Polisi Iringa wajiandaa kuua mkutano wa Chadema Mufindi

Status
Not open for further replies.
Hivi Tanzania hatuna uwezo wa ku-multi task? Mkutano unafanyika kwa siku nzima? Mbona watu wanaenda kwenye ibada za masaa wakati huu wa sensa? Na CCM walivyo vipofu, wanafurahia unyanyasi wanaofanyiwa raia na polisi bila kujua kuwa 2015 wataenda kwa raia hao hao kuomba kura!

Polisi na TBC wamesaidia sana kukujenga CHADEMA.
 
Nadhani hakuna haja ya muungano maana zenji sio sehemu ya muungano no wonder uzinduzi unaendelea while bara watu wako bize na sensa
 
Duu hii kali!!
Jeshi la polisi ni kama genge la washirikina, kutwa nzima wanatafuta mtu wa kuua tu.

tayari david mwagosi mpasha habari wa ITV amefariki katika vurugu hizo
CHANZO:JIJI LETU ITV SAA KUMI NA MBILI JIONI
 
jeshi la polisi mkoani irinaga na chama cha demokrasia na maendeleo chadema wameshindwa kufikia maafikiano kuhusu makubaliano ya awali ya kuanza kwa mikutano yao baada ya kumalizika kwa zoezi la sensa ya watu na makazi.

Wakati jeshi la polisi wakitaka chadema kusubiri hadi tarehe 8 mwezi huu baada ya muda wa sensa kungezwa chadema wanasema mkutano wao ambao umepangwa kufanyika mafinga wilayani mufindi upo palepale.

kauli za viongozi

rpc iringa, michael kamuhanda.

-nina digrii ya maswala ya kipolisi, chadema hawawezi kutushinda.
-wasipotii agizo letu nakufanya mkutano wao mafinga tutumia uwezo wetu wote kuhakikisha tunawadhibiti.


benson kigaila.........

Wamezuia mkutano wetu kwa kisingizio cha sensa, wakati bububu zanziba leo kuta uzinduzi wa kampeni za uchaguzi,je huko hakuna sensa?

-liwalo na liwe mkutano leo lazima ufanyike mafinga.

Dk. Slaa........

Kauli ya benson ndo msimamo wa chadema.

-nilionge na igp jana kumweleza kuwa tulikubaliana kistaarabu kwahiyo aheshimu makubaliano.
-mkutano wetu leo mafinga lazima ufanyike tumechoshwa na ukandamizaji wa jeshi la poisi.

My take.........
Kama kweli mkutano utafanyika mafinga maafa huenda yakawa makubwa kuliko ilivyokuwa morogoro kwani tayari magari 8 ya polisi yameshakwenda mafinga kupambana na lolote litakalotokea

kweli mmetumia uwezo wenu kuwadhibiti......mlianza morogoro,mkaenda tarime na saizi iringa.....kumbukeni nyie polisi mnaishi na sisi mitaani huku huku mtaumia !!
 
Asiye fuata maagizo ya serikali ni mpuuzi ndo mlivyokuwa mnasema wakati Watu wanakataa kuhesabiwa Leo na nyie mmekataa maagizo ya serikali.What comes around goes around andamaneni Kama hamjaacha meno chini
Maagizo gani ya serikali? By the way It is "what goes around, comes around"
Policcm ni WAUAJI, hakuna NENO la kuwatetea. SOON watu watakuwa sugu na hizo TEAR GAS, ambazo madhara yake huenea sehemu kubwa zaidi ya hayo maandamano. Kwanini wasingewaacha waandamane kama kulikuwa hakuna uvunjaji wa Amani. Then kesho au Usiku wangewaita Viongozi na kuwafungulia mashtaka. Simple, no blood, no tears. Policcm wameshindwa kazi
 
Mkuu ULICHOKIONA NDICHO KILICHOTOKEA LEO HUKO MUFINDI, R.I.P DAVID MWANGOSI
 
mkuu wewe unaweza ukawa mtabili. hongera sana. Mia

Hongera ya nini? Kwa yeyote mwenye akili timamu haya ndio atakayotegemea. POLISI SASA NI GENGE LA MAJAMBAZI WAUAJI WA HATARI SANA, NI TISHIO KWA USALAMA WETU SIO WALINZI TENA!
 
Kama Zanzibar kuna mkutano wa SSM je huu wa CDM una kitu gani usifanyike? Double standards. Ila ningekuwa na ndugu yangu au mtoto askari au polisi wa Tanzania ningejilaumu sana. Ninamshukuru sana Mungu watoto wangu hawakufanya kazi hizi za uuaji usio na hatia.
 
Ccm itaendelea kutawala kiulaini sana maana imeshafanikiwa kuwagawa watanzania kwa misingi ya udini, ukabila, matijiri na masikini. Comment zilizomo humu ni dhahiri watanzania sio kitu kimoja, hakika furaha ya ccm ni kuona wtz hawaungani badala yake wanazodoana wenyewe kwa wenyewe.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom