Polisi kuendeleza mabomu na risasi na mauaji ya raia kuilinda serikali iliyo madaraka

DENYO

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
698
57
Wanajf naomba mnisaidie labda mimi sikuelewa vizuri nilipomsikia camissiona chagoja akiongea kwa niaba ya polisi alipoongea na waandishi wa habari tarehe 13 jan 2011. Alisema

1. Polisi inalinda serikali iliyopo madarakani na kwamba itadhibiti maandamano yoyote atakayejaribu kuikosoa serikali hiyo- hivi alimanisha polisi itaendelea kuua, kuumiza raia kwa mabomu na risasi za moto na maji washa?

2. Aliposema wanaodai haki wasubiri 2015 - ina maana alimanisha mafisadi, wanyonyaji wote na wachakachuaji waendelee kupeta mpaka 2015 au na yeye ni mmoja wapo? Au ameahidiwa kitu? Au ana maslahi binafsi.

3. Aliposema sema polisi walivunja maandamano kuzuia vurugu -hivi kulikuwa na vurugu polisi ilipoenda kuanza kufyatua risasi na maji washa?

4. Aliposema polisi wanafanya kazi kwa kufuata sheria za nchi, hivi anajua ni haki ya kikatiba kutoa mawazo katika mkusanyiko? Hivi anajua kuwa kuua ni kosa la jinai, hivi anajua muuaji laziima afikishwe mahakamani ili kuonesha kuwa kuua huko kulikuwa si kwa makusudi?

5. Aliposema kuna tume inafanya uchunguzi ya kipolisi -hivi anajua nyani hawezi kumchunguza ngedere? Je alisema askari waliofyatua risasi wamefikishwa mahakamni ili mahakama iwasafishe??? Siyo polisi kuwasafisha? Iweje polisi ijisafishe yenyewe? Kama walivyofikishwa mahakamani akina slaa-hao walioua wamefikishwa mahakamani? Au ndio kuthibitisha kweli ccm iliwatuma kuua ndio maana hawatafikishwa mahakamni manake wao ndio walioshika mpini.?

Naomba mnisaidie walioua raia wa arusha wako wapi sasa hivi? Na kwanini wasifikishwe mahakamani kama akina zombe kwani kuna tofauti gani??
 
Back
Top Bottom