Polisi huwa na kadi za CCM wawapo Kazini

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
May 9, 2007
3,832
2,790
Hakika kama huamini utaamini hili ninalosema, kabla ya kuanzisha mfumo wa vyama vingi ulitolewa mwito kwa vyombo vya usalama kujihusisha na siasa. Kadri siku zilivyosonga mbele mwitikio wa wananchi kwa vyama vya upinzani umekuwa ukiongezeka hivyo kupunguza idadi ya wanachama wa CCM toka katika makabrasha yake kwa sababu nyingi moja wapo wengi wao kuona chama cha CCM kukosa mwelekeo, kupoteza dira nk.

Mauaji yaliyoshamiri hivi karibuni dhidi ya wananchi wanaoviunga vyama vya upinzani yameongezeka sana, hii inaashiria kuwa askari polisi bado wana itikadi ya chama cha CCM japo kadi hawana. Kadi za chama hiki kwa polisi hawa ziko mioyoni mwao. Wanazo kwa njia mbili aidha kwa matakwa yao yasiyo na maslahi au kwa kulazimishwa na viongozi waandamizi wa CCM.

Tunawataka Polisi waachane na tabia ya kuegemea upande mmoja wa chama wawapo kazini kwani kama tunavyoona kuna athari kubwa sana kwa maisha ya raia. Aidha tunawataka wanasiasa wa CCM waache kuwatumia polisi kulazimisha wananchi kukiunga mkono chama cha CCM.
 
Huo ndio ukweli kabisa. Polisi wa Tanzania ni Wana-CCM. Lakini, hakuna marefu yasiyo na ncha. Ipo siku tu, haya yote yatakwisha.
 
Back
Top Bottom