Polisi kenya ahukumiwa kifo na mahakama

digodigo

JF-Expert Member
Dec 2, 2010
255
178
Polisi mmoja nchini kenya mwenye cheo cha OCS jana alihukumiwa kunyongwa hadi afe baada ya Mahakama kumpata na kosa la kuua kwa makusudi mtuhumiwa mmoja aitwae Martin Koome mnamo mwaka 2013 akiwa ndani ya sero.
Polisi huyo alimvunja mbavu mtuhumiwa huyo baada ya mateso makali na baadae alimtoboa kichwa kwa kutumia kitu chenye ncha na kama haitoshi alimzamisha kichwa kwenye pipa lenye maji na baada ya hapo akawafungulia watuhumiwa wengine walioshuhudia ili wasimshitaki na pia kumbambikia kosa hilo mmojawapo wa watuhumiwa!.
Hii ni kwa mujibu wa vyombo vya habari Kenya na BBC hapo jana.
 
Huku kwetu Mkuu wa kaya anawazawadia vyeo maaskari wanaoua na kukamata viongozi wa Upinzani huku maamuzi ya mahakamani kwa kila kesi anayatoa yeye. Ni swala la Muda tu.
 

Polisi wa Kenya waje kuomba kazi Tanzania. Huku askari akiua raia hapaswi kushitakiwa, kwa mujibu wa raisi wetu ambaye neno lake ni sheria
 
Back
Top Bottom