ntagunga
JF-Expert Member
- Aug 13, 2011
- 654
- 256
Tangu 2006, Jeshi la Polisi Tanzania lilizindua mfumo mpya wa kiutendaji ambapo ilizindua POLISI JAMII NA ULINZI SHIRIKISHI.
Maana halisi ya dhana hii ni kwamba kuna uwezekano wa kuwa na jamii ambayo haina uhalifu. .Kufikia hili ndipo jamii nzima inatakiwa iwe mdau wa kuhahakisha kuwa uhalifu unapingwa/jamii nzima kushiriki katika ulinzi.
Kufanikisha mkakati huu, Jeshi la polisi linamtaka kila mwana jamii ashiriki katika ulinzi kama sheria inayounda serikali za mitaa inavyotaka. Kuna namna nyingi za kushiriki katika hili, nitazitaja mbili tu:-
1. Ni kuzuia vyanzo vya uhalifu katika jamii.
Katika kufanikisha hili, Jeshi la polisi linahimiza kila mwana jamii kuwajibika na kutoa huduma anayotakiwa kuitoa kwa uaminifu. kwa kufanya hivyo huduma bora kwa jamii zitapatikana na hivyo inakuwa ni chanzo cha kuwa na jamii/wanajamii wanaojitosheleza na hivyo kuziba mianya ya watu katika kuwa wahalifu.
Mjia hii inaaminika kuwa inaweza kuzuia uhalifu kwa kiwango kikubwa kwa kuwa, inaaminika kuwa wahalifu wengi, hawafanyi uhalifu kwa utashi wao binafsi, bali hulazimishwa na mifumo dhalimu kwa kuwa inakuwa haitoi huduma bora, inatelekeza watu wake na hivyo huamua kujitafutia maisha mazuri na hivyo kupelekea watu kuwa wahalifu.
2. Jeshi linaitaka jamii kuanzisha vikundi vya ulinzi katika mitaa, kuwa na daftari maalulu la ubalozi kufahamu nani kaingia nani katoka, kutoa taarifa za kuwepo kwa mipango ya kuvuruga amani na utulivu, na kuwa na maamuzi yenye baraka toka kwa wanajamii/uongozi wa jamii husika.
Katika hili, uhalifu mwingi hutokea kwa kuwa baadhi ya viongozi wanmejifanya miungu watu na kudiriki kuamua maamuzi yanayoathiri watu wengi peke yao. Kwa kuwa maamuzi hayo si sehemu ya jamii, wanajamii watayakataa na hivyo kupelekea uvunjifu wa amani. Hivyo jeshi linawataka viongozi kushirikisha jamii/viongozi wenzao.
Je dhana hii ikisimamiwa inatusaidia au ndo itazidisha taabu katika jamii ya ktanzania?
maoni yako nayahitaji ewe mdau wa jamii forum