Joel Johansen
JF-Expert Member
- May 12, 2016
- 242
- 319
Hi guys,
Nina jambo nahitaji ushauri.
Mwaka juzi nikiwa mkoa flani (sitautaja jina) kwa kazi binafsi, niliingia kwenye tatizo na watu watatu ambao ni Expats (wageni wa nje walio kikazi hapa). Wawili nilichukua pesa zao; laki 5 kutoka kwa kila mmoja kama malipo ya huduma niliyoitoa, bahati mbaya kazi ile ilinishinda, na mmoja alikuwa mwajiri wangu tuliepishana kauli hadi kufikia kutukanana kwa simu na emails. Please note kuwa pia alikuwa ni rafiki yao wale wawili.
Kwa pamoja kwa msaada wa mtanzania mmoja au wawili (boyfriends), walilipeleka swala Polisi na mimi nikawekwa mahabusu wiki nzima isivyo halali kwasababu kwa kesi ya wale wadai wawili, kama tungeenda mahakamani, nisingetakiwa kuwarefund 100% kwasababu tayari kazi ilikuwa imeshafanywa ila yenye upungufu wa ki-technical, hivyo haki ilikuwa upande wangu kuongezewa muda kurekebisha mapungufu yale sawasawa na nature ya kazi ilivyo.
Mtu ambaye kesi yake ilikuwa serious (kwa mjibu wa Polisi ni ya yule tuliyetukanana na ushahidi wa SMS na Emails ulikuwepo).
Polisi wakafikia muafaka kwa kusema kwamba, 1) tusiwasiliane tena mimi na wale washtaki watatu, 2) nilipe milioni 1 kama refund kwa wale washtaki wawili, 3) watajua watakavyo malizana na yule mmoja mwenye kesi ya kutukwana/watampotezea. Basi nikalipa, na kesi ikaisha hivyo na nikahama huo mji.
Baada ya mwaka na kitu baadae, nimekuja kuskia kuwa Askari wale (kitengo cha upelelezi, hapo kituo kikuu cha polisi) hawakuwapa hiyo hela wale wateja wawili, na pia, waliwaambia kuwa nimefungwa, yaani sipo uraiani na niliwekwa hatiani.
Nilijiskia vibaya kuskia nimetangazwa hivyo, isitoshe kwa jinsi walivyokuwa wanalazimisha hadi senti ya mwisho ya kutolea pesa zile kwa njia ya simu. Na pia hadi sasa wale wateja bado wanakinyongo wakidai kuwa waliwahi kudhurumiwa.
Kwa maelezo hayo utakuwa umeelewa. Hivyo naomba ushauri, niwachukulie hatua gani wale Polisi? pia nijisafisheje kwa wale washtaki wawili? vipi kuhusu yule mwenye kesi ya matusi (sijui walimalizana nae vipi, lakini pia anajua kuwa niko jela), itakuwaje siku tukionana?
Ntashukuru kwa maoni, ntafanyia kazi maoni yako