Polisi isidai vitambulisho vya mpiga kura kama kigezo cha kupata dhamana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi isidai vitambulisho vya mpiga kura kama kigezo cha kupata dhamana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ntamaholo, Mar 26, 2012.

 1. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,150
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  wakuu!

  Kumekuwa na kawaida ya jeshi la polisi kudai kitambulisho cha mpiga kura kama kigezo mhimu cha mtu kupata dhamana ya polisi. Hali hii imepelekea vijana wengi kuathirika kwa kupoteza vitambulisho vyao na hivyo kuwa kikwazo kushiriki uchaguzi.

  Mifano iko wazi kwa uchaguzi wa 2010, ambapo kati ya watu waliojiandikisha kupiga kura 20,137,303 ni wapiga kura 8,000 na ushehe waliojitokeza kupiga kura.

  Pamoja na sababu za vifo, kuhama maeneo na wengine kuona hakuna jipya kwenye siasa, ni dhahiri kuwa idadi ya ambao hawakutokea kupiga kura kwa kutokuwa na vitambulisho ni kubwa zaidi. Wengi wao ni vijana.

  Sababu ya wao kutokuwa na vitambulisho vya kupiga kura ilihali wamejiandikisha kupiga kura ni wengi wao kuvitelekeza vituo vya polisi walikofikishwa kwa tuhuma mbalimbali. Mtu akitoka selo, hakumbuki kuuliza kitambulisho, mtu akiomba dhamana, hata kama kesi itamalizika, huwa hawadai vitambulisho vyao pamoja na kuwa PPR zinaonesha walikabidhi vitambulisho.

  Kinachosababisha haya, mtu hajui haki zake awapo polisi na hivyo huogopa kudai kitambulisho kwa hofu kuwa kesi inawezwa kuhuishwa, akarudishwa rumande na hivyo kupunguza maneno, ni heri kwake kuacha kudai kitambulisho au mali alizokabidhi CRO, wala hata police loss report hawadai ambayo ingekuwa msaada kwa baadae.

  Hivyo, nawaomba watanzania tuanze kudai mfumo huu kurekebishwa, ikiwezekana, kitambulisho cha mpiga kura kisitumike kama kigezo cha kupata dhamana.Au wadai kivuli na si kitambulisho chenyewe

  nawasilisha
   
 2. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #2
  Mar 27, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,150
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  natoa wito kwa researchers kufanya utafiti kwenye vituo vya polisi waone ni vitambulisho vingapi vitapatikana ili hatua zichukuliwe
   
Loading...