Polisi Jamii ingetufikisha pabaya

Wakuacha

JF-Expert Member
May 19, 2015
2,046
1,337
Hakika tumempata Rais naanza kuamini hili ni chaguo la Mungu..

Suala la kuitumbua Polisi Jamii kiukweli nampongeza sana Mh Magufuli kwa kuliona hili. Kiukweli ukitizama tu utaona namna gani hii Polisi Jamii ilivyopeleka kushusha hadhi ya jeshi la polisi kwa nchi kama Tanzania.

Watu walishindwa kuelewa dhana ya Polisi Jamii na hatimaye ikapelekea raia kumzoea askari kupitia kiasi. Kwa mtindo huu tusingefika.

Hata polisi kunyang'anywa silaha vituo vya polisi kuchomwa moto hii yote ni zao la Polisi Jamii. Ukiangalia haya mambo ya vituo vya polisi kuchomwa moto miaka ya 1995 hadi 2005 hayakuwepo, lakini cha ajabu katika kipindi cha huyu mdudu Polisi Jamii kuingia, 2006 tumeshuhudia vituo vingi vikichomwa moto kwa sababu tu polisi kushindwa kuchukua maamuzi Magumu kama kuwalaza watu chini pale.

Watu walikuwa wanaona mbona kituo Fulani kilichomwa lakini hakuna hata raia mmoja aliyevunjwa kiuno au aliyelazwa chini.

Lazima ifike mahala RAIA akimuona polisi amuogope sio kubaki kumchekea chekea.

Polisi ongezeni ukauzu ikibidi muwe wakali kweli kweli ili ile heshima ya polisi irudi kama enzi za Mkapa. Ilikuwa ukimuona polisi unatoka mbio kweli kweli.

Nalipenda kweli jeshi la polisi na pia nawapenda kweli polisi..
 
Nasikitika kwa kuwa watu wengi hawana experience yoyote ya maisha zaidi ya hapa hapa Tanzania. Dhana ya polisi jamii siyo mpya na wala siyo ya hapa kwetu tu, iko nchi nyingi mno duniani na hufahamika sehemu zingine kama "neighborhood watch".

Kama yalivyo mambo mengi hapa nchini hili la polisi jamii ni concept nzuri iliyoharibiwa. Jeshi la polisi haliko kitaalamu na ni la hovyo mno, wazo la polisi jamii lilipoanzishwa halikuchukuliwa kitaalamu matokeo yake uozo ule ule ulioko polisi ukahamia kwenye polisi jamii.

Ni sawa na mfano wa kisu kwamba unaweza ukakitumia kumenyea chungwa lakini kisu hicho hicho mwingine akakitumia kuua mtu.

Polisi jamii ni nzuri ila imetekelezwa vibaya sababu haikusimamiwa kwa usahihi.
Idadi ya askari polisi ikilinganishwa na idadi ya raia umuhimu wa polisi jamii unaonekana bayana.
 
nchi gani duniani polisi anaogopwa? Kwahiyo na wewe umefurahi kusikia polisi wakihamasishwa kuwalaza chini raia? Au kupewa pesa ya kung'arishia viatu na sio rushwa? Wewe ni polisi
 
Wakati nchi zilizo na record ndogo ya uhalifu raia wake wakiwaona polisi wanajihisi kuwa wako salama na wanakuwa na amani!Bado elimu yako haijakukomboa,kiufupi hujaelimika au haujakomaa!
Kwa nchi kama Tanzania yenye RAIA wagumu kuelewa na wavivu Wa kufikiri polisi jamii bado sana...najua upo pamoja na Mimi sema povu tu linakutoka
 
Nikikujibu nahitaji kuwa na million saba
ngoja nami nifuate mkumbo kwako kwa maana tamko la mkuu ni amri na kwa bahati mbaya utekelezaji wake utarudisha nyuma uhusiano uliopo baina ya raia na majeshi yetu.
hivi mkuu akikosea awamu hii unaenda kuongelea wapi chooni?!
 
Ukweli upi mkuu ?! Mafanikio ya police yanategemea sana raia tukiwaogopa tutawaficha siri na Mungu asihusishwe ktk mawazo ya kibinaadam tena ambayo mara nyingi si fair
Watu waendelee kutoa taarifa. .lakini ule ujinga ujinga Wa mazoea kupitiliza nouu
 
kwani polisi sio binadamu, kwanini umuogope binadamu mwenzako???
Hapo Mkuu kachemka vibaya mno. Wanaofikiria alichokifanya ni sahihi hawajui dhana nzima ya polisi jamii. Kwanza kwa nji kama zetu hizi kuondosha polisi jamii nikuwafanya polisi wawe na kazi ngumu sana na hata hivyo washindwe kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Kwanza polisi niwachache hawezi kutosheleza mahitaji ya ulinzi na usalama wa wananchi. Mitaani vipaka wataongezeka mara dufu. Polisi jamii walikuwa wanasaidia sana kwenye suala na ulinzi shirikishi.
Kuweka gap kati ya polisi na raia pia hilo ni pungufu kubwa mno. Ambalo litafanya polisi washindwe kutimiza majukumu yao.

Polisi kutumia raia ni jambo la kawaida dunia nzima. Ndio maana kila taasisi ya polisi dunia wana informers. Hawa ni raia wanaowajua waharifu na ndio huwasaidia polisi kupata taarifa kama kuna mipango ya kutekeleza uharifu unaopangwa na magenge ya kiharifu. Hawa watu huwasaidia polisi kujua wahalifu walipo hivyo polisi kukabiliana kuzima jario la uharifu.

Ndo maana tumekuwa tukisia kwenye vyombo vya habari wasemaji wa polisi wanapofanikiwa kuzuia au kuwakamata waharifu wakisema "Baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasiri wetu au raia wema". Kuwaambia polisi wasishirikiane na raia ni kuwafanya polisi washindwe kukabiliana au kuzuia matukio ya kiharifu kwani yawezekana wakashindwa kupata taarifa kama hizo kutoka kwa raia.

Mh. Anataka kuturudisha miaka ya giza. Ambapo watu walikuwa wakiona waharifu wanafanya uharifu au wanapanga mipango ya uharifu wanaogopa kutoa taarifa kwa kuhofia kuwekwa ndani na jeshi la polisi. Hapa Mkuu kachemka vibaya mno kama polisi watatekeleza haya maagizo. Tatizo la tatu ni kuwajengea uhasama polisi na raia. kitu ambacho kitaleta misugoano kwenye jamii.

point yangu ya mwisho. Huu ni mtazomo wangu (and I stand to be corrected). Labda mheshimiwa anafanya hivi kwa nia ya baadaye kuwa Iddi Amini wetu. Make hata Idd Amini alianza hivi kuwapa jeshi na polisi mamlaka makubwa kupitiliza. Akaanzisha research bureau na matokeo yake tuliyaona.
 
Back
Top Bottom