Polisi kuwakamata wabunge wa CHADEMA waliokatwa mapanga! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi kuwakamata wabunge wa CHADEMA waliokatwa mapanga!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Invisible, Apr 2, 2012.

 1. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #1
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  CHANZO: Polisi kuwakamata wabunge wa CDM waliokatwa mapanga | Fikra Pevu | Kisima cha busara!

  JESHI la Polisi Mkoani Mwanza, limeanza kuonekana kutaka ‘kuwageuzia kibao' wabunge wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mkoani Mwanza, waliovamiwa na kukatwa mapanga na watu wanaodaiwa ni wafuasi wa CCM, kwani polisi wanatarajia kuwakamata wabunge hao kuhusiana na tukio la kukatwa kwao mapanga usiku wa kuamkia Jumapili ya Aprili mosi, 2012.

  [​IMG]
  Wabunge waliojeruhiwa, Kiwia na Machemli


  Siku hiyo, ilikua ni siku ya upigaji kura katika kata ya Kirumba mkoani Mwanza, ambako wabunge hao Highness Kiwia wa jimbo la Ilemela na Salvatori Machemli ambaye ni mbunge wa jimbo la Ukerewe walikuwa miongoni mwa viongozi waandamizi walioshiriki kampeni na mikakati ya chama hicho katika uchaguzi wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wao, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.

  Mgombea wa Chadema Dany Kahungu ameibuka na ushindi katika uchaguzi huo wa Udiwanai kata ya Kirumba.
  Polisi imesema, inaweza kuwakamata wabunge hao, wakiwa bado wamelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ya jijini Dar es Salaam wanakopatiwa matibabu, au inaweza kuwasubiri watoke hospitalini kisha iwakamate, huku wabunge hao wakiwashutumu polisi kuhusika na uvamizi huo kutokana na kushindwa kuchukua hatua kwa wahusika wanofahamika.

  [​IMG]
  Mbunge Kiwia akiwa amejeruhiwa mgongoni


  Mkuu wa Upelelezi wa Jinai (CID) wa Jeshi la polisi Mkoani Mwanza (RCO), Deusdedith Nsimeki, amesema, inabidi wabunge hao wahojiwe kwani ndiyo wanaweza kuwa chanzo na watuhumiwa wa kwanza katika ghasia hizo zilizotokea usiku wa kuamkia Aprili Mosi mwaka huu katika eneo la Ibanda Kabuholo, Kirumba jijini Mwanza.

  "Hawa wabunge lazima tuwakamate watueleze vizuri kuhusiana na tukio la kukatwa kwao mapanga usiku. Watueleze kwa nini walienda huko Kabuholo gizani usiku tena bila kutoa taarifa polisi?.

  "Kukatwa kwao mapanga isiwe sababu ya kutokamatwa na polisi, lazima tuwakamate tuwahoji. Inawezekana wabunge hawa ndiyo chanzo kikubwa katika kesi hii.

  "Tunaweza kuwakamata wakiwa wamelazwa hospitalini huko huko, au tukaamua kuwasubiri watoke hospitalini halafu tuwakamate!. Sheria zinaturuhusu sisi kumsomea mashtaka mtu yeyote hata kama kalala kitandani", alisema RCO Nsimeki ambapo alitania kwa kusema: "Unajua mtu anaweza kukutwa na mke wa mtu akakatwa mapanga na kichwa kikaning'inia, sasa utasema huyo mtu si chanzo?".

  Hata hivyo, mwandishi wa habari hizi alipomuuliza RCO Nsimeki iwapo kuna watu wamekamatwa na polisi kuhusiana na tukio hilo la wabunge kukatwa mapanga na kuumizwa sehemu mbali mbali za miili yao alisema, hakuna mtu hata mmoja aliyekamatwa hadi kufikia jana jioni.

  "Hatujakamata mtu yeyote kuhusiana na tukio hili. Lakini tulishaanza kazi yetu ya upelelezi na tutawakamata tu hilo halina tatizo", alisema Mkuu huyo wa Kitengo cha Upelelezi Makosa ya Jinai Mkoani Mwanza.

  Kitendo cha jeshi la polisi mkoani Mwanza kushindwa kuwakamata watuhumiwa wa tukio hilo, inaweza kuwashangaza watu wengi, ikizingatiwa na uzito wa tukio lenyewe.

  [​IMG]
  Majeraha zaidi katika kichwa cha Mbunge Kiwia

  Aprili Mosi mwaka huu, usiku wa kuamkia upigaji wa kura katika uchaguzi mdogo wa Kata ya Kirumba, wabunge hao walitekwa na kundi la watu wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa CCM, wakati wabunge hao na makada wengine wa Chadema wakidaiwa walikuwa wakiwasambaza mawakala wa chama chao kurudi majumbani kwa ajili ya kujiandaa kwenda kusimamia kura za mgombea wa Chadema Kata ya Kirumba, Dany Kahungu katika uchaguzi huo mdogo.

  Katika tukio hilo, Mbunge wa Ilemela, Kiwia ndiye aliyeumizwa zaidi kutokana na kupata majeraha makubwa sehemu mbali mbali za mwili wake ikiwemo sehemu ya kichwani na mgongoni, ambapo alilazimika kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando (BMC), ya jijini Mwanza kwa matibabu zaidi, huku Machemli akikimbizwa Sekou Toure.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow (RPC), aliwathibitishia waandishi wa habari juzi na kusema kwamba: "Ni kweli wabunge hao wamevamiwa na kujeruhiwa kwa mapanga usiku, na sisi tulipokea taarifa kuwa wafuasi wa CCM wamewateka na kuwaweka chini ya ulinzi wabunge watatu wa Chadema, Kiwia, Wenje na Machemli".

  Alisema baada ya kupata taarifa hizo, muda mfupi polisi walifanikiwa kufika eneo la tukio na kuwakuta wabunge hao ambao wakiwa wamewekwa chini ya ulinzi na wafuasi hao wa CCM, ambapo polisi walipambana na kufanikiwa kuwaokoa.

  Kamanda Barlow aliwataja majeruhi wengine watatu waliokimbizwa katika hospitali ya mkoa ya Sekou Toure na kulazwa kuwa ni pamoja na Haji Mkwenda (21), ambaye amevunjika mguu wa kulia, Judith Madaru (26), ambaye amechomwa kisu sehemu ya ziwa upande wa kushoto na Ivori Festo Machimba (26), ambaye amejeruhiwa kichwani na mdomoni.

  Alitaja namba za magari yaliyokutwa kwenye eneo la tukio kuwa ni pamoja na T 377 ARF linalomilikiwa na mbunge Kiwia, T 729 DAD linalomilikiwa na Mohamed Juma pamoja na T 397 ANU aina ya Land Cruiser ambalo mmiliki wake hakupatikana.

  Wabunge hao wamehamishiwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi, ambako hali zao zinaelezwa kuendelea vyema, huku wote wawili wakishangazwa na kitendo cha polisi kushindwa kuwakamata watuhumiwa.

  Katika maelezo yake mtandaoni, Zitto Kabwe alisema mmoja wa majeruhi ni kiongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) ambaye upo uwezekano wa kuwa alipigwa na wenzake katika vurugu hizo, na aliwaomba polisi kutomruhusu kutoka hospitalini.

  "Kuna mmoja wa majeruhi ambaye yupo hapa mwanzoni alisema yeye ni mtu wetu na ameumizwa pia. Imegundulika ni mtu wa UVCCM, Ahmed Mkilindi ambaye ndiye alikuwa anaongoza kikosi kilichowavamia kina Kiwia. Amepata jeraha mkononi (friendly fire?). Mwenyekiti wa CCM mkoa yupo hapa kaja kumwona. Nimewaambia Polisi mtu huyu asitolewe hospitali kinyemela bali atoe maelezo polisi kwanza. Huyu ni mtuhumiwa wa kwanza kabisa. Hali ya Kiwia sio nzuri sana. Anatakiwa kufanyiwa ct scan kuona athari aliyopata (maana kapigwa na shoka na mapanga kichwani). Bahati mbaya hapa Bugando kifaa hicho hakifanyi kazi," alisema Zitto kabla ya wabunge hao kuhamishiwa Dar es Salaam.

  Zitto aliendelea kwa kusema, "Siasa za Tanzania zinazidi kujidhihirisha kuwa hazina tofauti na nchi nyingine za Kiafrika. Chama cha siasa kuwa na makundi ya wahuni na kupiga watu ni hatari na chama hicho kinakosa ‘moral' authority ya kutawala. Tusubiri uchunguzi zaidi wa Polisi. I am so depressed."


  Habari hii imeandikwa na Sitta Tumma – Mwanza na waandishi wa FikraPevu Dar es Salaam
   
 2. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  PoliCCM at work
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  Apr 2, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,791
  Trophy Points: 280
  Kwani mwisho wa kutembea usiku Tanzania bila kuvunja sheria ni saa ngapi? Kwani kutembea usiku tunahitaji kuwa na vibali vya polisi? Polisi acheni maneno yenu bwana.
   
 4. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #4
  Apr 2, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Naona baadhi ya watu wachache kwa kutumia jeshi la polisi wanataka kusababisha vurugu kila kona ya nchi hii,bado hawasomi tu alama za nyakati,yetu macho!
   
 5. kongomboli

  kongomboli Senior Member

  #5
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 154
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  kwa maoni yangu mimi nahisi ukombozi umefika,kwani damu inayomwagika kutetea haki hushinda daima,lakini pia sipati picha kama na sisi tusiofurahishwa na ujambazi kama huu tutaamua kulipa kisasi kwa viongozi wa ccm.Mungu yupo na ccm imeshakufa,tunasubiri cku ya maziko tu!!! poleni sana wahanga
   
 6. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #6
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  policeCCM at work shame on them
   
 7. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #7
  Apr 2, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kufanya kazi kwa maelekezo huko mkuu!kauli ya Nape leo juu ya sakata ili inaashiria kabisa kuna maelekezo yametoka ili kupindisha ukweli wa suala ili na hatimaye wahusika kutotiwa hatiani!hawa watu naona wanajaribu kupima akili na hasira za Watanzania,kama wanataka kuziona wataziona tu!
   
