Polisi kuungana kupanga njama za kuniua wakiungana na mtandao wa ufyatuaji noti bandia nchini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi kuungana kupanga njama za kuniua wakiungana na mtandao wa ufyatuaji noti bandia nchini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mushi ndesamburo, Apr 24, 2012.

 1. M

  Mushi ndesamburo New Member

  #1
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yahusu polisi kuhatarisha maisha yangu baada ya kushindwa kumdhibiti muhalifu ambae ni jambazi anayejulikana kwa kumlinda na kumpa nafasi ya kunishambulia mara kwa mara na kunisababishia hasara kubwa na kunisababishia kukimbia makazi yangu.

  Polisi hawa wanashirikiana na jambazi huyu mana nimekuwa nikiwataarifu mara kwa mara juu ya usalama wa maisha yangu ni askari wa jeshi la polisi naushaaidi upo nimewapa taarifa hizi viongozi wangazi za juu katika wizara hii juu ya swala hili lakuwindwa na mtandao huu ambao una husika na uchapishaji noti bandia hapa nchini na toa taarifa hii kwa jamii yote kuwa mtandao huu ni hatari sana na wanambinu nyingi zakuzoofisha mtu yeyote ambae atawabaini kwa matukio yao kwakutumia jeshi la polisi.

  Nina ushaidi wa kutosha na mtandao huu umetuhumiwa mara kwa mara kwa uhalifu na kesi nyingi zimefikishwa mahakama ya wilaya mbeya mjini kwa kuujumu uchumi na sasa mtandao wajambazi huyu wamenipa taarifa kuwa wiki hii wataniua najua taarifa hii ni ya kweli maana hata mwaka jana walinitumia ujumbe wa sms kwenye simu yangu kua wataniua baada ya siku chache. Baadae waliniteka kwa silaha nakunipola lakini wizara hii nimeipa taarifa hizi wala hawatoi tamko lolote nawakati wao ndio viongozi wangazi ya juu na usiku wakuamkia pasaka walinivamia askari kwa madai wametumiwa na mkuu wa kituo kunipeleka polisi usiku saa saba; kweli walikua askari nanilipoomba msaada kwa viongozi wa mtaa polisi hao walikimbia. Tulipowafuata kituoni asubuhi kukawa utata mkubwa na taarifa hii nilimpa afisa wa ngazi ya juu ndani ya jeshi la polisi lakini hakuna hatua yoyote iliochukuliwa nikampa taarifa kiongozi mkuu katika wizara hii lakini yuko kimya mpaka sasa najua wanaogopa kukichukulia hatua kikundi hiki lakini hata usalama wa maisha.

  Sababu za kuniwinda ni hizi hapa
  Mimi ninafanya biashara za nguo na kubadilisha fedha katika mji wa Tunduma Mbeya.

  Siku moja nikiwa safari nilikutana na bwana mmoja ambae alinisaidia kunibeba kwenye gari lake baada ya kukosa usafiri kutoka Iringa mpaka mbeya nikiwa kwenye gari lake aina ya prado yeye ni dereva aliniuliza jina langu na wapi naishi na kazi ninayofanya nilimweleza kua nauza nguo aina ya majins ila sikumueleza biashara yangu ya pili yakubadilisha fedha na yeye akajitambulisha kwa jina la Joseph Mawenzi anaishi Mbeya na akasema anafanya biashara ya nguo kama mimi ila yeye kuwa nguo huwa anazifuata Kenya kwenye kiwanda cha nguo hizo ikabidi ni nimuulize aina mbalimbali na bei zake akataja bei za chini sana ikabidi mwambie kua siku akiwa na mzigo aniite niuone.

  Siku chache baadae alipiga simu kwa namba tulizopeana akaniambia tayari anamzingo na analeta Tunduma niuone alileta mzigo huo dukani kwangu kwa bei zile alizonitajia nikamkabizi hela akaondoka wiki moja baadae alinipigia simu kuwa ameleta mzigo mwingine nikamwambia kuwa mimi sipo niko arusha ila upeleke mzigo huo tunduma dukani kwangu yupo kijana wangu nitampigia simu aupokee mzigo huo na hakupe hela alipofika dukani kwangu akatumia mbinu zake kumlaghai kijana wangu kwauaminifu wa kibiashara akamwambia gari ameliacha mbali kidogo ampe milioni tatu ili akamkabidhi huo mzigo kijana alipomkabili pesa kulingana na uaminifu wa mzigo wa kwaza wakaondoka mpaka alipoacha gari huko kwenye gari lake alimuacha kijana mmoja ambae walipofika tu kwenye gari lake yule kijana akawaeleza kuwa ule mzigo ameuuza kwa mtu mwingine.

  Yule bwana Jose akanipigia simu akaniambia kuwa samahana ndugu ule mzigo nimekuta mdogo wangu amehuuza samahani naomba niondoke na mdogo wako akachukuwe mzigo mwingine Mbeya kwakua tayari alikuwa ashachukuwa pesa zangu milioni 3 zangu mimi nikampigia simu mdogo wangu akaongozana nae mpaka Mbeya. Huko nako akamwambia kijana wangu kuwa hata mzigo wake mwingine aliouacha kule umeuzwa wote aliponitaarifu kwa simu taarifa hiyo nilimwambia amkabidhi pesa zangu mdogo wangu arudi Tunduma akaniambia kuwa pesa ameziingiza kwenye akaunti ya jamaa zake wa kiwanda akaniomba nikirudi safarini tuonane niliporuri kutoka safarini nikakutana nae akanipeleka.

  NO: 0655419915

  mushindesamburo@gmail.com
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Pole Ndesambulo,labda jina linawaogopesha.
   
 3. sosoliso

  sosoliso JF-Expert Member

  #3
  Apr 24, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 7,519
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  Duh kama haya ni kweli ndugu yangu itabidi uhame huko.. Hao Polisi wanaofanya vitendo hivyo wana roho za kijambazi so hawaoni shida kukumaliza..
   
 4. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #4
  Apr 24, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Polisi watasababisha watu wafiche majina yao ya ubini, badala yake watu kwa ajili ya kulinda maisha yao watalazimika kutumia majina yenye yatakayoishia na Kikwete, Lowassa, Mkwawa, Mkapa, Nyerere, nk. Ukipatikana jina linaishia na Ndesa, Slaa, Zitto, Mbowe, Lema, Lissu, Mnyika inakuwa tatizo
   
 5. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #5
  Apr 24, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Pole sana ndugu,ili jambo linaonekana ni very serious,ila kwa ushauri tu ni bora ungelitolea taarifa kwa ngazi za juu zaidi za jeshi la polisi,vyombo vya habari vingi na hata asasi zisizo za kiserikali mapema iwezekanavyo ili wajue kabisa njama zao zimegundulika,vinginevyo unaweza ukawa late na wakakumaliza kweli!ili jeshi letu la polisi kwa kiasi fulani limepoteza uadilifu kabisa,pole sana ndugu!
   
 6. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #6
  Apr 24, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Dah, Tanzania kisim? cha amani.
   
 7. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #7
  Apr 24, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Dah! pole sana kama ni kweli cha kukushauri tafuta gazeti linaloheshimika uwape habari hii ili ijulikane mapema kama alivyofanya Mwakyembe vinginevyo unaweza kupotea hivi hivi.
   
 8. akilimtindi

  akilimtindi JF-Expert Member

  #8
  Apr 24, 2012
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 423
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ndugu yangu Ndesamburo kwa sasa achana kabisa na maswala ya kuwafuata polisi kwa hili, peleka hii issue kwenye vyombo vikubwa vya habari na ikiwezekana tuma hii habari hata vyombo vya kimataifa ili walimwengu wote walisikei hili. Nahisi kwamba hii ndio njia peke itakayookoa maisha yako kwa sasa, this is a very serious issue..!
   
 9. O

  Original JF-Expert Member

  #9
  Apr 24, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 326
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mpigie simu Kikwete umpe taarifa hizo.
   
 10. K

  Kishalu JF-Expert Member

  #10
  Apr 24, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 850
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  Pole sana ndugu naamini hapa wajamii watakupa njia mbadala ili usiwe mkimbizi kataka nchi yako
   
 11. m

  maliyamungu JF-Expert Member

  #11
  Apr 24, 2012
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 481
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  pole sana ntaongea na manumba kesho ofisini kwake then ntakupigia.
   
 12. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #12
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Umenikumbusha kesi ya zombe wale wauza madini walivyouawa pale nyuma ya jengo la tcra sam mujoma road na kwenda kutupwa msitu wa pande!! Cha msingi Ndesamburo nenda ITV warushe habari yako soon tu utapata ulinzi wa kutosha! Kwamba title waweke unahitaji msaada wa kisheria
   
 13. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #13
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Pole sana Lucky...
  Mungu atakusaidia utakuwa salama na watakusikiliza tu...
  Natumai ujumbe umewafika
   
 14. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #14
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Tunakutumia mwandishi wetu ambaye atakusikiliza na kisha ataongea na wakuu ndani ya Jeshi la Polisi!

  Karibu JamiiForums
   
 15. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #15
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Kesi ya nyani unataka kumpa ngedere?
   
 16. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #16
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Safi sana Invisible..
   
 17. Triple A

  Triple A JF-Expert Member

  #17
  Apr 24, 2012
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 750
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Pole san ndesapesa,hii issue iko hot sana nakushauri ita waandishi wa habari wape hii habari kwa undani zaidi nadhan watakusaidia katika hili.
   
 18. Mu-sir

  Mu-sir JF-Expert Member

  #18
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 3,633
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  mkuu utakuwa umefanya kutu kizuri sana kumsaidia huyu jamaa
  much respect to you.
   
 19. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #19
  Apr 24, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Pole Sana Ndesamburo!
  Nchi hii sijui tumwamini nani tena.
  1. Baada ya Jitihada zako kuwasilisha barua kwa IGP na kwa Gavana wa BOT kushindikana uliwasilisha nakala za barua hizo ofisini kwangu.
  2. Mimi binafsi niliwasiliana na IGP Saidi Mwema na akaniahidi kulishughulikia yeye mwenyewe. Alimtuma kamanda wake kuchukua nakala ya barua yako. Nikaamini swala litashughulikiwa. 2. Nikaongea na Gavana Beno Ndulu akanihakikishia atashughulikia yeye mwenyewe. Kama hakuna hatua hadi leo basi tumekwisha. Maana sasa tutaachaje kuamini kauli ya wahusika kuwa mtandao wao unamhusisha Advocate Nyombi RPC Mbeya na IGP Saidi Mwema! Kama ni kweli tuko pabaya kuliko tunavyodhani.
   
 20. akilimtindi

  akilimtindi JF-Expert Member

  #20
  Apr 24, 2012
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 423
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nakushauri usiwaachie tu waandishi wa JF washughulikie hii habari, peleka hii habari kwa vyombo vyote vya habari. Ukilifanyia mchezo hili kama ni la kweli litakugharimu na tutakusahau, hatutaweza kufanya lolote maana ushahidi utakuwa umepotea.
   
Loading...