Polisi FFU Ukonga nimewakosea nini? Nimepigwa mimi,mke wangu na Mama mkwe bila kosa lolote. Nifanyaje kuchukua hatua?

Who lied to you?

Dhambi ya uonevu ni mbaya sana, yaweza kusababisha maangamizo hata ya wasio na hatia.

Polisi wanapaswa wawe makini sana kushughulika na Raia. Katika kutekeleza majukumu yao waepuke kabisa kuonea Raia. Maana mnyonge akisema basi, huwezi kumdhibiti hata ufanyeje.
Kawaida huwa nawafananisha na mbwa kwani mbwa akiambiwa kamata anafata amri na si kushughulisha akili yake
 
Siku nyingine uwe unatembea na bastola brodher,sheria imeturuhusu kujitetea kwa silaha tunapohisi hatari ya kupoteza maisha. Una chapa bastora wote hao
 
Nilishaapa kutokuja ruhusu mwanangu au mtu yoyote aliye chini yangu kuja kufanya kazi ya upolisi, bora apange nyanya auze kuliko kazi hiyo.
Asilimia kibwa Polisi wa kiAfrica wanafanya kazi bila ya weledi na ujuz.
mara nyingi huwa wanatumia ubabe na vyeo vyao vibaya
 
Pole sana mkuu, kesi ya nyani huwezi kumpa ngedere. Jeshi zima la polisi kwa sasa limeoza, hawatekelezi majukumu kwa mujibu wa sheria inayowaongoza bali kwa utashi wao binafsi. Madhila haya nafuu yake utaipata Mahakamani ingawa nako kwa sasa kumeingiliwa lakini si kwa kiwango kikubwa cha mhimili kutoaminika kabisa. Fungua kesi ya madai (tort) dhidi ya uonezi huo, upate hela lakini pia usaidie kuweka precedent itayookoa wengine baaade.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom