Polisi: Huu sasa ni wakati wenu wa kujivua gamba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi: Huu sasa ni wakati wenu wa kujivua gamba

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by babalao 2, Sep 13, 2012.

 1. babalao 2

  babalao 2 JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,218
  Likes Received: 1,270
  Trophy Points: 280
  Habarini wandugu, Leo asubuhi nimesikiliza maoni ya bwana mmoja kuhusu polisi na wajibu wao hakika amenifurahisha.
  Kwanza kabisa ametolea mfano polisi wa mataifa yaliyoendelea jinsi wanavotimiza wajibu wao kwa haki ili kukwepa baadae kugeuziwa kibao.
  Mfano polisi anapomkamata mtuhumiwa
  (1). Anatakiwa awe na vitambulisho vinavyomtambulisha yeye ni nani.
  (2). Wajibu wa kumueleza mtuhumiwa ni kwa nini anakamatwa.
  (3). Kumueleza mtuhumiwa ni nini haki zake wakati wa kupelekwa kituoni.
  (4). Kutotumia nguvu na vitisho wakati wa kumpeleka mtuhumiwa kama yeye hakupinga kwenda kwa hiari yake.
  (5). Akimfikisha kituoni mtuhumiwa huelezwa tena haki zake upya na huulizwa iwapo polisi walitumia nguvu wakati wa kumleta kituoni.
  Kwa kweli kama polisi wetu wangetumia njia hizo hapo juu hakika wangekua marafiki na raia.
  Kinyume chake tunashuhudia kila cku polisi wakitumia nguvu na vitisho pale wanapomkamata mtuhumiwa na tena wengine bila hata kujitambulisha huku wakijua wamevalia kiraia.
  Sasa fika kituoni utaambiwa kwa lugha kali vua viatu toa mkanda na vitisho vingine vingi.
  Mtuhumiwa yampasa kujua haki zake pale kituoni kama muda wa kukaa pale kabla ya kufikishwa mahakamani uwepo wa wakili wake wakati wa kutoa maelezo kama ana wakili na mengine yanayostahili pale kama haki yake.
  Pia polisi ama wanajua au hawajui ni kipi kifanyike na kwa wakati gani ili kuepusha vurugu na kutoaminiwa na wananchi kama ilivo sasa.
  Tunataka polisi mjue wajibu wenu ili mjenge imani mpya kwa wananchi.
  Kwa kweli ni maoni mema kwa jeshi la polisi kujivua gamba.
   
 2. N

  Ndyali JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,222
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Polisiccm hawawezi kufuata utaratibu kwa sababu serikari inayotawala inawatumia kutawala kwa mabavu huku ikiwapa mishahara kiduchu,lakini kwakuwapumbaza kuwa polisi wako juu ya sheria za nchi. Polisi wa tanzania wanaridhika sana na utendaji wao wa kazi za dhuruma (rushwa ya kurazimisha kwa mabavu) kwa watuhumiwa na wanaobambikiziwa kesi.
   
 3. n

  nyantella JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Ndyali!
  sii police wote ni wabaya! tuwape heshima yao maana sisi pia wananchi hatuwasaidii kufanya kazi ya vizuri hatuwaheshimu, tunawadharau saana. cha msingi ukitaka kujua umuhimu wa police, nenda katembelee kituo chochote cha police popote nchini, kaa muda japo nusu saa utagundua police ni sawa na hospital! kila dakika watu wanakuja na matatizo yao mengine wala hayahusu police lakini wanapelekewa wao, halafu police wenyewe kwa sasa ni vijana wadogo sana, wanalipwa pesa kiduchu!.
  ushauri wangu, tuwapende na kuwaheshimu kwani nao ni binadamu kama sisi only that wako in uniform na wanafanyakazi kwa amri hata kama ni ya kijinga, amri yoyote ya kijeshi ni amri halali! haijadiliwi! ndio maana ukiambiwa mguuuu pande!! huulizi kwanini? askari akiamriwa anatekeleza halafu matokeo anajibu aliyetoa amri. kwa mfano ile kule nyololo aliyetoa amri anatakiwa kuwajibika pia!
   
