POLISI hiyo intelijensia yenu iko wapi kuelekea July 23? Zuieni mkutano wa CCM.!

REAGAN C.MABOGO

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
1,269
1,007
Polisi waliwafanyia vurugu wana UKAWA/CHADEMA kule Kahama kwa hoja ya kuwepo habari kuwa kuna vyama vilipanga kuwajibu wenzao. Hoja mfu kabisa hiyo! Hali hiyo hata hivyo ndiyo inayoendelea kuelekea mkutano wa CCM July 23.

Haishangazi kuona jeshi la polisi wakishindwa kupiga marufuku huo mkutano licha ya habari kuenea kuwa BAVICHA wamejipanga kikamilifu na kishujaa na tena wameapa kuhakikisha wanauzuia huo mkutano usifanyike. Huku vijana wa CCM nao wakidai eti watawadhibiti BAVICHA.

Maana yake kutakuwa au huenda kukawa na mapigano kati ya pande hizo mbili. Badala yake polisi wanaapa kuwazuia BAVICHA na watanzania wengine watakaoenda Dodoma kuuzuia huo mkutano. Wanaahidi kuulinda kwa nguvu yoyote.! SWALI: "intelijensia" yenu iko wapi? Kwa nini hamzuii huo mkutano licha ya kuwepo habari zote hizo?!

JIBU: hamuwezi kuuzuia kwa kuwa amri zote zinatoka CCM, na ndio wanaowalipa mshahara na kuwapandisha vyeo na kuwapa nyongeza ya mshahara na marupu rupu. Ushauri wangu kwenu , acheni kushangilia mtego wa panya.
 
Tayari vijana wa BAVICHA tumeshaanza kutinga kanda ya kati, kuhakikisha jeshi la polisi linapata msaada wa raia wema kuhakikisha siasa haifanyiki mpaka 2020.
 
Back
Top Bottom