Polisi imewaonya waendesha pikipiki (bodaboda) wanaochakachua vyombo hivyo ili vitoe mlio mithili ya bomu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
MKUU wa Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha, Solomon Mwangamilo amewaonya waendesha pikipiki (bodaboda) wanaochakachua vyombo hivyo ili vitoe mlio mithili ya bomu.

Amewataka waache mara moja, la sivyo watakamatwa katika operesheni maalumu itakayofanyika wakati wowote kuanzia sasa. Alisema hayo katika kikao kazi kilichozungumzia changamoto za usafiri wa bajaji na pikipiki kwa lengo la kupunguza ajali za barabarani.

Solomon alisema milio hiyo imekuwa kero na inaleta mshtuko kwa wasiopenda kelele. Wakati mwingine milio hiyo imesababisha vifo kwa watu wenye maradhi ya moyo.

Alisema vyombo hivyo vinatengenezwa viwandani vizuri, lakini madereva hao wanazichakachua na kuanza kusumbua mitaani na barabarani kwa kupiga ovyo milio hiyo.

"Kweli hii imekuwa kero kubwa maana kama kuna mtu mwenye ugonjwa wa moyo au hospitalini, inaleta shida, hata mimi mwenyewe juzi kidogo nikimbie, nilikuwa mahali nikasikia mlio kama bomu kuangalia pikipiki imeshakimbia," alisema.

Alisema kutokana na malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa mengi, jeshi hilo limejipanga kuendesha operesheni ya kuzikagua pikipiki hizo zilizochakachuliwa ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.

Alisema wameanza kutoa elimu kwenye vijiwe vya bajaji na pikipiki ili kupunguza ajali barabarani ambazo nyingi zinasababishwa na madereva wa vyombo hivyo kutojua sheria za usalama barabarani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Salum Hamduni alisema ni vyema kila mmoja wao, atii sheria za usalama barabarani, ili kutolazimisha jeshi hilo kutumia nguvu kwao.

"Tiini sheria kwani sipendi kutumia nguvu sana kwenu, naomba kila mmoja atii na kuzifuata sheria za barabarani, ili mkoa wetu tupunguze ajali," alisema.

Alisema matukio ya ajali ni mengi; na mengi yanasababishwa na madereva wa bajaji na pikipiki.

"Kutoka Januari hadi Novemba mwaka huu jumla ya ajali 647 zilitokea na katika ajali hizo watu 63 walipoteza maisha, majeruhi ni 60 na 99 walipata majeraha madogo. Lakini pia kuna ajali 924 ndogondogo zilitokea zilizosababishwa na bajaji na pikipiki,"alieleza.
 
Mbona Wamechelewa Police?

Walikuwa wapi miaka yote, ama watunga sheria ya mlio tu
 
Ila kusema ukweli kale kamlio kanakera sana hata kama huna ugonjwa wa moyo
 
Ukimamshika akikuambie nipeleke mahakamani utatumia kitu gani kama ushahidi?

Nijuavyo mimi ni kwamba pikipiki yoyote ile unaweza kuifanya itoe ule mlio wakati wowote bila kuiweka alama.

Hawa bodaboda ni kama special group persons, hivyo tuwachukulie madhaifu yao. Wanakutana na kero nyingi road kutoka kwa polisi(tigo).

Bodaboda ni watu muhimu sana.
 
Paaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!
Kuna Mkoa fulani waliwaonya, sasa bodaboda wakajifanya wakaidi kama kawaida yao. Mkuu akaanzisha operation kisiri. Unapiga hapa paaaa!!!!!, huna habari namba yako imechukuliwa.

Baada ya muda, raia anakukodi: "Naomba mipeleke kituoni". Priiiiiiii!!! tap, kituoni, "nisubiri", ghafla afande mdada traffic, " aisee hebu zungusha pikipiki yako kule nyuma" . Inakuja kamera, "Wewe si ndio huyu? " Risiti yako hii hapa. Paki pikipiki yako palee. Uje na pay in sleep ya bank au wakala'' . Unabaki umebung'aa unang'aa macho
 
MKUU wa Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha, Solomon Mwangamilo amewaonya waendesha pikipiki (bodaboda) wanaochakachua vyombo hivyo ili vitoe mlio mithili ya bomu.

