Polisi FFU Ukonga nimewakosea nini? Nimepigwa mimi,mke wangu na Mama mkwe bila kosa lolote. Nifanyaje kuchukua hatua?

Kibiti yalikua ni matokeo ya mambo kama haya......binadamu atavumilia mambo yote ila sio uonevu
 
Acha kupiga kelele humu hutopata msaada ..nenda karipoti tukio kituo cha polisi au kwa kamanda kanda maalumu .
Sisani kama anapiga kelele, JF ni uwanja mpana wenye watu tofauti, kuandika na kutoa hisia zake ni kufikish ujumbe kwa walengwa,
Ila pia inasijitisha n kuhuzunisha sana, sio tu kuzalikishwa mbele ya mkwe wake, ila kitendo cha kupigwa bila kosa lolote sio sawa kwa nchi Huru na yenye amani kama Tz
 
Hakuna aliye juu ya sheria...kuwa makin..acha uwoga karipoti kwa mkubwa waoo
Hakuna kitakachotokea mkuu,hata akaripoti Kwa IGP bado hakuna msaada wowote atakaoupata,...askari wetu tunawajua vyema Kwa tabia yao ya kubebana na kufichiana maovu,.....kule Arusha mwaka flani mwanajeshi Wa JW aliuwawa maeneo ya majengo juu,kambi nzima ya jeshi ilihamia majengo,wananchi walipigwa wiki nzima,na taarifa zinapelekwa vituo vya polisi na wanaopiga wanajulikana lkn hakuna anaewachukulia hatua....hao watu ndivyo walivyo....wanabebana....haijalishi ni mkubwa au Mdogo,....adhabu yao kubwa watakayoitoa ni kuwahamisha vituo vya kazi wahusika,....kuna askari alimpiga kijana waliomkamata usiku Wa SAA 3 eti wakimtuhumu ni mzururaji huko Babati-manyara mwaka 2007 hadi kumsababishia kifo,amempiga hadharani kwenye rundo LA watu wanaofanya biashara,na watu wamemuona akimpiga,waliokamatwa walikua wa3,mmoja ndo alipigwa sana,..baadae walipoona hali take ni mbaya wakamkimbiza hospitali,lkn wakamfikisha akiwa maiti tayar,....jamaa hata kukamatwa hakukamatwa pamoja na wananchi na ndugu Wa marehemu kuripoti ili jamaa akamatwe,lkn wapi...hadi alipokuja wazir mkuu wakati huo Ndg Lowasa akafanya mkutano Wa hadhara uwanja Wa kwaraa pale na wananchi wakapewa nafasi ya kuuliza maswali na kueleza kero zao,ndipo mmoja alipotema ubuyu Kwa Lowassa kuhusu ishu hiyo,Lowasa akaamrisha RPC amkamate huyo askari Mara moja na amfikishe mahakamani haraka,...jamaa akakamatwa,akakaa jela km mwez akiwa mahabusu,....wakati wananchi wakiamini yupo jela,kumbe alishatolewa cku nyingi na wakamuhamishia Moshi Mjini tens wakampa u traffick maana mm nilimuona Moshi Kwa macho yangu na tukasalimiana.,Leo unamwambia akaripoti?...labda akaripoti Kwa Mungu lkn sio Kwa polisi Hawa tunaowajua....mifano IPO mingi sana
 
ww nende polisi halafu jukua p3 halafu pia kwa wandishi wa abari hama nenda kuwa ofisi za haki za binadamu watakusaidia
 
Inatia huruma sanaaa yani...alafu viongoz waziri anasema eti ni panya road ndo waliopiga raia...hiii serikali ya ajabu kabisa
 
cha kusikitisha wanasahau wao ni wachaxhe sana na wengi wao wanaishi uraiani siku RAIA wakiwachoka watakula kichapo cha haja
 
Jana tarehe 24 Oct hii niliangalia taarifa ya habari, kwa kweli nilihuzunika na kusikitika sana, Yaani nilihuzunika zaidi pale Kamanda Mambosasa aliposema kuwa hao ni wahuni wanaojiita polisi, hivi inawezekana wahuni wa mitaani kujiita polisi? Mbali ya kujiita pia wametumia silaha, magari, uniform za polisi, kwa maana hiyo hao wahuni walikwenda hapo makao makuu ya FFU wakateka hivyo vifaa vya polisi na kuvitumia wao, linawezekana hili kweli?
Naamini Mambosasa ameongea kisiasa tu lakini waliofanya vile ni polisi na sio wahuni kama alivyoongea.
Kuna usemi mmoja kwenye somo la kemia unasema "All alkali are bases but all bases are not alkali" hapa nikiwa na maana kwamba " Polisi wote ni watanzania lakini watanzania wote sio polisi" hivyo ni sawa na kusema " kwenye kundi la polisi kuna wahuni, lakini kwenye kundi la wahuni hakuna polisi ", kauli ya Mambosasa kwakweli sio nzuri kwani watu wameumia na wengine biashara zao kuharibika na wengine wamepoteza vitu vyao vya thamani. Upande wa pili wa shilingi ni kwamba hao Mambosasa alowaita ni wahuni je kama wangeshambuliwa wao angesema kuwa raia wamewashambulia wahuni au polisi? Kila binadamu ana ustahmilivu lakini huwa na kikomo chake. Katika waliojeruhiwa wamo wanajeshi, wamo magereza, je na wote ha wakiamua kufanya mashambulio ya kulipiza hivi ni kweli Ukonga kutakalika? Kwa kweli kauli yake sio nzuri.
Kwako ndugu yangu uliekumbwa na mkasa huu, naomba usamehe tu na wala usifikirie kufanya malipizi wala kitendo chochote kibaya kwani kufanya hovyo sio vizuri na unaweza hata kumdhuru ambae hakuhusika na kitendo hicho. Pole sana.
Hizi ni kazi tu na ni sehemu ya maisha isiwe ni kigezo cha kumuonea Mtanzania mwenzako. Mungu yupo.
 
Umeongea kiuhalisia kabisa mkuu sasa hivi ma RPC wanajibu majibu ya mkato sana wakiongozwa na boss wao mzanaki lkn wajue kuwa na wao ni watanzania tena ndg zao tunaishi nao huku mitaani siku mambo yakiharibika tunaumia wote!!!
Nawashauri wanapoona matukio kama haya wayakemee Mara moja
Tunakumbuka utawala wa Jk ulikuwa ni wa kupiga pesa na watu hawakuwa na sauti lkn kwenye huu utawala ni wa kupigwa hadharani lkn baadaye inakuwa kwamba ni watu wasiojulikana au wahuni

Shame on this government.
 
Wakuu nimesononeka sana,nimeumia na kuaibika sana.Jeshi la polisi kitengo cha FFU pale Ukonga kimenidhalilisha mimi,mke wangu na mama mkwe bila makosa yoyote yale.Nimeumia sana wakuu.

Jana majira ya saa tatu hivi usiku nilikuwa na Mama mkwe na mke wangu,nilikuwa namrudisha Mama mkwe kwao Mazizini ambako ndiko anakoishi.Tulipofika maeneo ya Mombasa njia panda ya kwenda Moshi Bar,niliamua guegesha ili kumnunulia Mama mkwe dawa kwenye duka la dawa linaitwa Waki (J) Phamarcy.

Ajabu ni kuwa,kwa mara ya kwanza nilikuta eneo la Mombasa likuwa halina shamrashamra nilizozizoea,majereta na taa za wauza chips zimezimwa,maduka yamefungwa na vibanda vya chips vina majiko na makalai yenye kukaanga chips yakiwa bila watu,masufulia ya supu ya kongoro yakiwa yanachemka bila walaji wala wauzaji,kidogo nikastuka lakini sikuwa na mtu wa kumuuliza nini kilichojili,kituo cha daladala wala daladala zikawa hazisimami pale Mombasa,iwe za kutoka Banana,Gongo la Mboto au Moshi Bar.

