Polisi kuwaachia Wapemba

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
POLISI wamekubali kuwaachia kwa dhamana Wapemba inaowashikilia pamoja na kusisitiza kwamba kitendo cha wao/na yeyote kudai kujitenga kwa Wapemba ni kosa la Uvunjaji wa wazi wa KAtiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Katika ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Habari zaidi zinafuata
 
Last edited by a moderator:
Taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa Habari na Polisi, Makao Makuu leo hii.

PRESS RELEASE

Hivi karibuni Taifa limeshuhudia kauli mbalimbali za baadhi ya wananchi wa kutoka kisiwa cha Pemba hususan wafuasi wa chama cha CUF za kutaka kujitenga kutoka ndani ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iii waunde Serikali yao ya Pemba. Nia ya wananchi hao ya kutaka kujitenga, ilitolewa vile vile mbele ya Balozi wa Marekani hapa nchni wakati alipokitembelea kisiwa hicho. Baadaye tulishuhudia wananchi 12 wafuasi wa chama cha CUF na wakazi wa Pemba wakipeleka waraka wao wa kuomba wajitenge na Zanzibar kwenye ofisi za Umoja wa mataifa zilizoko Dar es Salaam.

Ufuatiliaji uliofanywa na Jeshi la Polisi umeonyesha kuwa harakati hizi za baadhi ya wananchi wa Pemba na ambao ni wafuasi wa chama cha CUF kutaka kujitenga na kuunda Serikali yao ya Pemba zimechochewa zaidi na uamuzi wa halmashauri Kuu ya CCM ilipoketi huko Butiama na kuelekeza kwamba suala la kuundwa kwa Serikali ya Mseto Zanzibar lirejeshwe kwa wananchi iii watoe maoni yao.

Si nia ya Jeshi la Polisi kujiingiza kwenye malumbano ya kisiasa yanayoendelea hapa nchini. Na wala hayo siyo majukumu yake. Hata hivyo malumbano yoyote ya kisiasa yanatakiwa yawe ya kistaarabu, ya kuvumiliana ya kupingana bila kupigana, na yasiyo na mwelekeo wa kuchochea vurugu, au uvunjaji wa amani.

Kwa ujumla, pamoja na haki ya kikatiba na kisheria ya kuendesha harakati za siasa za vyama vingi, haki hizo pia zina wajibu wake kwamba viongozi wetu wa vyama vya siasa pamoja na wafuasi hao, wana wajibu wa kuhakikisha kwamba wanatii na kuheshimu sheria za nchi.

Kitendo cha baadhi ya wafuasi wa CUF na wakazi wa Pemba cha kutaka kujitenga kutoka ndani ya Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ni cha uvunjwaji wa Katiba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Jeshi la Poslisi, likiwa ndicho chombo kinachosimamia na kulinda sheria za nchi, hali wezi kukaa kimya na kuendelea kushuhudia baadhi ya wananchi wakikiuka Katiba ya nchi ambayo ndiyo mhimili na msingi ya Demokrasia na amani tuliyonayo hapa nchini.

Kwa mantiki hiyo, tunawasihi wanasiasa wote hapa nchini waendeshe siasa zao kwa misingi iliyowekwa na Katiba na sheria za nchi. Nje ya hapo ni ukiukwaji na uvunjaji wa sheria za nchi.

Kwa ajili hiyo, nia au matakwa yoyote, pamoja na harakati zozote zinazofanywa za kisiwa cha Pemba kutaka kujitenga kutoka ndani ya Serikali ya mapinduzi Zanzibar kina lengo la kutaka kuathiri na kuvuruga Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ndiyo imeundwa na Katiba. Kitendo hicho ni cha uhaini.

Kwa hali hiyo, Jeshi la Polisi limeanza kuchukua hatua za kisheria za kuwakamata na kuwahoji watu wote wanaotajwa kujihusisha na njama hizo iii wachukuliwe hatua za kisheria.

Kwa mara nyingine, tunawasihi viongozi wote wa kisiasa, pamoja na wafuasi wao wajenge utamaduni wa kuheshimu na kuzingatia sheria za nchi, pamoja na kuzitumia katika madai yoyote pale wanapodhani hawakutendewa haki. Huo ndiyo utawala wa sheria.

Ahsanteni sana.

S.A. MWEMA

INSPEKTA JENERALI WA POLlSI
 
Jamani hao wazeee walijua wanachokifanya lakini???maana ile ni kisiwa kilichomo ndani ya jamhuri halali kabisa ambayo yatambuliwa hata Un ....sasa walichokitaka wao mi nakiona kama ni kosa ingawa sio uhaini.....moja kwa moja
 
POLISI wamekubali kuwaachia kwa dhamana Wapemba inaowashikilia pamoja na kusisitiza kwamba kitendo cha wao/na yeyote kudai kujitenga kwa Wapemba ni kosa la Uvunjaji wa wazi wa KAtiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Katika ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kumekucha; nguvu ya umma sasa inafanya kazi!!
 
Jamani hao wazeee walijua wanachokifanya lakini???maana ile ni kisiwa kilichomo ndani ya jamhuri halali kabisa ambayo yatambuliwa hata Un ....sasa walichokitaka wao mi nakiona kama ni kosa ingawa sio uhaini.....moja kwa moja
Mzee wa Skills, nadhani walichofanya hawa wazee ni KUWEKA MAWAZO YAO KWENYE KARATASI. Yanaweza kuwa mawazo ya wengi ama wachache japokuwa haipotei ile maana kwamba yanabaki kuwa mawazo.

Monks wa TIBETI walifanya fujo wala hawakuandika Barua lakini Dunia nzima ilipata ujumbe wa nini kinaendelea. Hawa wazee wametumia niia ya kistarabu zaidi
 
Yaani Katiba is supreme when it suits them? Hakuna Jaji anayeweza kuwa convict hawa kwa ushahiddi wa kwenda UNDP?
 
Polisi imekubali kuwaachia kwa dhamana watu saba waliokamatwa kwa tuhuma za kutaka Pemba ijitenge.

IGP Saidi Mwema, amesema kwamba watawaachia baada ya kufanya nao mahojiano ili waweze kuendelea na upelelezi.

Mwema alisema kwamba baada ya taarifa kadhaa kupatikana wamewahoji watu wengine zaidi, lakini alikataa kutaja idadi yao wala mahali walipo.

Watuhumiwa wote wanatajwa kuwa wafuasi wa Chama cha CUF,

Mwema alisema ikiwa mtu anataka Moshi iwe nchi, kwa ajili ya Wachaga na Wapare anakua anavunja katiba.

IGP anasema taratibu zote za kisheria zimezingatiwa katika kuwakamata, kuwahoji na hata kuwaachia kwa dhamana.

Ameasema baada ya upelelezi kukamilika, majalada yatapelekwa kwa DPP ili kuona kama kuna ushahidi utakaowezesha kushitakiwa kwa watuhumiwa hao kwa makosa kadhaa ikiwa ni pamoja na uhaini, au uvunjani amani ama vyote kwa pamoja au mashitaka mengineyo kwa kuzingatia ushahidi wa kisheria utakaoonekana. Upo pia uwezekano wa kuachiwa huru na kufutiwa kesi ikiwa hakutakua na ushahidi wa kutosha.
 
Vigeu geu wakubwa.... kama watu walitaka kujitenga na kuvunja sheria kwa nini tena unawaachia? Hii inamaanisha kuwa huu ni usanii na upuuzi tu unaendelea hapa.
 
Ushindi Mwingine wa Kwanza Wa Jamii forums,Haya yote ni baada ya jana Jk kukomaliwa na wale Wahisahani,hasa Mkuu wa Nchi za EU,nadhani alikuja na ujumbe mzito

Kulikuwa hakuna haja ya kuwashikilia hawa watu,cha msingi ni wakati umefika kwa wale wahafidhina kukubali mapendekezo ya rasimu ya makubaliano.
 
Hiki ndicho tulichokuwa tunakisubilia kweli nguvu ya umma tunaona inavyo fanya kazi....mapambano yaendelee....
 
Wa Jamii forums,Haya yote ni baada ya jana Jk kukomaliwa na wale Wahisahani,hasa Mkuu wa Nchi za EU,nadhani alikuja na ujumbe mzito

Kulikuwa hakuna haja ya kuwashikilia hawa watu,cha msingi ni wakati umefika kwa wale wahafidhina kukubali mapendekezo ya rasimu ya makubaliano.

haiwezekani kuwa Ushindi Mwingine wa Kwanza
 
Kilichotokea si tu ni UJUMBE bali ni ALAMA ZA NYAKATI, kumbukeni headline za Raia Mwema;

"CCM Mambo Mazito"
http://www.raiamwema.co.tz/08/02/06/index.php
na
"Nchi inayumba" http://www.raiamwema.co.tz/08/04/16/index.php

Yote haya ni mambo ambayo yana maana kubwa kwetu kama Taifa.
HADI SASA HALI SI NZURI HATA KIDOGO KWA CCM, SERIKALI NA WATAWALA

Mfa maji hakosi kutapa.

