Polisi kuwakamata wabunge wa CHADEMA waliokatwa mapanga!

Polisi wasilete usiasa wao hapa, wanapaswa kuwakamata watuhumiwa waliowafanyia fujo hawa waheshimiwa. Kama ni maelezo toka kwa hawa wabunge, yatatoka baada ya wao kupona.
 
kwa maoni yangu mimi nahisi ukombozi umefika,kwani damu inayomwagika kutetea haki hushinda daima,lakini pia sipati picha kama na sisi tusiofurahishwa na ujambazi kama huu tutaamua kulipa kisasi kwa viongozi wa ccm.Mungu yupo na ccm imeshakufa,tunasubiri cku ya maziko tu!!! poleni sana wahanga

Hawa wabunge walijitakia wenyewe, waliisha ambiwa mwisho wa kampeni ni saa 12 , wao saa 6 usiku wanafanya kampeni kilicho wapata ndicho hicho vijana wenye kulinda sheria wakawa GECHA
 
Ama kweli kazi ya UKOMBOZI ndiyo imeanza!

Maana kwa maono yangu binafsi nasema na naapa ya kwmb ccm ni JANGA kubwa kwa Taifa letu la leo!

mafisadi walichotenda kwa hawa MAKAMANDA wa CDM hakika malipo ni hapa hapa na haita chelewa hapa punje!

Haiwezekani!!
 
Sipati picha nzuri kuhusu hii kauli ya RCO anatumia nini kufikilia au Masaburi watu wako hospitali bado unatoa kauli za hovyo kiasi hicho subiri M4C sijui utakimbilia wapi.

Mimi nafikili kitu cha kufanya hapa ni kumuhamisha kamanda aende kituo kingine, na itakuwa even better wakikaa kimya hili IGP afanye uchunguzi wake kimya kimya na kubaini ukweli, swala hili lipuuziwa lita set a very BAD precedence. Wakumbuke kwamba mambo haya yanasomwa na kila mtu duniani na tuna Mabarozi wa nchi rafiki TANZANIA, ninacho waomba POLISI wasije kufanya mambo ya kumdhalilisha Raisi wetu Mh. J.M.Kikwete kwa kuwakamata wabuge kwa kisingizio chochote kile to save their skin.

Msifanye mambo ambayo DUNIA itatushangaa na kusema kumbe BUZZ WORD ya Tanzania ni kisiwa cha AMANI ni hadaa tupu na Raisi wetu akaonekana inakuwaje TANZANIA imeweza kusuruhisha mapigano ya Kenya lakini kwao panafuka moshi, msimdhalilishe JK kwenye International Community anako heshimiwa sana kwa busara ZAKE.
 
Alisema baada ya kupata taarifa hizo, muda mfupi polisi walifanikiwa kufika eneo la tukio na kuwakuta wabunge hao ambao wakiwa wamewekwa chini ya ulinzi na wafuasi hao wa CCM, ambapo polisi walipambana na kufanikiwa kuwaokoa.

Halafu kama waliwakuta wahalifu wahalifu wakaambiwaje, mko chini ya ulinzi au kimbieni? Sielewi.
 
Sina imani na hawa polisi. Sasa siku tutakapopewa ridhaa na wananchi kuchukua dola sijui watajificha wapi!
 
Kwani mwisho wa kutembea usiku Tanzania bila kuvunja sheria ni saa ngapi? Kwani kutembea usiku tunahitaji kuwa na vibali vya polisi? Polisi acheni maneno yenu bwana.

Na ni nani aliyotoa taarifa ya kuvamiwa kwa Wabunge Polisi? Wavamizi au waliovamiwa?
Polis wetu bana, hovyo kabisa, hawaamini hata kidogo na ndo maana siku hizi haishangazi wananchi kuchukua sheria mkononi.

Wenye hekima hapa watagundua Polisi ndo wanataka kujiondoa kwenye lawama lakini hapa hawachomoki.
 
Tatizo la polisi kuhojiwa akiwa under influence of viroba. This is strange, mlalamikaji awe arrested kwa kosa aliloripoti kabla hata polisi hawajakamata suspects? Assumption za RCO zinatoka wapi na zimebase kwenye Nini?

Hivi huyo RCO alikuwepo Mwanza wakati wa uchaguzi wa 2010? Au anataka kujaribu muziki wa wana Mwanza 2010 kuwa akiamini kuwa sasa ana ubavu zaidi ya ule wa 2010? Nahisi huyu RCO alikuwa hajapelekwa Mwanza wakati huo.
Yetu macho na masikio.
 
policcm at work! Good work I-G-Pel maana shemeji utamtupaje bana!!!
 
Hawa wabunge walijitakia wenyewe, waliisha ambiwa mwisho wa kampeni ni saa 12 , wao saa 6 usiku wanafanya kampeni kilicho wapata ndicho hicho vijana wenye kulinda sheria wakawa GECHA

Akili ni nywele kila mtu ana zake! Walao ungesema Wabunge na majambazi walikutwa wanavunya nyumba usiku wa MANANE kidogo ningekuelewa. Eti vijana wa kulinda sheria, unajua sheria ni kitu gani?-kwani kuna sheria unayo ruhusu kumchabanga Raia kwa kutumia mapanga na shoka na kumbuka si raia wakawaida ni mbunge anaye husika na utungaji wa sheria unazo zungumzia!

Toka lini Tanzania tukawa na Vigillante - kwani kazi ya Polisi ni nini? vijana wasitumike vibaya kwa kufanya uvunjivu wa AMANI kwa faida ya watu wachache wenye agenda zao za SIRI. CCM na Serikali yake haiwezi kuhamrisha watu wawajeluhi wengine, haya ni mahamuzi ya watu binafsi tu CCM na Serikali yake haiwezi ku-condone kitu kama hicho - nina uhakika ninacho zungumza hapa.
 
Hawa wabunge walijitakia wenyewe, waliisha ambiwa mwisho wa kampeni ni saa 12 , wao saa 6 usiku wanafanya kampeni kilicho wapata ndicho hicho vijana wenye kulinda sheria wakawa GECHA

Kilaza naona unakonda kama mnazi kwa mapenzi uiyonayo kwa magamba!!! Upo lakini?
 


“Hawa wabunge lazima tuwakamate watueleze vizuri kuhusiana na tukio la kukatwa kwao mapanga usiku. Watueleze kwa nini walienda huko Kabuholo gizani usiku tena bila kutoa taarifa polisi?.


Nipo nje ya TZ kwa miezi 4 sasa;hivi Bunge lilipitisha mswaada na Rais akasaini sheria inayosema Mbunge akitaka kwenda sehemu hasa usiku lzm awajulishe Polisi?

Waziri Malima aliibiwa hotelini Morogoro nae aliwataarifu polisi sehemu alipo?
 
Hii ndo moja ya kazi aliyofanya lema arusha...polisi huku wana heshima na wananchi,,,,waulizeni polisi wa mafunzo walioingia arusha kwa pupa...walifika shemu moja inaitwa olmategoo,,yaliwakuta makubwa
 
wakuu ndio leo narudi kutoka ban nakutana na kichefuchefu hiki naomba kwanza wadau wote niwapongeze kwa kutujuza yalioendelea kipindi chote cha uchaguzi pili namuomba dr awaongeze kwenye orodha ya kuwashugulikia hao viongozi wa policcm wa mwanza baada ya uuuuuuuuuuuuuchaguzi 2015
 
Hawa wabunge walijitakia wenyewe, waliisha ambiwa mwisho wa kampeni ni saa 12 , wao saa 6 usiku wanafanya kampeni kilicho wapata ndicho hicho vijana wenye kulinda sheria wakawa GECHA
we tahira unayejiita genius matope walikuambia hao wabunge walikuwa kwenye campaign muda huo au unadhani? shame on u hamtoki 2015
 
polisi wanawazakitotozaidi ETIKWANINI WALITEMBEA USIKU TENA BILAKUTOATAARIFA POLISI.MKUU WA UPELELEZI ANAONGEA UTUMBO.HOVYOOOOOOOOOOOOOOOO KUBWAJINGA
 
