Polisi kupiga na kutesa watuhumiwa vituoni inaruhusiwa hapa nchini? Wasomi wa sheria mtusaidie hili

Unsub

Senior Member
May 4, 2018
113
250
Salaam. Kama heading inavyosema. Naomba kufahamu maana kesi nyingi watuhumiwa wanasema waliteswa na askari polisi mf watuhumiwa wa kesi ya Msuya.
Karibuni.
 
Mbao za Mawe

JF-Expert Member
May 11, 2015
22,921
2,000
Ni moja ya njia ya kukusanya taarifa hasa kwa watuhumiwa wa kesi za jinai, mfano wamemtia hatiani mtuhumiwa wa mauaji ya Kibiti hawawezi kutumia lugha ya maneno tu kutafuta kile wanachotaka ila inatakiwa ufanyike kwa weledi sana.
 
Unsub

Senior Member
May 4, 2018
113
250
Ni moja ya njia ya kukusanya taarifa hasa kwa watuhumiwa wa kesi za jinai, mfano wamemtia hatiani mtuhumiwa wa mauaji ya Kibiti hawawezi kutumia lugha ya maneno tu kutafuta kile wanachotaka ila inatakiwa ufanyike kwa weledi sana.
Je inaruhusiwa kisheria? Na hizo taarifa zinaweza kutumika mahakamani? Na hiyo ni moja ya kazi ya askari polisi wetu? Na je ni kwetu tu au kila nchi dunia nzima yanafanyika hayo?
 
Unsub

Senior Member
May 4, 2018
113
250
Ni moja ya njia ya kukusanya taarifa hasa kwa watuhumiwa wa kesi za jinai, mfano wamemtia hatiani mtuhumiwa wa mauaji ya Kibiti hawawezi kutumia lugha ya maneno tu kutafuta kile wanachotaka ila inatakiwa ufanyike kwa weledi sana.
Mtuhumiwa (suspect) ni mtu ambaye hajahukumiwa bado. Na haimaanishi kila mtuhumiwa atakuja kuhukumiwa kuna wengine wanaachiwa na kuonekana hawajatenda kosa. Sasa wanapoteswa na askari polisi wakiwa vituoni halafu mahakama ikaja kuwaachia huru, watesi wao hawatakiwi kuchukuliwa sheria?
Mlolongo mzima wa kukamatwa mtuhumiwa mpaka kufikishwa mahakamani upoje kisheria?
 
Baija Bolobi

JF-Expert Member
Feb 25, 2009
1,096
2,000
Kutesa watuhumiwa ni kiwango cha juu kinachoeleza kutoendelea kwa taifa lolote (Barbarism). Ikithibitika polisi wametumia mateso kupata ushahidi, katika mifumo ya utoaji haki iliyoendelea, ni kigezo cha mahakama kufukuza kesi papo hapo.
 
Unsub

Senior Member
May 4, 2018
113
250
Kutesa watuhumiwa ni kiwango cha juu kinachoeleza kutoendelea kwa taifa lolote (Barbarism). Ikithibitika polisi wametumia mateso kupata ushahidi, katika mifumo ya utoaji haki iliyoendelea, ni kigezo cha mahakama kufukuza kesi papo hapo.
Je hapa nchini kuna kesi ishawahi kufutwa na mahakama kwa sababu hiyo?
 
Baija Bolobi

JF-Expert Member
Feb 25, 2009
1,096
2,000
Kwa=kwani
Nitajie mfano wa nchi zilizoendelea.

Naweza nisizijue lakini nazijua zisizoendelea na ya kwetu imo. Wakusanya ushahidi wamefundishwa kukusanya ushahidi bila kutesa watu. Ziko mbinu nyingi zisizo physical torture. Kuna sleep deprivation, lie detector, pyschological manipulation, DNA n.k
Kutesa ni unyama wa atesaye.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom