POLISI Geita 'wateka', wampiga na kumharibu jicho Mwandishi wa Habari

Pwaaaa

JF-Expert Member
Feb 16, 2013
248
67
Nimepata taarifa za kusikitisha kutoka mkoa wa Geita. Taarifa zinadai kwamba, juzi kati ya saa moja jioni, askari polisi wapatao 8 wakiwa na silaha nzito za kivita-SMG- 'walimteka' kisha kumkamata, wakampiga na kumuumiza vibaya kwa kumpasua mishipa midogo ya damu katika jicho la kushoto, Mwandishi wa habari Salumu Maige, anayeandikia gazeti la Mwananchi na Redio Free Afrika huko Geita. Polisi walikuwa na gari Namba PT 1998-OCD Geita. Mwenye taarifa zaidi atujuze!.
 
IGP nimepisha naye hapa mnazi moja anachekelea tu, nikuomba mungu tu nchi sasa ilipofika.....
 
Poleni waandishi wa habari,Hichi kirusi cha kuwajeruhi na kuwauwa waandishi kumbe bado kipo?
 
Nimepata taarifa za kusikitisha kutoka mkoa wa Geita. Taarifa zinadai kwamba, juzi kati ya saa moja jioni, askari polisi wapatao 8 wakiwa na silaha nzito za kivita-SMG- 'walimteka' kisha kumkamata, wakampiga na kumuumiza vibaya kwa kumpasua mishipa midogo ya damu katika jicho la kushoto, Mwandishi wa habari Salumu Maige, anayeandikia gazeti la Mwananchi na Redio Free Afrika huko Geita. Polisi walikuwa na gari Namba PT 1998-OCD Geita. Mwenye taarifa zaidi atujuze!.

Mkuu ni kweli wamemfanyia unyama sana huyo Mwandishi.
 
Waandishi wenzake wapo wapi toka juzi tusisikie hii habari na kuilaani? .Naona wapo bize kupokea vibahasha na kuandika habari za matamko feki dhidi ya chadema.
Pole sana Salumu Maige , mwenyezi mungu akujaalie upone kwa wepesi.
 
waandishi wenzake wako bussy na kuichafua chadema, ajiuguze mwenyewe, wako bussy sana sijui kama watamsaidia
 
Kwa tabia za waandishi njaa akina Kibanda na kundi lake mie sina huruma hata kidogo .Nimeona leo mtu kaamua kutukana KK ya Chadema kisa mwandishi na maslahi na mgogoro wa Chadema .Polisi wagongeni tu wafuga tumbo hawa .
 
Back
Top Bottom