Polisi hawana jukumu la kuzuia uvunjivu wa amani?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,283
33,887
Mara nyingi vyama vya siasa huzuiwa kufanya shughuli zake kwa maelezo toka polisi kwamba "taarifa" za kiintelejensia zinaonesha kwamba kutakuwa na uvunjivu wa amani" kwenye shughuli husika.

Huwa najiuliza kama Polisi imepata "taarifa" hizo za "kiintelejensia" inakuwaje huwa hatutajiwi hao wataka kuvunja amani ni kina nani na ni kwa nini mara zote hawakamatwi na kushitakiwa kwa kupanga njama za kuvunja amani?

Jee kupambana na wavunja amani si ndiyo kazi ya Polisi. Yaani ni kwa nini Polisi wasiwazuie hao wataka kuvunja amani badala ya kuwazuia watu wema kufanya mambo yao. Siku Polisi wakiambiwa kuna Mkutano wa Kamati Kuu ya CCM au Halmashauri Kuu ya chama hicho kuna viashiria vya kuvunja amani, nao pia watauzuia?

Kwa nini inaonekana kama vile Polisi wanaogopa kupambana na hao wanaotaka "kuvunja amani" badala yake njia rahisi wanayoona inafaa kuchukua ni kuvunja mikutano ya vyama vya Upinzani?

Lakini pia Polisi hao hao wanaozuia mikutano kwa madai ya kuwepo viashiria vya uvunjivu wa amani, inashangaza wanapokuwa na nguvu za ajabu kuzuia mikutano hiyo badala ya kuitumia nguvu hiyo hiyo kupambana na wanaotaka kuvunja amani?

Idadi ya Magari na Polisi wanaokuwepo wakati wa harakati za kuvunja ama kuzuia mkutano wa chama cha upinzani, kwa nini nguvu hiyo isitumike kuzuia hao wahalifu wanaotaka kuvunja amani?
 
Back
Top Bottom