RCO Mkoa wa Mwanza unaweza kusema yote kuanzia asubuhi mpaka asubuhi nyingine lakini ukweli unabaki palepale kuwa police department ya Tanzania ina matatizo na imechafuka kiasi maelezo yako au poilisi mwingine mwenye cheo zaidi yako hayawezi kuwa hisopo ya kuifanya iwe safi. Hamhaminiki katika jamii ya Kitanzania na pia nyie wenyewe hamjiamini. Mesimama njia panda na msipojirekebisha saa yaja nchi hii itakuwa ni uwanja wa mapambano.

Mara ngapi tumeshuhudia majambazi wanavamia duka au nyumba ambayo iko umbali kidogo na kituo cha polisi. Sasa ni heshima gani mmebaki nayo kama kweli wezi, vibaka na majambazi wanaweza kudhubutu kufanya uhalifu machoni kwenu? Hamuoni kuwa sasa mnaogopwa tu kidogo lakini hamuheshimiwi?

Mara ngapi watu wanavunjiwa nyumba zao na magari yao na wezi na vibaka na wanatoweka na mali na vito vya thamani au aliyejeruhiwa anakuja kutoa taarifa polisi anaaza kuulizwa maswali utafikiri yeye ndiye mshukiwa? Na badala ya kwenda sehemu ya tukio na kufanya vipimo vya kuwasaida katika upelelezi wenu manishia kupokea maelezo toka kwa mtu aliyejeruhiwa. Kana kwamba hiyo ahaitoshi mnamwomba awape pesa ya mafuta ya gari la polisi au mnamwambia ni bovu yeye atoe gharama ya kokodi gari. Kipimo ni hicho. Asiyekuwa na uwezo mtamwambia nenda kamkamate mwizi wako au wezi uwalete polisi. Au unaambiwa wataje unaowahisi ndio wamekuibia baada ya siku moja hao nyumbani kwako wanakuja kukutukana kuwa umewataja polisi. Badala yake siku hizi mtu akiibiwa anajililia mweyewe kwani polisi imekuwa ni kijiwe cha umbea kuliko sehemu ya maada. Section iliyobaki inachacharika chini ya kivuli cha rushwa ni traffic polisi. Hawa watakudai usafiri kwenda kupima ajali ilipotokea, utamwonga atayeandika report ya awali, ukitoka vehicle iinspector atakwambia bila mimi, insurance haitakulipa. Utampa pesa akitoka hapo faili litaenda kwa mpelelezi atakwambia bila mimi unapelkwa mahakamani hata kama ulipalamia kichuguu gari likaumia utaambiwa una kesi ya kujibu, utatishwa na utaonekana wewe ni mwalifu. Utaambiwa hata adhabu ambayo hakimu atakupatia labda kifungi cha miezi sita. Ukiagalia muda utakaopoteza mahakamani maana na huko na polisi ni kiatu na kidole. Lazima pesa uiache hapo.

Hapa hatujaongelea siku hizi polisi fanya wao ndio watunga Sheria. Na sheria wanataka itekelezwe na mwananchi wa hali chini au chama cha upinzani. Wapinzani ndio wanajua virungu, risasi na maji ya washawasha. Hatujaona wala kusikia dhahama hiyo wameshushiwa CCM. CCM wao watatukana, watakiuka sheria na taratibu lakini huwezi ukasikia mkono dhalimu wa polisi umewashukia.

Kwa jinsi hii msije mkafikiri jamii inawaelewa au kuwapenda na msipojirekebish amkatimiza wajibu wenu kama polisi wa nchi nyingine heshima yenu katika jamii itatoweka, mtachukiwa na kudharauliwa. Mtaogopwa kwa sababu mna silaha na manjua kuzitumia lakini hamtaheshimiwa na kuenziwa.
 
Back
Top Bottom