Polisi huwa wanapitia changamoto gani kwenye kazi yao? Kenya 2000 wana matatizo ya kiakili yasiyoruhusu kuendelea kubaki kazini!

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,444
7,808
Yawezekana badala ya kuwa tunawesema kila siku labda iangaliwe namna ya kusaidiwa au tunawashikia bango watu ambao akili zao haziko sawia. Hata hapa kwetu zipo hizi shida labda tu hawajazifanyia utafiti. Unakutana na polisi jambo la kawaida lakini mtu anakuwa mkali na kutumia nguvu kupitiliza, unapata ghadhabu kumbe mhusika akili zake haziko sawa.

=====

Mkuu wa huduma ya kitaifa ya Polisi nchini Kenya Inspekta Jenerali Hilary Mutyambai amesema takribani Maafisa 2,000 wa Polisi wa Kenya wana matatizo ya afya ya akili na kwamba hawana uwezo wa kiakili wa kufanya kazi yao.

Amesema wamebaini jambo hilo la kushangaza baada ya kuwafanyia uchunguzi wa kimatibabu Maafisa wote wa Polisi, Kenya ina Maafisa 100,000 wa polisi wanaofanya kazi chini ya Huduma ya Kitaifa ya Polisi ambapo ripoti hii inakuja huku kukiwa na ongezeko la idadi ya matukio ya Polisi kujiua kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo msongo wa mawazo.

Mutyambai amesema shughuli ya kuwaondoa kazini baadhi ya Polisi hao wenye matatizo ya afya ya akili imeanza kwa kuzingatia umuhimu wa kuwa na Polisi walio sawa kiakili "Zana yetu ya kazi ni bunduki na risasi moja inapopigwa madhara yake ni makubwa"

Siku za hivi karibuni Kumekuwa na wasiwasi unaoongezeka juu ya afya ya akili ya Polisi ambapo Serikali ya Kenya imeanza kulishughulikia hilo kwa kuanzisha Bodi ya Kitaalamu ya Afya inayojumuisha Washauri na Madaktari wa akili walioidhinishwa na Wizara ya Afya kutoa huduma za afya ya akili.
 
Magufuli, Kingai, Jumanne, na like genge lao wote ukiwatafakari Hawa no watu wenye akili timamu? Lazima watakuwa wagonjwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom