Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwaua majambazi watatu

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,861
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwaua majambazi watatu na kukamata silaha moja bastola aina ya REVOLVER.

Katika taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa inasema kuwa Mnamo tarehe 11/05/2021 majira ya saa tatu usiku huko Mbagala jirani na ukumbi wa Dar Live majambazi wapatao watatu wakiwa kwenye Pikipiki namba MC 640 CGT aina ya TVS wakijiandaa kufanya ujambazi kwenye maduka na vibanda vya miamala ya fedha, lakini kabla hawajatimiza azma yao ya kufanya uhalifu.

Taarifa hiyo imesema Kikosi kazi cha kupambana na ujambazi cha Kanda Maalum Dar es Salaam kilipata taarifa na kujipanga vizuri, ambapo ilipofika majira saa nne usiku majambazi hao wakiwa kwenye pikipiki walipewa amri ya kusimama lakini walikaidi amri hiyo na kuanza kuwarushia askari risasi, ndipo askari wakajibu mashambulizi na kufanikiwa kuwapiga risasi sehemu mbalimbali za miili yao na kufariki dunia papo hapo.

"Kikosi hicho kilifanya ukaguzi kwenye eneo la tukio na kufanikiwa kupata silaha moja Bastola aina REVELVOR ikiwa na risasi tatu ndani ya magazine na walipopekuliwa kwenye miili yao walikutwa na risasi tano za bunduki ambayo haifahamiki ni ya aina gani." Imeeleza

JESHI LA POLISI KANDA MAALUM DSM KUIMARISHA USALAMA SIKUKUU YA EID EL-FITRI
Jeshi la Polisi Kanda Maalum kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama limejipanga kikamilifu kuimarisha usalama katika kipindi cha sikukuu ya Eid el-fitri inayotarajiwa kuadhimishwa tarehe 13/05/2021 au 14/05/2021 pindi itakapothibitishwa na Mh. Mufti wa Tanzania.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawaasa wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kusherehekea sikukuu ya Eid El-fitri kwa amani na utulivu na kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa sheria.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum limejipanga kuimarisha doria maeneo yote muhimu zikiwemo nyumba za ibada, fukwe za bahari, kumbi za starehe na maeneo mengine yote yatakayokuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu ili kuhakikisha Wananchi wote wanasherehekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu.

Pia wazazi wahakikishe watoto wao hawatembei peke yao bila ya kuwa na uangalizi wa karibu na kutowaruhusu kuogelea pekenyao, kitendo ambacho kinaweza kuzuia watoto hao kuzama kwenye maji.

Wamiliki wa kumbi za starehe wanatakiwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji wa kumbi hizo.

Aidha, Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limepiga marufuku Disko toto katika kumbi zote za starehe za hapa Jijini Dar es Salaam.

Vilevile Madereva wa vyombo vya moto wanatakiwa kuendelea kufuata sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kutoendesha magari au pikipiki wakiwa wametumia vilevi/pombe.

Hata hivyo Jeshi la polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawaomba Wananchi kuendelee kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu kwa namba zifuatazo 0653616277, 0755980633 na 0769360416.
 
Pongezi kwa jeshi, yule askari machachari wa kupambana na majambazi kisharudi?
Waongeze masnichi mtaani.

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Mmmhhh mara mmeanza kuua?
Msije mkawa mnatengeneza stori
Kwa nini kila siku huwa mnaua tu hamuwezi kuwakamata na kuwapeleka mahakamani?
Nyie haya
Kutulinda mpaka mshitukizwe mpange tukio weledi mmh mmh upo kweri au show?
Hili jeshi kwa kweri
 
Watanzania walio wengi hawapendi Ujambazi.... Unaona wale vijana waliotoka jela majuzi nao wameuwa na wananchi wenye hasira Kali.

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Yaani majambazi watatu wanapanga kuiba hafla polisi hao bang bang bang chaliii kifo cha mende. Bila ya shaka hawa majambazi walikuwa Facebook live ndio maana siri yao ikavuja. Wakati ukipiga simu polisi mara nyingi kama kuna wahalifu watakwambia hawana hela ya mafuta
 
Vyema.
Ila isijekuwa ni Mambosasa anataka kujihalalishia nafasi yake kwa kuwachapa risasi raia.
Ngoja usiku wa leo nikutumie majambazi watatu wenye bastola moja waje wakushugulikie mbele ya mkeo ndipo utaacha kuwa na huruma kwa majambazi.
 
Katika taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa inasema kuwa Mnamo tarehe 11/05/2021 majira ya saa tatu usiku huko Mbagala jirani na ukumbi wa Dar Live majambazi wapatao watatu wakiwa kwenye Pikipiki namba MC 640 CGT aina ya TVS wakijiandaa kufanya ujambazi kwenye maduka na vibanda vya miamala ya fedha, lakini kabla hawajatimiza azma yao ya kufanya uhalifu.

Taarifa hiyo imesema Kikosi kazi cha kupambana na ujambazi cha Kanda Maalum Dar es Salaam kilipata taarifa na kujipanga vizuri, ambapo ilipofika majira saa nne usiku majambazi hao wakiwa kwenye pikipiki walipewa amri ya kusimama lakini walikaidi amri hiyo na kuanza kuwarushia askari risasi, ndipo askari wakajibu mashambulizi na kufanikiwa kuwapiga risasi sehemu mbalimbali za miili yao na kufariki dunia papo hapo.

"Kikosi hicho kilifanya ukaguzi kwenye eneo la tukio na kufanikiwa kupata silaha moja Bastola aina REVELVOR ikiwa na risasi tatu ndani ya magazine na walipopekuliwa kwenye miili yao walikutwa na risasi tano za bunduki ambayo haifahamiki ni ya aina gani." Imeeleza
Hii imewezeshwa na nani? Ni mama au RC?
 
Yaani majambazi watatu wanapanga kuiba hafla polisi hao bang bang bang chaliii kifo cha mende. Bila ya shaka hawa majambazi walikuwa Facebook live ndio maana siri yao ikavuja. Wakati ukipiga simu polisi mara nyingi kama kuna wahalifu watakwambia hawana hela ya mafuta
Unajitia dole na kujilamba.!!
Ikiwa sudden event,polisi sometimes huwa hawana mafuta au gari mbovu maana hao jamaa maisha yao ni magumu na hata vitendea kazi kwao ni changamoto hasa mafuta kwao imekuwa mtihani usiofanyika sijui ile bajeti inayopitishwa pale bungeni huwa inaishia wapi!jamaa wamekuwa wakiendesha kazi zao kwa kuomba sapoti kwetu sisi 'wadau wa polisi'.

Ila tukio kama hili 'liloripotiwa' ni planned event hivyo iliwachua rahisi polisi kujiandaa kivyote(gari+mfuta &nguvu kazi).
 
Huku kwetu jamani tunatabika na vibaka wanakata madilisha na kuiba TV,wajina wale nadhani atatuma madawa,jamaa kaibiwa TV huku mdogowake kalala hapo sebuleni alikuwa anajisomea.
 
Mmmhhh mara mmeanza kuua?
Msije mkawa mnatengeneza stori
Kwa nini kila siku huwa mnaua tu hamuwezi kuwakamata na kuwapeleka mahakamani?
Nyie haya
Kutulinda mpaka mshitukizwe mpange tukio weledi mmh mmh upo kweri au show?
Hili jeshi kwa kweri
Unamkamata mtu anakutupia risasi?
 
MAJAMBAZI NA POLISI WANAFAHAMIANA VIZURI SANA. NI SUALA LA KUTOA AMRI TU KUWA MAJAMBAZI WATOWEKE.

HEKO MAMA SAMIA.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom