Polisi Kutumia vitisho vya ugaidi kuzuia maandamano ni kuzidi kudidimiza uchumi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi Kutumia vitisho vya ugaidi kuzuia maandamano ni kuzidi kudidimiza uchumi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Hofstede, Nov 23, 2011.

 1. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #1
  Nov 23, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Ni dhahiri kuwa katika dunia ya utandawazi ya sasa habari yoyote ile inatambaa kwa kasi sana. Tanzania imebarikiwa kuwa na vivutio vingi vya watalii. CCM wanapotumia polisi kuzuia maandamano kwa kisingizio cha intelijensia ya Al shabab siyo tu wanakuwa wamekomoa waandamanaji bali wanazidi kudididmiza taifa hasa kwenye sector ya utalii.

  Nchi nyingi sana zinajaribu kupunguza risk kama hizo kwa kuwahakikisha watu kuwa wanafanya kila liwezekanalo ili kuwalinda wao na mali zao dhidi ya ugaidi. Kutumia tishio la Al shabaab kupitishia agenda ya kuzuia maandamano will serve well for those who have been told to use anything they can to thwart demonstration but their actions have more negatives to our country's prosperity than the positives to afraid ruling elites.

  Potential and current foreign investors will also see this as a threat to their investments in the country and therefore transfer their capital to other country with less terror risk. But another issue is political risk, CCM using police to thwart peaceful demonstrations is an incubation for confrontation which in one way or another can be avoided.

  This also increases risks for tourism and Import of foreign investments. Letting people vent their anger is the best way of reducing risk than forbiding them and suffer internal discrimination in their own country. Police or CCM have nothing to lose when people go the streets pieceful, but they are losing big when they force people remaining with their anger.

  Kuwatumia polisi ambao wengi wao ni darasa la saba kama mbwa wa kuumia wanaokutisha hata kama hakuna potential ya kukudhuru ni kutengeneza mazingira ya kuogopesha wageni kuja Tanzania. Marekani ni Taifa ambalo lenye less political risk na lenye watu wenye uhuru wa kuongea na kufanya chochote kile ili mradi hawavunji sheria za nchi. Kuwaacha watu waandamane kutoa hisia zao Tanzania ni jambo lenye afya kwa amani yetu na ustawi wa demokrasia na uchumi wetu.

  Mwanadamu kazaliwa huru na ataendelea kuwa huru hata kama uhuru huo utauchukua kwa muda kwa kutumia mabomu ya machozi na risasi. Serikali iache woga, njia pekee inayoweza kufanya watu wasiandamane ni kuwapa watu nafasi ya maamuzi katika nchi yao na si kulazimisha hata yale yasiyolazimizika.
   
 2. Black Rose

  Black Rose JF-Expert Member

  #2
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 243
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Na siku kuna Al Shabaab wa ukweli..nani atawaamini?
   
 3. Zed

  Zed JF-Expert Member

  #3
  Nov 25, 2011
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 359
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nikiwa kama mfanyabishara katika sekta ya utalii hapa Arusha nasikitika sana kuliarifu jeshi la polisi, kuwa mayowe yao ya hatari ya Alshabaab kama kisingizio cha kupiga marufuku maandamano ya Chadema yamenisabaishia hasara kubwa, kwani kumekuwa na cancellations za bookings za watalii kutoka Marekani na Ulaya wakiogopa kutekwa na Alshabaab hapa Tanzania.

  Jamani serikali, mambo haya amabayo ni sensitive kiuchumi kuwaachia watu kama wakina kamanda Kagonja kutoelea matamko bila tathmini ya athari zake kwa uchumi ni kuvuruga uchumi!

  Naoma serikali itoe tamko wazi kwa balozi zote nchini na pia balozi zetu zilizopo nchi za nje kuwa Tanzania ni salama kwa utalii na kwamba inawahakikishia watalii na watanzania wote kuwalinda na kwamba tuendelea na shughuli zetu za kiuchumi. Vinginevyo tunaangamia kiutalii hapa Arusha. Serikali itambue kuwa inflation, devaluation of the shilling, shamble economy na sasa Al-Shabaab inatufilisi wajasiriamali wa utalii!
   
 4. WAFU FM

  WAFU FM Member

  #4
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nani anataka kwenda kwenye nchi ambayo imeshindwa kuwalinda raia wake itakua sisi wagen bana, endeleni na kupambana na hao vijana wa somalia mkamliza tutakuja kutembea tu mlima si upo na mbuga si zipo na hazihami...
   
 5. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #5
  Nov 25, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Hii ni unaweza kuiita double edged sword au boomerang
   
 6. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #6
  Nov 25, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Meanwhile nenda SA ukadhuru kwenye Table Mountain kiongozi
   
 7. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #7
  Nov 25, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,383
  Likes Received: 22,259
  Trophy Points: 280
  POlisi wanaangamiza nchi kwa kukosa maarifa
   
 8. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #8
  Nov 25, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Hii ndiyo Tanzania wanaona ni heri uchumi uanguke lakini CCM ibaki madarakani, Tatizo lilipo ni kwamba Uteuzi wa wakuu wa idara mbali mbali za Serikali upo chini ya wanasiasa, inaingia akilini kweli watu wanaoandamana kupinga malipo ya Dowans hawaruhusiwi kwasababu ya uwepo wa Al-shabab lakini siku hiyo hiyo Simba na Yanga walicheza polisi walidai Alshabab hawana tatizo nao waende tu na watazamaji waliingia kwa maelfu.

  Kwa sasa Wanaharakati walipanga kuandamana Tarehe26/11/2011 wamekatazwa kwasababu ya Alshabab wakati huo huo kuna maandamano ya kuchangisha Mil500 ya ujenzi wa shule kesho yatakayokwenda Kilomita2 na mgeni rasmi atakuwa Waziri mkuu yameruhusiwa.
   
 9. Zed

  Zed JF-Expert Member

  #9
  Nov 25, 2011
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 359
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Juhudi zote za bodi ya utalii kutangaza mpaka kwenye ligi kuuya soka ya Uingereza sasa inaonekana kuwa kuvurugwa na matamko ya polisi. Mie naona serikali imekosa utashi hapa! Hawa wanatuharibia sana, fikiria kufutwa kwa safari 5 ya makundi ya watalii wasiopungua wa5 kwa mwezi huu kwa hofu ya Alshabaab hadi leo ni hasara kubwa!
   
 10. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #10
  Nov 25, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Polisi wanafikiri kila kitu ni kupayuka tu. Hawaangalii madhara yanayoweza kutokea kutokana na utafiti wao na wanadhihirishia wananchi ya kuwa Tanzania hakuna polisi wala maafsa usalama. Na ndio maana wameshindwa hata kuwakamata wauza madawa ya kulevyia na biashara hii imebaki mikononi mwao ni hatari kwa Taifa la Tanzania. Kenya wamewakamata na ndio maana wametangaza hata kwenye vyombo vya kimataifa, sasa mbona hatujaona Tanzania wakiwa hewani kama Kenya kuonyesha ya kuwa wameshakamata hawa Al-shabaab?
  Polisi fanyeni kazi yenu kama polisi acheni kupiga mayowe, shirikianeni na wananchi na mtafanikiwa kuliko mnavyowanyima wananchi haki yao ya kutafuta maendeleo na kuogopa nchi yao. Ukiangalia kwa upande mwingine polisi hao hao ndio wahusika wakuu kwenye mitandao mbali mabali ya matukio mabaya hapo Tanzania.
   
Loading...