 4. G

  Gwakisa Mwandule JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 520
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jambo la kwanza la kujua ni kwamba jeshi la polisi sio moja kama tunavyoliona kwa nje au sheria inavyolitaka na inavyofahamika kwa watanzania!Jeshi la polisi limegawanywa sehemu tatu!1)Wakubwa wa jeshi ambao ni IGP,makamishna na makamanda wa mikoa hawa wanakaa pamoja na wanasiasa wa chama tawala wanatabia za kisiasa na kama kochi la kukalia la wanasiasa na sehemu muhimu ya watawala wa CCM na serkali hii ovu!Wanapokea posho kubwakubwa bila kazi za msingi wanapewa feva za kimaisha kama wanazopewa mawaziri au makamishna wa wizara na maisha yao hujitafsiri moja kwa moja kwenye mfumo wa chama tawala na wengi hawana kazi za kiuweledi hivyo kazi zao hutegemea na maagizo gani kutoka kwa mtawala atapenda yatekelezwe na polisi hivyo yeye hutoa oda kwa waliochini yake!
  (2)Makamanda wa wilaya na maofisa wao wanaohusika na operation ngazi za wilaya ambao hupokea maagizo ya watawala kupitia viongozi wao ngazi za taifa au mikoa na kutakiwa kuyatekeleza bila kujali madhara yake kwa taifa!Kimaslahi wanategemea sana rushwa kutoka kwa maofisa waliopo chini yao mfano trafiki wapelelezi pia hutegemea saana mapato kutoka kwa majambazi ambao huazima silaha kwa polisi wakawaida na dawa za kulevya kwenye maeneo yao nk.Hawana ushawishi sana wakisiasa maana hutegemea na hutenda kwa kufuata wakubwa walioko ngazi za juu au maagizo ya chama tawala ngazi ya wilaya maana hayo huwa ni mapenzi ya mabosi wao ngazi za juu pia!Wanatabia ya kujipendekeza saaana kwa waliojuu yao na hutegemea zawadi za vyeo kwa kutekeleza kwa kiwango cha juu yale wanaotakiwa kuyafanya hata kama ni kuua watu wote ktk wilaya!
  (3) Hawa ni askari woote waliochini ya hao hapo juu ikiwa ni pamoja na wale aina ya Pacificus Cleofas Simon ambao ndio huwa vitendea kazi vya hao walioko huko juu ngazi ya wilaya,hawaheshimiani maana heshima hutegemea na kamanda wa wilaya anampenda nani kati yao,hawakusoma vya kutosha wengi ni kutoka familia duni za walala hoi hufundishwa kutumia nguvu,kunyanyasa watu kubambika kesi hata zile za mauaji watu wasiohata husika ili kujipatia rushwa kwa nguvu,wanamishahara midogo saana na hufanya hata ujambazi ili waweze kuendesha maisha,hufanya urafiki na wahalifu ili wapewe angalau bia moja,huchochea maovu katika jamii ili waweze kuhongwa na wahusika chochote kitu na hawawezi kabisa kutumia akili katika kazi zao na ndio maana husikika aidha wameiba wanauza bangi nk.
  Hivyo ukitaka kuwakomboa watu hawa ni lazima kwanza uiondoe Ccm madarakani kwa nguvu ya umma na jeshi hili lisukwe upyaa na wala sio hawa waliopo sasa!!!Amin
   
 5. N

  Ndyali JF-Expert Member

  #5
  Sep 13, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,222
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Mkuu Nyantella, kama swala ni la Amri na ni lazima watekeleze, uzuri wa baadhi ya polisi utatoka wapi? Uzuri ni vitendo sio kudhania, Kwani kama ni wazuri lakini wakaamrishwa kunipiga risasi raia nisie na hatia niendelee kuwaita wazuri kwa kuwa Nyantella ameniaminisha hivyo? Tatizo la TZ. ni mfumo na mfumo ukiwa mbovu wa polisi wa tz, watu hawana chaguo la kupata huduma za kipolisi kwingine isipokuwa kwa hawahawa polisi wanaowageuza watz maskini kuwa kipato cha kunenepeshea vitumbo vyao.
   
 6. kisugujira

  kisugujira JF-Expert Member

  #6
  Sep 13, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 769
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Babalao,

  Maoni uliyoyatoa ndivyo askari polisi wanavyotakiwa kufanya na kuyafuata kama sehemu ya mafunzo waliyoyapata. Taratibu za kazi na sheria nyingi za jeshi la polisi hapa nchini zimetokana na athari au matokeo ya ukoloni.

  Kinachoshangaza ni kuwa askari hawa wanafundishwa na kuiga utii usio na manufaa kwa raia wanaotakiwa kuwalinda na mali zao.Ni nini faida ya kuwa na askari polisi wala rushwa,wauaji na wanaobambikiza watu kesi? Na hii si kwa polisi tu,hata kwa viongozi waliopewa dhamana ya kuliongoza Taifa letu!

  Hivi kweli asasi hii inatakiwa kujirekebisha na kuundiwa tume hata kama ukweli unafahamika kila baada ya maafa kutokea? Hizi ni rasharasha tu.Tusiombe gharika likatupata tutashindwa kupata sehemu ya kukimbilia na muda wa kuunda kamati na tume hautakuwepo tena.

  Wako wapi wazee wenye busara wasio na woga,manabii wa kweli na siyo wa uwongo,kwa maana imekwisha andikwa,watakaoweza kukemea maovu haya. Je,sisi sote tumekosa maarifa?
   
 7. babalao 2

  babalao 2 JF-Expert Member

  #7
  Sep 13, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,218
  Likes Received: 1,270
  Trophy Points: 280
  Mkuu maarifa yapo kwa wengi ila tatizo ni WOGA utayasemea wapi kwa ukakamavu ilihali watz tumejawa na hofu mioyoni mwetu.
  Si unajua tanzania ni mfumo wa watawala kuogopwa na si watawala kuogopa wananchi ni suala la kupeana elimu ya utambuzi tujijue sisi ni nani kwanza.
   
Loading...