Polisi, Jamii na Kilichotokea Arusha

Oct 22, 2010
78
0
Mara nyingi wananchi wa Tanzania wamekuwa na hofu kila wanapomuona polisi. Tumekuwa tukishawishiwa kwamba polisi ni rafiki wa raia na kwamba hatuna haja ya kuwaogopa bali kushirikiana nao katika vita dhidi ya uhalifu na uvunjifu wa amani. Tukio la hivi karibuni huko Arusha limesikitisha wengi na wengi tumebaki na maswali, mojawapo likiwa 'Hivi polisi wa Tanzania ni rafiki wa raia'? Swali hili si tu kwa tukio hilo moja la, yapo matukio mengi yanayotutia wasi wasi wananchi, mfano, ujambazi, kutetea baadhi ya wahalifu, kuwabambikizia watu makosa wasiyotenda rushwa na mengi mengi. Naomba kuuliza, hivi polisi wetu ni rafiki zetu? Wapo kwa ajili ya raia au kuwalinda wakubwa wachache?
 
Back
Top Bottom