Polisi Marekani wakamata gari lililokuwa na mabomu karibu na jengo la bunge wakati wafuasi wa Trump walipofanya vurugu

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Polisi nchini Marekani wanasema wamekamata gari lililokuwa na mabomu na bunduki likiwa limeegeshwa karibu na jengo la bunge siku ya Jumatano wakati wafuasi wa Rais Donald Trump walipovamia jengo la bunge, mtandao wa CNN umeripoti.

Mtu mwingine aliingia ndani ya jengo la bunge akiwa na bunduki na risasi zaidi ya mia moja huku akiwaambia wenzake kuwa anataka kumpiga risasi Spika Nancy Pelosi.

Haya ni baadhi ya mambo yanayoendelea kujitokeza wakati uchunguzi wa polisi ukiendelea kuhusu tukio la siku ya Jumatano la kuvamiwa kwa jengo la bunge wakati kikao cha kumuidhinisha Joe Biden kikiendelea.

Watu watano wamepoteza maisha, akiwemo mwanamke mmoja aliyetaka kuingia kwa nguvu ndani ya ukumbi wa mikutano wa jengo hilo la bunge, pamoja na polisi mmoja aliyefariki akiwa hospitali kuuguza majeraha yaliyotokana na kuvamiwa na kundi la wafuasi wa Rais Donald Trump walipokuwa wakitumia nguvu kupita vizingiti vya polisi waliokuwa wakilinda eneo hilo. Watu wengine 67 wamekamatwa huku 13 wakifunguliwa mashtaka kufuatia tukio hilo.

Taarifa zaidi kuhusu vifaa vilivyokuwepo ndani ya gari lililokuwa na vilipuzi lililokuwa limeegeshwa takriban mitaa miwili kutoka eneo la jengo la bunge hazijawekwa wazi katika taarifa ya polisi, huku mtu mmoja mwenyeji wa jimbo la Alabama aliyetambulika kwa jina la Lonnie Leroy Coffman akishikiliwa na polisi. Kikosi cha kutegua mabomu kimesema kuwa mabomu kadhaa pia yamegunduliwa katika maeneo mbalimbali ya mji wa Washington DC.

Mtu mwingine ametiwa mbaroni kwa tuhuma za kutuma ujumbe mfupi kusema kuwa anataka kumpiga risasi spika wa bunge, Nancy Pelosi. Cleveland Grover Meredith, Jr., aliyefika Washington DC siku moja kabla ya tukio la siku ya Jumatano alimtumia ujumbe mfupi mwenzake akisema kuwa anataka "kumpiga risasi [Pelosi] kichwani wakati matangazo mubashara ya televisheni yakiendelea" huku katika ujumbe mwingine akisema kuwa anaenda Washington akiwa na silaha za kutosha. Polisi wamesema kuwa Meredith alipamba ujumbe wake kwa kutumia 'emoji' za shetani huku akitumia maneno yanayoashiria viungo vya mwili wa mwanamke kumtaja Spika Pelosi.

Tukio la siku ya Jumatano limeibua wasiwasi mkubwa kuhusu uthabiti wa ulinzi katika majengo ya serikali ya Marekani, hali iliyopelekea baadhi ya nchi kupitia hali ya usalama wa majengo yao, ikiwamo bunge la Ubelgiji.

Tayari baadhi ya wanasiasa wa Demokrat wameonesha nia ya kutaka kumuondoa Rais Trump madarakani kwa nguvu, huku mitandao ya kijamii kama vile Twitter ikifungia akaunti zake kwa kile kilichotajwa kama kuchapisha maudhui yanayochochea mgawanyiko.
 
Hiyo nchi siku kikinuka itageuka majivu kabisa! Maana kule kila mtu ana binduki yake.
 
...hao wafuasi wa Trump washtakiwe kwa 'ugaidi', ili waone sifa ya kuitwa hivyo.
 
Issue yao haihusiani na chanzo chochote cha vita yoyote ya Dunia.
Hao jamaa ni kama kama sehem ambayo isha mwagiwa petrol, apo anangojewa msela wowote akatize na sigara yake palipuke.

Wasipo mtuliza huyo Trump, wenda ndio akawa msela mwenyewe anae subiliwa.
Sio uoga mdogo wangu ..popote alipo mzungu lazima amani itawale ..sasa wakizichapa wao ujue hakuna maisha tena angalia vita vya dunia mdogo wangu
 
Back
Top Bottom