POLISI: Marufuku kukohoa pale unapopishana na mwanamke mwenye makalio makubwa, hilo ni shambulio la aibu tutakukamata

*"Uzuri Wa Mwanamke Sio Sura Ni Tabia.. TABIA Ni Kifupisho Cha Maneno "TAko BIdhaa Adimu" .. Na Kweli Wanaume Tunazingatia Hilo Ndo Maana Tukipishana Njiani Na Madem Lazima Tugeuke Kuangalia Kama TABIA Njema Ipo..*



*Wanaume Oyeeeh .."*
‍♂‍♂‍♂‍♂‍♂‍♂
 
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa mjini Magharibi Unguja Hassan Nasir Ally amekemea vitendo hivyo alivyovitaja kuwa ''shambulio la aibu''
''Mwanamke akipita pengine maumbile yamejazajaza ukaanza kukohoa mh mh hilo ni shambulio la aibu, tutakukamata tukupeleke mahakamani".


Tunaomba definitiona ya kujazajaza, ni ujazo wa kuanzia sentimeta ngapi hadi ngapi
 
yaani sasa ni kuwaweka ndani tu wanaume. hakuna kuvaa chupi na ukipita unarusha rusha chura mpaka wakohoe wapaliwe .koh koh koh koh mpaka segerea! asante jpm sasa tutapitisha makalio yetu barabarani kwa raha bila kupigwa tochi
Kho khoo khooooooo!
 
Wanaume wa unguja na ndugu zenu wa Dar Mkome kukohoa kohoa hovyo, mwanaume wa kweli anakojoa na sio kukohoa
 
treehe tehe tehe heheee!
waungwana hizi ni drama tu za kutusahaulisha jambo fulani la kisiasa ,
hao jamas si wanajua watz akili zetu zinapenda mambo ya namna gani , ukitaka kuwapata watz kuwadestruct ni rahisi sana.
 
yaani sasa ni kuwaweka ndani tu wanaume. hakuna kuvaa chupi na ukipita unarusha rusha chura mpaka wakohoe wapaliwe .koh koh koh koh mpaka segerea! asante jpm sasa tutapitisha makalio yetu barabarani kwa raha bila kupigwa tochi
Duuuhhh,,, nimecheka sana!!! bila chupi itakuwa balaa
 
Kama mada inavyojieleza

Kamanda mmoja wa polisi amesema ni marufuku kukohoa pale unapopishana au unapomwona mdada/mwanamke mwenye makalio makubwa

Kamanda huyo amesisitiza kwamba kukohoa huko kutapelekea kukamatwa kwa maana kitendo hicho ni "Shambulio la aibu"

Chanzo:video mtandaoni nimeshindwa kuiupload hapa


====

Tanzania: Kukohoa kohoa Unguja sasa kwaweza kuwatia wanaume matatani
15 Mei 2018
Sambaza habari hii Facebook Sambaza habari hii Twitter Mshirikishe mwenzako

Image caption
Baadhi ya wanawake hukumbwa na vitendo vya udhalilishaji wanapopita njiani na wanapokuwa kwenye maeneo yenye mikusanyiko ya watu
Vijana wanaodaiwa kukosa maadili mkoani Kaskazini Unguja, Tanzania wakijihusisha na vitendo vinavyotafsiriwa kuwa udhalilishaji wa utu wa mwanamke, watajikuta matatani iwapo wataendelea na vitendo hivyo.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa mjini Magharibi Unguja Hassan Nasir Ally amekemea vitendo hivyo alivyovitaja kuwa ''shambulio la aibu''
''Mwanamke akipita pengine maumbile yamejazajaza ukaanza kukohoa mh mh hilo ni shambulio la aibu, tutakukamata tukupeleke mahakamani".

Akizungumza na BBC kamanda Hassan ametaja kuwa kumekuwepo na ripoti kuhusu udhalilishaji katika eneo lake.

''Tuna wastani wa ripoti tano kwa wiki kuhusu udhalilishaji wa wanawake mkoa wa Kaskazini Unguja, tuliona tunahitaji kupambana na vitendo hivyo''

''Kuna ndugu zetu , watoto wetu, Mama zetu unakuta wana maumbo makubwa unakuta mtaani kuna vijana wasio na maadili, hawana adabu wamezoea kukohoa na kuzomeazomea wanapowaona wanawake wanapita mbele yao wanafanya wakiwa hawajui kama ni kosa la jinai jeshi la Polisi linafanya kazi ya kulinda utu wa mwanamke.Tutawashitaki kwa sheria ya kulinda wanawake na watoto.''

Polisi imesema itapambana na vitendo vya mashambulizi ya aibu dhidi ya wanawake na watoto

Idadi ya kesi za udhalilishaji wa wanawake imeongezeka kwa mujibu wa Takwimu zilizotolewa na chama cha waandishi wa habari wanawake TAMWA-ZANZIBAR ambapo kwa miezi mitatu ya mwanzo wa mwaka huu 2018 tayari kumeripotiwa kuwepo kwa kesi 44 za udhalilishaji dhidi ya wanawake, watoto na vijana wa kiume vilevile takwimu hizo zinaonyesha kwamba mkoa wa Kaskazini Unguja unaongoza kwa vitendo vya udhalilishaji.

Mwaka 2017 zilifunguliwa kesi 105 za udhalilishaji wa wanawake pamoja na watoto visiwani zanzibar ambapo kati ya kesi hizo, 57 zilikamilika na kutolewa hukumu.

Asilimia 81% ya kesi zote zilizosajiliwa mwaka jana zilikuwa za kubaka.Mzuri Issa ambaye ni mkurugenzi wa TAMWA Visiwani Zanzibar alieleza kuwa hali si shwari

''Vitendo vya ukatili vinafedhehesha kwa miaka mingi. Zanzibar iliangaliwa kuwa yenye ustaarabu wa hali ya juu na yenye kufuata misingi ya dini lakini vitendo hivi vimekuwepo kwa muda mrefu na vinaongezeka''

Wakati wananchi katika ngazi tofauti wakilalamikia sheria kuwa haziko rafiki kwa waathirika wa vitendo vya udhalilishaji, sasa watakaotuhumiwa kudhalilisha wanawake na watoto wakifikishwa mahakamani hawatapewa dhamana na wakikutwa na hatia adhabu imeongezeka kwa kila ngazi ya mahakama na hii ni kwa mujibu wa chapisho lililotolewa na TAMWA la Mwezi Aprili mwaka huu.

Chanzo: BBC

Mara mwizi mzigo umeng'ang'ania mgongoni
Mara watapigwa kama mbwa koko..
Mara...
Ni shidaaaa...
 
Back
Top Bottom