Polisi Kilimanjaro walioshambulia raia waachishwa kazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi Kilimanjaro walioshambulia raia waachishwa kazi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Saint Ivuga, Jul 29, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,290
  Likes Received: 19,445
  Trophy Points: 280
  Polisi Kilimanjaro walioshambulia raia waachishwa kazi 29/07/2011

  0 Comments


  Jeshi la Polisi limewafukuza kazi askari polisi wawili wa kituo cha Okaoni Kibosho Wilaya ya Moshi Vijijini kutokana na kumshambulia mwananchi mmoja kwa marungu na nondo hadi kumvunja miguu.

  Polisi waliofukuzwa kazi ni pamoja na G 816 Pc Stanslaus na G 1191 Pc Maiga, ambao pia wanadaiwa kumshambulia Theopili Mallya kwa nondo na marungu na kumvunja miguu hali iliyomsababishia kupata maumivu makali mwilini mwake.

  Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Absalom Mwakyoma, alisema kuwa tukio hilo lilitokea Juni 5, mwaka huu majira ya saa 3:30 za usiku katika kituo kidogo cha polisi Okaoni.

  Alisema askari hao walifukuzwa kazi Julai 8, mwaka huu baada ya kupatikana na hatia katika mahakama ya kijeshi kwamba kitendo walichokifanya ni kinyume na mwenendo mwema wa jeshi, "Baada ya mashitaka ya kijeshi kuendeshwa na kutiwa hatiani, walifukuzwa kazi na hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani kujibu shitaka la kumvunja miguu Mallya," alisema Mwakyoma.

  - via NIPASHE
   
 2. F

  Froida JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  MMH isije ikawa wana respond kwenye hotuba ya kambi ya upinzani nchi hii kwa propanganda haina mwenyewe
   
Loading...