa Mwaka Mpya

Bramo

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
13,160
10,007
Akiongea katika Pozi lililobeba Maslahi ya Ki Taifa Zaidi,
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP (Commissioner of Police) Alhaji Suleiman Kova amepiga Marufuku kikundi ama mtu yeyote kulipua Fataki kwenye Mkesha wa Mwaka Mpya
Msingi wa Katazo hili unabebwa na Matishio ya Ugaidi yanayoukumba ukanda wa Africa Mashariki.
"Tunajali Maslahi ya Taifa, Starehe ya Mtu mmoja au kikundi cha watu wachache haiwezi ku Compromise uhai wa watu wengi, Magaidi wanaweza kutumia Loop hole ya ulipuaji Mafataki kulipua Mabomu yao ya Ukweli, hii inaweza ku mis lead Polisi na kushindwa ku act on time" alisema Alhaji CP Kova.

Source ITV Habari, 20:00 Hours

My Take.
Kwa kweli leo Binafsi nimefarijika sana na amri ya CP Kova
 
Uwezo wa inteligensia za nchi unapimwa kwa kuzuia matukio ya uvunjifu wa sheria na siyo kufika mapema katika tukio baada ya kutokea.

Maelezo ya Afende Kova yanaonyesha kuwa vyombo vyetu vya ulinzi vinafanya kazi kwenye misingi ya reactive than proactive. Hii ni failure katika majukumu yake ya kila siku.

Kwa nchi ambazo vyombo vyake vya ulinzi vinafahamu vizuri pilika pilika za nchi, swala la mafataki ni non agenda.

Kwa nini watu wasipewe angalau muda maalum wa kufyatua hayo mafataki na wakashangilia kuuona mwaka mpya.
 
Akiongea katika Pozi lililobeba Maslahi ya Ki Taifa Zaidi,
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP (Commissioner of Police) Alhaji Suleiman Kova amepiga Marufuku kikundi ama mtu yeyote kulipua Fataki kwenye Mkesha wa Mwaka Mpya
Msingi wa Katazo hili unabebwa na Matishio ya Ugaidi yanayoukumba ukanda wa Africa Mashariki.
"Tunajali Maslahi ya Taifa, Starehe ya Mtu mmoja au kikundi cha watu wachache haiwezi ku Compromise uhai wa watu wengi, Magaidi wanaweza kutumia Loop hole ya ulipuaji Mafataki kulipua Mabomu yao ya Ukweli, hii inaweza ku mis lead Polisi na kushindwa ku act on time" alisema Alhaji CP Kova.

Source ITV Habari, 20:00 Hours

My Take.
Kwa kweli leo Binafsi nimefarijika sana na amri ya CP Kova

Ook Kova!!
Kwa sisi wa hapa Arusha tumezoea fataki kuanzia kwa wahindi(baniani mbaya) pale msikitini kwao chini ya ofisi za nssf mpaka migodini.
Sasa kwanini mtunyime kufyatua vitu tulivyovizoea milio yake?? Au mpaka tuwe Baniani ndiyo turuhusiwe kulipua fataki??
Wadau wa Ar, other alternative ni bastola, gobore, musbag n.k( kwa ujumla bunduki zilie za kutosha) Hii inakubalika hata alshabibi wakisikia wanasepa.
Au Uwongo Kova??
Hata intelijensia inajua baniani mbaya kiatu chake "dahwa"
 
Mjomba wangu Kova hapo umechemsha, maana watu tuisha ingia gharama kununua mafataki so tuyafanyie nini naona liwalo na litakuwa ila lazima mi nifyatue fataki zangu.
 
Mimi lazima nifyatue mafataki yangu....kova wewe ni janga la taifa. ..usituletee movie zako za joshua malundi
 
Hili katazo linahusu hoteli kubwa kama Naura springs,ngurdoto,kibo n.k?
Siku hizi fataki zinatumika hata kwenye harusi!
Kwa arusha hii amri sio halali kwani tumeshashihudia milipuko ya kigaidi mara mbili mchana kweupe bila shamrashamra za fataki...Kova Kajipange upya.
 
Sitakubali kuingia hasara kwa sababu ya domo la kova..mimi nitalipua kama mbwai na iwe mbwai..sasa yeye anataka mafataki tukayapikie ugali?....Hebu atutole interejenshia yake ya MAFATAKI
 
yaani mwaka mpya upite kimya kimya kama tunaomboleza msiba?.....huu nao ni unyanyasaji wa kirahatupuka...hajui kuwa now days magaidi yanafunga silencer kwenye mabomu yao?...
 
Back
Top Bottom