Ile tunashuka tu kwenye gari nikasikia watu wanasema mpo chini ya ulinzi,sikuwa na hili wale lile,kundi la vijana kama watano hadi nane wakiwa na suruali za (mfano) askari wa FFU,na juu wakiwa na mashati ya kiraia wakitusogelea kutokea kwenye eneo la kiza pale Mombasa,sijakaa sawa nikala mtama na kofi la kisogo,mama mkwe akala bakora za mgongo na wife akapigwa mitama na makofi juu.

Sijatulia nikasikia mkanda wa mgongo na kibao kingine cha uso,kosa likawa kuuliza mnatupigia nini na sisi ni raia wema?Tazama huyu ni mke wangu na huyu ni Mama mkwe wangu,tena mgonjwa,mwenye umri sawa na mama zenu,kwanini mnatupiga?Kauli hii ikawa kama ni kuchoche moto,mmoja wao akasema kwani mliyemuua hamkujua kuwa alikuwa na ndugu na wazazi wanaotegemea??

Pale nikawa na wasiwasi labda nimefananishwa na majambazi,au pengine gari langu limehisiwa kwenye tukio la mauwaji na watu walikuwa wananifuatilia sasa nimeingia kwenye mikono yao,nikiwa bado nataka kupata ufafanuzi,jamaa mwingine nilisikia wakimuita kwa jina la Cobra akaniwasha tena mkanda wa mgongo,na teke juu...Wife wangu ni muoga sana,kuona vile akachukua upenyo na kulala mbele kukimbilia kwenye ile pharamcy,bahati mbaya kukawa na dada mle ndani naye kajifungia mlango kuogopa kipigo.

Mimi ilibidi nikomae na mama mkwe nisikimbie,japo nilikuwa na uwezo wa kujinusuru kwa mbio,lakini huruma na mawazo yangu ikawa kwa huyu Mama ambaye ni mtu mzima,ikabidi niwaambie wale jamaa,kama ni askari na mini nina kosa kwanini wasinikamate na kunipeleka kituoni?na kwanini watupige wakati mie sina silaha na wala sijatishia mtu na silaha?Looh...Jamaa akasema unajidai unajua sana sheria eee!!Nikapigwa mkanda mwingine na kofi juu...mangumi na mateke!!

Mama mkwe akabaki kupiga kelele kuwa mtaniulia mwanangu,amekosa nini?kilichosaidia sikuwa nimefunga milango ya gari,mama mkwe akarudi ndani ya gari mbio na mie nikatafuta upenyo wa kurudi mbio mpaka kwenye gari,hapo jamaa wanaendeleza vichapo kwa kila raia anayeshuka au kuonekana lile eneo.

Baada ya pale nikatembeza gari mpaka UEFA Pub/Bar,pale tukakuta napo wamefunga kwa kukimbia kichapo.Si bodaboda wala nani,wote ilikuwa ni dozi tu,waifu tumekuja kukutana home kwa Mama yake.

Aibu hii na uonevu huu umenisikitisha sana,hivi hata kama kuna mauwaji,mimi mkazi wa Tabata Bima ninayemrudisha mkwe wangu kwao ninapigwa kwa sababu gani?Huu utaratibu wa jeshi la polisi kupiga watu hovyo bila hata kuhoji kisa mwenzao ameuwawa umeanza lini??

Tafadhali sana mkuu wa IGP Siro na huyo kamanda wa Kanda Maalumu Dsm,mimi nimepigwa mbele ya mkwe na mke wangu,tena bila kosa lolote,aibu hii sitakufa nayo...Ipo siku tu,haiwezekani jamani tuabishane hivi kwanini??Nashindwa hata kuandika,ila kwa kweli FFU UKONGA mmenionea sana mimi,mke wangu na mkwe wangu.Tumewakosea nini jamaniiiiiiii!??Ipo siku tu..
Pole sana mkuu. Nayaona majonzi yako yalivyo mazito. Hakika utaiona haki yako siku moja endelea kuamini uwepo wa Mungu.
 
Nikisema majambawaxi ndio hayahaya kuna watakatoa povu km wamemeza foma Ndio maana tukiilia timing tutaitungua tu po pote tunapoikuta NYAMBAF KBS ninausongo na hii mijitu yaani basi tu. Vichwa vya panzi wote
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom