Polisi: Hatuna taarifa ya kukamatwa kwa Kijana aliyetuma picha za Nyufa za Hosteli

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
mambosasa.jpg

Jeshi la Polisi Kanda ya Dar es Salaam, limesema halina taarifa za kukamatwa kwa mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Kumbusho Dawson kwa tuhuma za kupiga picha hosteli mpya za chuo hicho (JPM) Block A, zinazoonyesha nyufa katika jengo hilo.

Awali, taarifa za kukamatwa kwa Kumbusho, zilithibitishwa na Waziri Mstaafu wa Mikopo chuoni hapo, Shitindi Venance ambaye alidai alipelekwa kupelekwa kituo Kikuu cha Polisi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema, jeshi lake bado halijapata taarifa kamili kuhusu tukio hilo na endapo watapata taarifa hizo na watazifanyia uchunguzi wa kina na kutatoa taarifa.

Wakati huo huo, Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), umesema baada ya ukaguzi wa wataalamu wao wamebaini nyufa hizo ni za kawaida katika taaluma ya wabunifu majengo.

Mkurugenzi Mtendaji wa TBA, Elius Mwakalinga amesema kitaaluma majengo mapana huwekewa nafasi ambayo hutenganisha na kuwa sehemu mbili ambapo hali hiyo husaidia kuruhusu jengo kupumua inapotokea hitilafu ya udongo kutanuka na kusinyaa kutokana na hali ya hewa.

“Kutokea kwa nyufa katika jengo letu hili si kwa sababu ya upungufu wa ubunifu ujenzi bali umetokea katika maeneo yaliyokusudiwa na kitaaluma hutokea hivyo, hazina madhara,” amesema Mwakalinga.

CHANZO: Mtanzania

Habari zaidi soma=>News Alert: - Kijana aliyetuma picha za Nyufa za Hosteli za Magufuli UDSM akamatwa na Jeshi la Polisi
 
Wakati huo huo, Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), umesema baada ya ukaguzi wa wataalamu wao wamebaini nyufa hizo ni za kawaida katika taaluma ya wabunifu majengo.

Mkurugenzi Mtendaji wa TBA, Elius Mwakalinga amesema kitaaluma majengo mapana huwekewa nafasi ambayo hutenganisha na kuwa sehemu mbili ambapo hali hiyo husaidia kuruhusu jengo kupumua inapotokea hitilafu ya udongo kutanuka na kusinyaa kutokana na hali ya hewa.

“Kutokea kwa nyufa katika jengo letu hili si kwa sababu ya upungufu wa ubunifu ujenzi bali umetokea katika maeneo yaliyokusudiwa na kitaaluma hutokea hivyo, hazina madhara,” amesema Mwakalinga.

Sijawahi kusikia hata siku moja kuwa nyuva ni moja katika ubunifu wa majengo marefu,,,,,,,:D,,,hao waliojenga hizo nyumba inabidi washtakiwe kwa kosa la kutaka kuuwa kwa makusudi..,na kumtapeli raisi mtukufu John Pombe Magufuli
 
Mkuu wa Polisi kituo cha UDSM kathibitisha kukamatwa.

Halafu Jeshi linasema hawana taarifa.

Au wanahamisha magoli juu juu?

Huenda wameshauriana, maana kama wanapitia maoni yetu humu lazima washtuke
 
Mkurugenzi Mtendaji wa TBA, Elius Mwakalinga amesema kitaaluma majengo mapana huwekewa nafasi ambayo hutenganisha na kuwa sehemu mbili ambapo hali hiyo husaidia kuruhusu jengo kupumua inapotokea hitilafu ya udongo kutanuka na kusinyaa kutokana na hali ya hewa.

Ukitazama kwa jicho hiyo siyo nafasi ya kuwekwa, labda aseme nafasi isiyojulikana
 
View attachment 643906

Jeshi la Polisi Kanda ya Dar es Salaam, limesema halina taarifa za kukamatwa kwa mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Kumbusho Dawson kwa tuhuma za kupiga picha hosteli mpya za chuo hicho (JPM) Block A, zinazoonyesha nyufa katika jengo hilo.

Labda imefikia mahali watu wa Usalama wa Taifa wasiruhusiwe kukamata raia hadi wawashirikishe Polisi, just as a check and control matter.
 
Kama vitu ambavyo vinaboa ni kuona kitu cheupe halafu weak justification developed to argue it is black. Hii kitu huwa inaniudhi sana funny enough huu ndio malengo wa wanasiasa wa nchi hizi zisizoendelea
Inakera sana, halafu ndio wasomi eti
 
Nyufa za kawaida? Mbona hapohapo UDSM kuna majengo ya zamani sana na makubwa hayajawahi kupata nyufa za hivo? Na kwa mujibu wa web ya mwananchi, makamu Rais wa DARUSO aamethibitisha kukamatwa kwa mwanafunzi huyo.
 
TBA kazi yao ni ubunifu majengo so most of the workers are architects, sasa wanalazimisha wafanye kazi za civil engineers ambazo wanautaalamu nazo mdogo sana... civil engineer anaweza kuchora ramani lkn si km architect. Na ndio maana tunaambiwa ufa ni kitu cha kawaida
 
Back
Top Bottom