 8. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #8
  Apr 2, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sishangai polisi ccm kusema hivyo, kwani wapo kwaajili ya masilahi ya magamba lakini wafahamu kuwa wakazi wa mwanza hawatakubali uchafu huo. kama huyo RCO hajui nguvu ya umma ajaribu kuwafungulia mashitaka aone. labda awahoji na kuwaachia bila mashitaka.
   
 9. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #9
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,318
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  hivi kazi ya polisi ni kukamata tu ndio ionekane wanafanya kazi?
  Nembo yao imeandikwa usalama wa raia...
  Kama kuna tuhuma inatakiwa upelelezi wa kina hadi kundika charges,and then mahakama ndio hutoa haki au hatia..sasa wao wamekuwa ndo kila kitu...wanacommitt offence..hawatoi ulinzi...wanakamata...hawapelelezi...wanaongea kama wao ndio mahakama...wanatoa ushahidi wao nk nk
   
 10. Ngadu

  Ngadu Senior Member

  #10
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 10, 2009
  Messages: 123
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  policcm hamna haya!
   
 11. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #11
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,318
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  ile nidhamu ya kikoloni ambayo wameikariri eti kuwa mkubwa akisema basi ubnasema ndio afande...hata ukiambiwa ujisaidie juu ya meza kwa kuwa ni amri halali unatii huthanmini utu wako wala utashi wa kazi na matokeo ya utekelezaji wa amri hiyo
   
 12. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #12
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 332
  Trophy Points: 180
  Wawakamate haraka aisee...
  Hii itakuwa chachu ya kuibua hasira ya watz dhidi ya CCM na serikali,kwan kila nikikumbuka jinsi tukio lilivyotokea napandwa hasira na kutafuta nafas ya kulipiza kisasi.
  Bravo POLICCM!
   
 13. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #13
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,009
  Trophy Points: 280
  Polisiccm ama kwa hakika wana mpango wa kuiharibia serikali ya Jk, ionekane hovyo kuliko awamu zote tangu uhuru wa nchi hii. Ufanywe uchunguzi makini kubaini kama polisi wapo kwenye mgomo baridi maana jinsi jeshi hilo linavyoendeshwa kwa sasa hata mgombo wa nchini talibani wana nafuu.. Mungu tukomboe watanzania.
  .
   
 14. F

  FJM JF-Expert Member

  #14
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hiki ndicho kile alichoandika Dr Mwakyembe kwenye waraka wake kwamba ni polisi wa Tanzania (peke yao duniani) wanakaa ili mlalamikaji apeleke ushahidi! Hawa wabunge wawili wamekatwa na mapanga, badala ya jeshi la polisi kusaka watu waliofanya hilo tukio wanatangaza azma yao ya kuwakamata 'victims'!

  Kama taifa hii statement ya huyu afande inatulizimu kuhoji weledi wa jeshi la polisi Tanzania. Wanapata mafunzo ya aina gani? Wanaelewa wajibu wa polisi ni nini? Na je jeshi la polisi linafanya kazi kwa maslahi ya nani? Tayari wananchi wameshaonesha (kwa vitendo) kutokuamini jeshi la polisi ndio maana huko Arumeru Mashariki vijana wamebaki kwenye vituo vya kuigia kura ili ku-linda usalama wa kura zao! Hili jeshi la polisi liko kwa ajili ya nani?
   
 15. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #15
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Kwa kila tone la damu lililomwagika siku ile latalipwa hakika nawaambieni,Mungu awape tahafifu majeruhi wote,
  dawa yao polisi inachemka,hawa jamaa sijui wamefukizwa na nini
   
 16. L

  Lsk Senior Member

  #16
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 178
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ...IGP anapokuwa shemeji wa mwenyekiti wa Chama kinachoongoza nchi,wewe unategemea kuwa na Polisi wa aina gani?
   
 17. J

  Jqnakei Senior Member

  #17
  Apr 2, 2012
  Joined: Dec 23, 2011
  Messages: 121
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huko ni kucheza na akili zetu. Hii tabia haikubalika kuendelea kwny nchi yetu.
   
 18. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #18
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Its only in Tanzania where polisi wanauanika upuuzi wao in series

  Kazi imewashinda ya kulinda usalama wa raia, sasa wanataka raia wema wawaeleze kwanini waliinteract na wahalifu

  WHAT A SHAME...........
   
 19. BONGE BONGE

  BONGE BONGE JF-Expert Member

  #19
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 3,398
  Likes Received: 1,523
  Trophy Points: 280
  ......yale yale, MUNGIKI.
   
 20. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #20
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,273
  Trophy Points: 280
  Hivi wale wapiga nondo wa Mbeya wameishia wapi? nadhani ndio dawa ya hawa Polisi no compromise with Magamba.
   
Loading...