mtu watu
JF-Expert Member
- Dec 10, 2017
- 2,123
- 1,616
Kila kukicha nazidi/tunazidi kupokea ujumbe mfupi wa kutuma pesa kwa mtu fulani, ili jambo limelalamikiwa sana na wananchi na watumiaji wa mitandao ya simu husika, mpaka ikapelekea polisi kuingilia kati na kudai imewakamata wezi hao wanaotumia namba husika katika kutapeli watu.
Lakini bado hao wezi hawajakoma wamezuka wengi sana, kila kukicha nitapokea ujumbe mfupi (sms)ukinitaka kutuma pesa kwa mtu husika, je polisi na kampuni za simu hawajafanikiwa kuwapata waharifu hao wote?
Imeenda mbali mpaka polisi wenyewe kuanza kunitumia/kututumia ujumbe kutusihi kuwa tusitume pesa kwa watu bila taarifa kamili kumuhusu huyo tunayetaka kumtumia hizo pesa.
Sasa swali langu ninauliza je mpaka sasa, polisi, kampuni za mitandao ya simu na Tcra wameshindwa kudhibiti uharifu huu mpaka sasa?