Polisi, hamtatutawanyisha kwa mabomu Kahama Shinyanga?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Kama makada wa CCM,tunajiandaa kisawasawa kwenda Kahama Shinyanga. Kule, kutakuwa na mkutano wa hadhara wenye kubwa hadhira utakaohutubiwa na Mwenyekiti wetu,Dr. John Pombe Magufuli.

Najua kuna katazo lenu la mwanzo. Katazo la mikutano ya hadhara ya kisiasa. Kama jeshi la polisi,hamkuwahi kuliondoa. Nauliza kwa niaba ya makada tutakaokwenda Kahama Shinyanga,hamtatusambaratisha vya kutisha kwa mabomu ya machozi na kutufanya tulie kwa uchungu?

Tuhakikishieni usalama na utulivu utiao wivu kupitia tamko lenu juu ya mikutano ya hadhara ya kisiasa. Tafadhalini polisi wetu,tuondoleeni maswali!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Ma-RPC nao kwa vile bongo zao zina dosari wala hutasikia kitu kama hicho, fanyeni mkutano wenu kwa amani kabisa! Mimi ningekuwa RPC ndo ilikuwa mahali pa kuchukua sifa, yaani unaandika barua ndefu kabisa ya kuupiga marafuku huo mkutano na kwa vile mkulu hana dogo utasikia atakavyo kufagilia. Mara vuuu u-IGP huo hapo!!
 
Kwani wewe ni polisi?

Mzee Tupatupa
 
fanyeni kahama na sisi tunafanya wetu Mwanza.
Kauli ya CUF hiyo ya miaka 1995 (JINO KWA JINO). Wapizani wasilegeze kama CCM wanafanya Kahama wao waitishe mkutano wa Hadhara DAR au ARUSHA hapa ni mwendo wa Jino Kwa Jino tu. Nchi ni ya wananchi wote. Lazima tucheze mechi kwa usawa.
 
Kama makada wa CCM,tunajiandaa kisawasawa kwenda Kahama Shinyanga. Kule, kutakuwa na mkutano wa hadhara wenye kubwa hadhira utakaohutubiwa na Mwenyekiti wetu,Dr. John Pombe Magufuli.

Najua kuna katazo lenu la mwanzo. Katazo la mikutano ya hadhara ya kisiasa. Kama jeshi la polisi,hamkuwahi kuliondoa. Nauliza kwa niaba ya makada tutakaokwenda Kahama Shinyanga,hamtatusambaratisha vya kutisha kwa mabomu ya machozi na kutufanya tulie kwa uchungu?

Tuhakikishieni usalama na utulivu utiao wivu kupitia tamko lenu juu ya mikutano ya hadhara ya kisiasa. Tafadhalini polisi wetu,tuondoleeni maswali!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Kumbuka kuwa Mwenyekiti wa CCM ndiye Rais wa nchi, bwana BAVICHA. By the way uliwadanganya BAVICHA wenzako kuwa Mwenyekiti Magufuli asingechaguliwa, vipi unasemaje sasa?
 
Hamna haja ya kuwatawanya kwani kuna mingine inakuja 1/9/2016 na yote ni ya kisiasa.
 
Kumbuka kuwa Mwenyekiti wa CCM ndiye Rais wa nchi, bwana BAVICHA. By the way uliwadanganya BAVICHA wenzako kuwa Mwenyekiti Magufuli asingechaguliwa, vipi unasemaje sasa?

Sasa kwani kachaguliwa? Yeye kapewa tuu na mtangulizi wake. Hivi hukuona hata sura ya JK ilivyo kuwa ya kebehi pale alipokuwa anatangaza, kura zilizoharibika 0, kura za hapana 0?
Ujifunze kusoma alama za usoni dhidi ya kauli itakusaidia sana hata kwenye familia yako hasa pale mkeo/mumeo atakapo kuambia nimechelewa kurudi nilipitia kumuona mgonjwa na kumbe ni mchepuko.
 
Tatizo lenu BAVICHA mkiishiwa hoja mnaanza viroja. Magufuli amechaguliwa kwa kura 2398, yaani alipata 100% ya kura zote. Kama ni swala la sura tu basi Mbowe anamkebehi Lowassa siku zote, unaona tu sura yake inavyokuwa kila akimtazama Lowassa. Na pia Mbowe anakukejelini nyie siku zote kwa jinis sura yake inavyokuwa wakati anatoa matamko na ndiyo sababu BAVICHA mlipigwa mkwara na Mbowe kutokwenda Dodoma nawote mkanywea.

Sasa hivi mmedanganywa na mmekubali kusimamia UKUTA. Subirini sasa muone jinsi tingatinga litakavyoufyagia huo UKUTA!
 
Back
Top Bottom