Amewataka waache mara moja, la sivyo watakamatwa katika operesheni maalumu itakayofanyika wakati wowote kuanzia sasa. Alisema hayo katika kikao kazi kilichozungumzia changamoto za usafiri wa bajaji na pikipiki kwa lengo la kupunguza ajali za barabarani.

Solomon alisema milio hiyo imekuwa kero na inaleta mshtuko kwa wasiopenda kelele. Wakati mwingine milio hiyo imesababisha vifo kwa watu wenye maradhi ya moyo.

Alisema vyombo hivyo vinatengenezwa viwandani vizuri, lakini madereva hao wanazichakachua na kuanza kusumbua mitaani na barabarani kwa kupiga ovyo milio hiyo.

"Kweli hii imekuwa kero kubwa maana kama kuna mtu mwenye ugonjwa wa moyo au hospitalini, inaleta shida, hata mimi mwenyewe juzi kidogo nikimbie, nilikuwa mahali nikasikia mlio kama bomu kuangalia pikipiki imeshakimbia," alisema.

Alisema kutokana na malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa mengi, jeshi hilo limejipanga kuendesha operesheni ya kuzikagua pikipiki hizo zilizochakachuliwa ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.

Alisema wameanza kutoa elimu kwenye vijiwe vya bajaji na pikipiki ili kupunguza ajali barabarani ambazo nyingi zinasababishwa na madereva wa vyombo hivyo kutojua sheria za usalama barabarani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Salum Hamduni alisema ni vyema kila mmoja wao, atii sheria za usalama barabarani, ili kutolazimisha jeshi hilo kutumia nguvu kwao.

"Tiini sheria kwani sipendi kutumia nguvu sana kwenu, naomba kila mmoja atii na kuzifuata sheria za barabarani, ili mkoa wetu tupunguze ajali," alisema.

Alisema matukio ya ajali ni mengi; na mengi yanasababishwa na madereva wa bajaji na pikipiki.

"Kutoka Januari hadi Novemba mwaka huu jumla ya ajali 647 zilitokea na katika ajali hizo watu 63 walipoteza maisha, majeruhi ni 60 na 99 walipata majeraha madogo. Lakini pia kuna ajali 924 ndogondogo zilitokea zilizosababishwa na bajaji na pikipiki,"alieleza.
Hahaha kweli wamezidi
 
Raha anaipata yule anaendesha unajihisi kama unaendesha zile pikipiki za bomba mbili..

Wasiwasahau na watu wa alteza
 
Kwa nini wanaonya ? Kwa nini hawakamati ? Kila siku onyo pnyo onyo WTF ? Watu wanakufa mnaonya, ...
 
Kama hivi sasa ukienda kwenye vituo vya polisi unakutana na utitiri wa pikipiki je hiyo sheria ikianza kufanya kazi? halafu nyie madereva wa bodaboda hivi mnapata raha gani mkifanya huo upuuzi.
 
Bodaboda wajisajili kwa vituo... Wapewe stika maalumu za namba za vituo. Madereva wavae reflector zenye namba ya kituo na Pikipiki.

Wamiliki wawe liable na Uhalali wa dereva anayeendesha... Kama hawawezi wakatie bima kubwa.. ili wanaposababisha ajali za kujitakia wahanga walipwe au wafidiwe substantially.

Wakisababisha ajali za kujitakia kwa mwendo kasi mitaani, maeneo ya shule, au penye msongamano.. washtakiwe kwa Attempted murder..

Akisababisha ajali na hana Leseni; mwenye chombo aende jela. Adabu itarudi... Hiyo iwe vivyo hivyo kwa wanaotumia high beams usiku mnapopishana.. au madereva wa serikali wanaoovertake hovyo.. heshima itarejea barabarani.

Watanzania wenye afya, furaha na usalama ndio Rasilimali namba moja ya Taifa hili. Tupa kule Tembo na milima na Dhahabu. Ni watu kwanza.
 
Pikipiki zenye milio mikubwa bi kero nchi nzima. Hilo jambo lifanyiwe kazi nchi nzima.
 
Back
Top Bottom