Naomba kujua, hii press relese iliotolewa na jeshi la polisi ni ya kwanza toka sakata la kuwakamata lianze?
 
Mimi naona Jeshi la Polisi limeliona hili kama siyo serious sana baada ya kuwahoji wazee maskini kutoka Pemba .Na pamoja na shinikizo za JF na wakulu wa West kufanya kazi,pia kuna nia nzuri ya Rais katika kujaribu kuutatua mwiba wa Zanzibar.Bila kuwa na nia hiyo isingekuwa rahisi kuwaachia na badala yake ingekuwa ni kamata kamata nyingine na brutal repression ikiongozwa na Polisi katika nchi nzima dhidi ya Wapemba.Busara za JK hapo nazifagilia.Hakuna mauaji na badala yake ni invitation ya kuaa pamoja na kujadili mambo mezani.Kiongozi anatakiwa kuwa hivyo na hapo natoa big up kwa Serikali.
 
Hizi ni hoja zisizo na msingi:

a. Jamii ya watu ambao wanaishi katika mashaka na hawana usalama katika eneo lolote lile la ardhi ya dunia wanayo haki ya kibinadamu kutafuta mahali pao ambao watakuwa huru kuwa binadamu.

b. Wakati wowote jamii ya watu inanyanyaswa, kuteswa au kutendewa kama nusu binadamu au nusu raia jamii hiyo ina haki ya kutafuta hifadhi mahali popote ambapo wanaweza kupaita ni pao.

c. Jamii ya watu ambao wako ndani ya nchi moja endapo wanajiona kuwa katika nchi hiyo hawatendewi sawa, hawana haki sawa, wananyanyaswa, wananyimwa nafasi ya kunusuru maisha na mali zao na kwa namna moja au nyingi wanatengwa na utawala wa Taifa basi jamii hiyo inayo haki ya kimsingi ya kujitenga na jamhuri au nchi hiyo.

- Wayahudi walipokuwa wanateswa wakati wa vita ya pili ya dunia na kwa muda mrefu wakiteswa na kufanywa duni sehemu mbalimbali duniani, walifikia mahali pa kuamua kujenga Taifa lao, mahali pekee ambapo wanaweza kupaita pao. Ndio mwanzo wa kuundwa kwa Taifa la Israeli baada ya vita ya 1948. Leo hii ni miaka 60 baadaya kuundwa kwa Taifa hilo.

- Watumwa waliokamatwa katika ile meli ya Amistad na kuletwa marekani kwa nguvu walitetea haki yao ya kuwa binadamu na ya kuwa walikuwa na kwao na hivyo kitendo cha kuwakamata kwa nguvu kilikuwa ni kinyume na haki ya watu hao kuishi kwa usalama wa maisha yao. Mahakama Kuu ya Marekani ilikubali na kuwaachilia.

- Wakurdi wa Iraq ambao waliishi katika mateso chini ya utawala wa Saadam kwa muda mrefu wamekuwa wakijitahidi kujitenga ili wawe huru kuishi kama binadamu na raia huru. Licha ya jitihada za Sadam kuwafunga na kuwaua mawazo ya wao kuwa na kwao hayakukoma. Na kwa muda mrefu wamekuwa wakijitahidi kujenga utawala wao. Na sasa hivi eneo la Kurdistan ambako Wakurdi wa Iraq ingawa ni sehemu ya nchi ya Iraq wanajiendeshea mambo yao katika shirikisho la Iraq lakini wakiwa na serikali yao na viongozi wao.

- Taifa la Marekani liliamua kujitangazia uhuru wake toka Dola ya Muingereza baada ya kutoa malalamiko yao (soma declaration of independence) na malalamiko hayo kutofanyiwa kazi na Mfalme. Walifanya hivyo ili wawe na sehemu ambayo wako huru kuamua mambo yao kwani mfalme hakuwa tayari kuwasikiliza. Kujitangaza kwao huko kulisababisha vita iliyozaa uhuru Julai 4, 1776.

- Biafra, wananchi wa Nigeria wa kabila la Igbo na makabila madogomadogo yanayohusiana nayo waliamua kujitoa katika shirikisho la Nigeria na kutangaza uhuru wao na taifa lao. Tanzania ilikuwa miongoni mwa nchi kama tano zilizotambua Taifa hilo jipya kwa misingi niliyoisema hapo juu. Kwa Wanigeria ilikuwa ni kitendo cha uhaini lakini kwa wa Igbo ilikuwa ni kitendo cha kulinda maisha yao na ya watoto na uzao wao. Baada ya muda si mrefu Biafra ikalazimishwa kusalimu amri na kurudishwa kwa nguvu kwenye Shirikisho. Hata hivyo hisia ya kutaka kuwa huru bado ipo na vizazi vya wa Igbo bado wanasimuliana juu ya njozi hiyo ya kuwa watu huru.

Nina mifano mingine ambayo nitaicha pembeni kwa wakati huu.

Ninachosema ni kuwa suala la Pemba si suala la uvunjaji wa sheria au Katiba per se. Ni suala la watu na jamii ya watu kuwa na mawazo ya kujitenga. Huwezi kuwalazimisha watu ati watii katiba wakati Katiba iliyopo inatumika kuwakandamiza, kuwatenda au kwa namna yoyote kuwafanya wawe duni.

Mwanadamu anayo haki ya kutii dhamira yake zaidi, utu wake, na haki yake kama mwanadamu na raia kuliko kutii sheria ambayo inatishia dhamiri, utu, au haki hiyo. Ndugu zetu wa Zanzibar wana madai tena mazito. Madai hayo ambayo yamekuwa yakitolewa mara nyingi kwa maoni yao yamepuuzwa na kutofuatiliwa. Kitendo cha kuwakamata sasa kinaendeleza mwelekeo huo huo kwamba lazima wapemba waconform kimawazo to the majority. Hili haliwezekani.

Matatizo ya wa Pemba ni matatizo ambayo yanahitaji kutambulika kwa kanuni kadhaa ili kuweza kuyatatua. Kutoa tishio la sheria au nguvu za dola ni udhaifu mkubwa kwani hakuna dola iliyowahi kuzima mawazo ya uhuru, au kutia pingu fikra za mabadiliko. Walishindwa wajerumani, walishindwa Waingereza, walishindwa Afrika Kusini, Alishindwa Mussolini, alishindwa Sadam, alishindwa Stalini, na kwa hakika atashindwa Mwema na Kikwete.

Kama mbegu ya kutaka kuheshimika na kutambulika utu wao imepandwa katika wapembwa hakuna atakayeweza kuizima. Hiyo ndio hali halisi.

Jukumu letu basi ni nini? Je tukubali wapemba wajitenge kwa sababu tumeshindwa kuwasikiliza? Je tuache sehemu ya Jamhuri yetu kujitenga kwa sababu wanasiasa wamekuwa goigoi kufikiri na wa wazito kutatua matatizo yao. La hasha!

Mimi binafsi kama mpenzi wa Muungano wetu na nikiwa mwanafunzi mzuri wa Mwalimu sioni jambo lililoshindikana. Ni wito wa kila mtanzania kuulinda, kuuenzi na kuutetea Muungano na Jamhuri yetu na hatuwezi kuacha jamii ya watu itishie muungano huo. Haiwezekani kikundi cha watu kikatae kusikiliza matatizo ya ndugu zetu wa Pemba hadi kuwalazimisha kutaka kujitenga.

Swali langu?

Je, utawala wa serikali ya CCM wamefanya juhudi gani za kushughulikia matatizo yanayotajwa na Wapemba? Muafaka siyo juhudi za kweli kwani hilo linahusu utawala na mambo ya siasa na hakuna ajenga ya hali ya wananchi wa Pemba au malalamiko yao. Je kwa vile Pemba wengi ni CUF ina maana serikali tawala haitakiwi kuonesha juhudi za kuheshimu maamuzi ya wananchi wa huko?

Ndugu zangu ipo njia ya haki, yenye usawa na yenye umoja. Njia ambayo itaweza kuondoa hisia hizi na kuzizika mara moja.

a. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, iangalie katika uongozi wake ina wananchi wangapi kutoka Pemba. Je ni lazima mtu awe CCM ndio apewe nafasi ya uongozi? Kama Pemba imetoa wabunge wengi tu kwanini wasiingizwe kwenye serikali? Hili halihitaji kura ya maoni linahitaji akili. Huwezi kushinda kwa asilimia 53 halafu ukaishi kama umeshinda kwa asilimia 90! SMZ ilipaswa mara baada ya uchaguzi kukaa chini na CUF na kupanga mkakati wa kushirikiana.

b. Rais Kikwete badala ya kuchagua wakuu wa mikoa na wilaya za Pemba toka CCM angechagua kutoka CUF na hata viongozi wengine angewachanganya wa CUF pia. Hilo halihusu sera au katiba ni suala la akili tu. Kwanini hakufanya hivyo wakati anajua kabisa kuwa Pemba ni kwa kiasi kikubwa mashabiki wa CUF. Angeweza hata kuunda ushirikiano wa aina fulani kati ya viongozi wa CCM na CUF kule Pemba. Lakini hakufanya hivyo.

c. Serikali iwaachilie wananchi hawa mara moja na kukaa meza moja na kuwasikiliza. Tusiingie kwenye mtego wa kufungana kwa mambo haya kwani tutaanza kutengeneza wafungwa wa kisiasa na kuanza kupandikiza zaidi fikra za mapambano. Tusiingie kwenye mtego huo. Serikali ifute madai yake, itengeneze timu ya ushirikiano (nje ya mazingaombwe ya muafaka) na kuamua kwa makusudi kabisa kuwashirikisha wananchi wa Pemba katika maamuzi na utawala. Walikipanda wenyewe, sasa wasishangae wanavuna miiba!

d. Viongozi wa CUF watangaze hadharani kuwa lengo lao si kuvunja muungano au kutangaza Taifa huru bali wanataka nafasi ya kutambuliwa na kuthaminiwa kama raia kamili wa jamhuri yetu. Maneno ambayo yamewahi kusikika ya "Mwarabu hatotawala Zanzibar" wakati mwarabu huyo ni raia ni maneno yanayowafanya waarabu wa eneo letu kuwa nusu raia. Leo hii Botswana inatawaliwa na raia ambaye baba ni mweusi na mama ni mzungu! Sisi tunahangaika na mambo ya ajabu ya nasaba! Leo Marekani inaweza kujikuta ikitawaliwa na kiongozi ambaye baba yake ni mweusi na mama ni mzungu! sisi tunashindana na alilala na Sultani na nani na kijakazi!

Ndugu zangu watanzania, matatizo ya Zanzibar yanatatulika na wala hayahitaji mkono mkubwa wa dola ili kuyamaliza. Yanahitaji utashi wa kisiasa, ushirikiano wa kuaminiana na moyo wa udugu. Watawala wa Zanzibar lazima wakubali kwa vitendo kuwa Wapemba ni wananchi sawa na wale wa Unguja na wanahaki sawa katika Taifa hilo bila kuangalia nasaba zao, historia zao n.k Na hili lazima lichukuliwe hadi kwenye serikali kuu. Kujifanya ati tunawakamata na kuwatia pingu na kuwatishia ni kitendo kilichofanywa na serikali ya makaburu na no sir, hatuwezi kuacha serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar kuanza kutenda kama serikali za makaburu au za kibaguzi.

That is my argument and I'm sticking to it.

M. M.
 
Ni sahihi kabisa kuwaachia wapemba waliokuwa wamewekwa ndani. Lakini hilo tu halitoshi. Kitendo cha kumuweka mtu ndani ni jambo zito. Hilo ni kosa kisheria "unlawful/wrongful confinement". Na kwa serikali kufanya makosa ya namna hiyo sidhani ni healthy, kwani nafasi ya kuchunguza kabla hawajawashika ilikuwepo. Huo kwa maoni yangu ni unyanyasaji na kutishia usalama wa raia, jambo ambalo si sahihi kabisa.

Kwa karne tuliyopo ni vyema serikali na vyombo vingine vya dola vikajifunza kufanya mambo kwa uelewa, umakini na usahihi badala ya kutumia nguvu. Hiyo inasababisha malumbano ya mara kwa mara ambayo si lazima pamoja na kwamba misuguano na malumbano nyakati zingine huboresha mambo. Hiyo inaongeza chuki zisizo za msingi na inaijengea serikali dharau ambayo si lazima. Kama kiongozi si vizuri kuwa na maamuzi ya jazba. Si sahihi kuonyesha udhaifu kiasi hicho. Watu wameandika tu barua na kuipeleka UNDP unatishika je, wakikuambia toka ofisini itakuwaje? Ingekuwa vizuri serikali ikataka kujua lalamiko lao ni nini. Assuming hajui.

Kama kiongozi usitegemee watu wote watakubaliana na mawazo au siasa zako, hivyo ni vyema viongozi wakajifunza kukubali kutofautiana na kutafuta njia ya kuweza kuendelea kuishi pamoja na sio mmoja kumtisha mwingine kwa vile tu hawafikiri sawa au hawana maono sawa.

Vyombo mbali na makundi yenye kutetea haki za binadamu, ni vyema wakawa makini zaidi kufuatilia hili. Huu ni mwanzo tu. Kuna mengi yamewachosha wananchi. Hiyo ni Pemba tu ambayo population yake ni ndogo. Wanahamaki hivyo, haya wakija idadi kubwa zaidi itakuwaje?
 
Back
Top Bottom