Polisi juzi Hamza aliwaua na kuwapora silaha, leo mahabusu wamewapiga na kutoroka, bado tu panapovuja hampaoni?

Hii inaweza kuchukuliwa poa Kama tulivyozoea watanzania kuchukulia Mambo simple simple.

Hamza alivyowaua askari wetu na kuwapora siraha wapo waliosema ni kwasababu aliwashitukiza vinginevyo asingeweza. Mimi nikajiuliza, askari si anatakiwa awe tayari muda wote? Iweje wajitetee kwa kusema walishitukizwa?

Siku zote adui anakusubiri uzubae achukue point, hakupi taarifa ujiandae hivyo askari wetu walifanya uzembe hilo halipingiki katika medani za kijeshi

Leo vyombo mbalimbali vya habari vimeripoti mahabusu kule Mbagala wamempiga askari aliyekuwa lindo kisha wakavunja lango wakatoroka

Je, na hapa tusemeje? Wameshitukizwa tena!?

Kwa tathimini yangu ya "ki-lay man" nimekuja kufanya conclusion jumuishi ifuatayo kwa baadhi ya watu wanaofanya kazi sehemu mbalimbali serikalini na taasisi za umma:-

1. Wafanyakazi wengi katika taasisi hasa za serikali ni vijana ambao bado hawajawa 'matured" ki ueledi katika nafasi wanazozitumikia. Bado wanaendekeza "ujana unaendana na ubishoo" pasipo kuonyesha kuwa committed kwa wanachofanya

Hapa ni kote. Angalia baadhi ya madkatari na manesi kwenye hospital za umma, chunguza askari wetu hata wakiwa kwenye magari yao ya PT au lindo, tembelea taasisi za umma uona utakavyohudumiwa

2. Vijana wengi wanafanya kazi wasizopenda. Wanafanya ilimradi tu wapate mshahara ila hawajali kuhusu performance na ubora katika wanachofanya. Hii ni kwasababu ya ukosefu wa ajira hivyo fursa yoyote itakayokuja mbele yake ataomba bila kujali ataiweza, au anaipenda

3. Watanzania wengi ni wavivu hivyo tunapokuwa kwenye mazingira ya kazi zetu tunajali kumaliza twende tukapumzike. Yaani tunawaza kumaliza kazi wakati ndo tunaianza. Hii inamfanya mtu aelekeza akili yake kwenye muda wa kuondoka kuliko kile anachofanya

Nini kifanyike?

Tuwekeze zaidi kwa watoto wetu! Tuwafundishe kupenda kazi, kujali ubora wa kazi zao, kujituma na kujibidisha kwa wanachofanya. Ifike mahali mtoto asipofanya kitu katika ubora uliotarajia aumie na ionekane ameumizwa na kushindwa kufanya vizuri

Hali hii italeta uwajibikaji huko mbeleni.

Askari wameuawa na kunyang'anywa siraha kitu Cha hatari kabisa (hata Kama baadae walizipata ) hakuna aliyewajibika. Kwa maana hiyo tumeona sawa tu na tunasonga mbele

Leo mahabusu wamempiga askari, wamevunja lango wametoroka. Hakuna anayewajibika. Tunaona simple tu hadi viongozi wanasema "wametoroka wenye makosa madogo madogo".

Umeme unaweza kukatika mtaani tukakaa giza hata wiki nzima na hakuna anayewajibika wala kujali

Maji yanaweza kukatika mtaani zaidi ya wiki na watu wasijali na wakachukulia poa tu. Yaani wafanyakazi wa idara husika hawajali wateja wao kukosa huduma na wananchi nao pia hawajali kukosa huduma yao ya msingi

Kwa utamaduni huu tutaifikisha Tanzania kwenye maendeleo ya kweli!?
Pole, na JPM alivyoingia akaanza kutunyoosha tukamchukia, aliyepo ni mtalii, kusema wanawake walivyokomaa na kuamuliwa mambo na viongozi wa zamani, nakuuliza, je tunaye JPM mwingine njiani au?!
 
Mkuu,hongera. Hii ni kweli,maeneo mengi ni vuruvuru. Kubwa ambalo umelisahau ni ajira za upendeleo,undugu,ukabila nk. Mtu hafanyi kazi ipasavyo kwa vile hata akikosea ana wa kumtetea. Nafasi za ajira zikitoka,peleleza wanaopatà zile nafasi na mahusiano yao na vigogo waliopo sekta hiyo!!
 
Umejuaje kwamba huyo Askari alikua kijana..au ndo unaleta youth-phobia.
 
Halafu Sirro anataka et mabank waweke ulinzi wa polisi kwamba kutoweka ulinzi wa polisi na kweka hawa security ndio sababu ya kutokea uhalifu kwenye mabank kwa sababu hao walinzi hawana weledi kama jeshi la polisi. Yani Sirro anaropoka kichizi, weledi wenyewe ndio huo wa kunyang'anywa silaha na Hamza au huo wa kutorokwa na mahabusu.
 
usijikite kulaumu polisi,chamsingi fata ushauri wa Sirro usizae watoto wa hovyo hovyo kama hao mahabusu wa mbagala.
Mi naona tusizae watoto hovyo hovyo Kama hao polisi wanaopigwa na mahabusu watakuja kuuza nchi. Mahabusu inaonekana wako smart wanafaa kuzaliwa wengi waikomboe nchi
 
Back
Top Bottom