Polisi Kenya Washindwa Kumtia Mbaroni Bilionea Fisadi Mkubwa Kenya

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,372
6,078
image.jpeg
Jimi Wanjigi ni Bilionea ambaye amehusika na ufisadi mkubwa Kenya Kama Anglo Leasing ameshindwa kutiwa mbaroni na Polisi jijini Nairobi baada ya kujifungia kwenye chumba lililojengwa kama kasha la kutunzia fedha ( Strong Room) kwenye jumba lake Muthaiga jijini Nairobi. Jimi Wanjigi ambaye alikuwa mwanachama maarufu wa Jubilee na alishiriki kikamilifu kuwaunganisha Ruto na Uhuru Kenyatta kwenye uchaguzi wa mwaka 2013 kabla ya kuhamia kumuunga mkono kinara wa NASA Raila Odinga kwenye uchaguzi wa mwaka huu. Polisi walivamia jumba la Mfanyabiashara huyo ili kumtia mbaroni kwa kumhusisha kwa kukamatwa kwa silaha katika jumba la huko Malindi Kenya. Jimi Wanjigi ambaye serikali ya Kenya inaamini kuwa ni mfadhili mkubwa wa chama cha NASA kifedha, Mfanyabiashara huyu maarufu nchini Kenya ambaye hutembea na zaidi ya walinzi zaidi ya kumi alikwaruzana na serikali ya Kenya baada ya kampuni aliyotaka ijenge reli ya Mombassa mpaka Nairobi kunyimwa tenda ya ujenzi huo.
Wakili maarufu wa NASA James Orengo aliwasilisha hati ya dharura mahakamani jijini Nairobi kuomba mahakama isimamishe Polisi kuendelea kumsaka huyo bilionea, mahakama walikubali ombi hilo na imeamuru Polisi wa Kenya waache kumkamata, licha ya Polisi kupewa amri hiyo lakini bado walikuwa wamezingira jumba la bilionea huyo wakijaribu kubomoa chumba hicho bila mafanikio.
Hiyo picha ni miongoni mwa magari ya kifahali ya bilionea huyo hiyo gari aliingiza nchini Kenya hivi karibuni inathamani ya dola laki 4 [ATTgACH=full]611644[/ATTACH]
 

Attachments

  • image.jpeg
    image.jpeg
    25.8 KB · Views: 58
Alipokuwa anamuunga mkono Uhuru Kenyatta hakuwa fisadi saivi kumuunga mkono Raila tayari kawa fisadi..
Kwa ufahamisho lazima uelewe sehemu kubwa ya vyama vya siasa ni madaraka Huyu Bilionea serikali ya Marekani imempiga marufuku kwenda nchini humo kwasababu ya Ufisadi. Edward Lowassa alipokuwa CCM chama cha Chadema kilikuwa kikimwita Fisadi lakini alipohamia Chadema hapo hapo alipewa nafasi yakuwa mgombea urais na kauli mbiu mabadiliko. Raila Odinga anadai anataka kuwakomboa wakenya kutoka kwenye ufisadi at the same time fedha za mafisadi zinamfanyia kampeni, je Raila yupo serious kupambana na ufisadi?
 
Haha kwahiyo huko kwenye chumba kama cha strong room ana kila kitu kwamba wala hatahitaji kutoka nje kupata huduma zingine.?
Police wenyewe hapo lazima wasande maana hawakutegemea hiko kitu hahaha
 
Back
Top Bottom