Polisi kushirikiana na wahalifu?

kukumdogo

JF-Expert Member
Feb 1, 2011
2,866
2,746
Habari zenu wandugu
nimeamua kuwaletea kwenu hii kitu maana inanisumbua kichwa sana. Kunakesi nyingi sana za wizi na ujambazi sasaivi wakati polisi wanaotakiwa kutulinda wapo na wanakula kodi zetu na ulinzi wenyewe hatuuoni. Mtu kama kova kazi yake ni kuita vyombo vya habari na kuongea pumba tu huku kazi anayotakiwa kufanya haifanyi kama inavyotakiwa.

Tuje kwenye wizi wa vyombo vya magari. Kilakitu ukiibiwa cha kwenye gari unakikuta gerezani, polisi wanalijua hili na wahusika wanajulikana ila kwanini hawakamatwi? Je polisi wanashirikiana nao ili waongeze posho zao? Naandika nikiwa na machungu sababu saivi polisi kazi yao imekuwa kama kupiga wanafunzi na wananchi wanaodai haki zao.
Mapendekezo yangu kwa serikali ni kwamba jeshi la polisi lifutwe na nafasi ya waziri mambo ya ndani ifutwe sababu hana kazi ya kufanya zaid ya kutuongezea matatizo.
 
Pendekezo zuri, unategemea nani atalifuta Jeshi la Polisi? JK? Itabidi umeze dawa za maumivu na za kukusaidia kusahau hoja yako.

Hii ni nchi inayoongozwa na wasanii, wangependa mambo yaendelee kwenda kimjin mjin tu!
 
Back
Top Bottom