Polisi Dar yakamata silaha nzito za kivita

Duuh.kumbe AK47 ni silaha nzito ya kivita?,sasa yangu sjui nikaisalimishe wapi kituo cha polisi ama lugalo
 
Polisi Dar imekamata silaha aina ya AK 47 na watuhumiwa wawili nyumbani kwa mzee Said Omary (62) baada ya kupata taarifa kuwa kuna wahalifu wanataka kufanya tukio la wizi wa kutumia silaha.

Polisi Dar imekamata watuhumiwa 2 wa wizi wa magari. Wamekutwa na radio call, kadi 10 za benki mbalimbali, leseni za udereva, master keys 15. Baada ya kuhojiwa walikiri makosa na kuonesha magari mawili na pikipiki moja vinavyodhaniwa kuwa ni vya wizi.

Waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo ni Ali Makwaya wa eneo la Tandale, Fredrick Odhiambo wa Tandale pia

Watuhumiwa 8 wamekamatwa kwa uhalifu jijini Dar pia na vielelezo mbalimbali

Watu 2 walikamatwa eneo la sheli ya Big Bon Kariakoo kwa wizi wa magari na wizi benki kwa kutumia master card na master keys

Walikutwa na radio call, leseni za udereva, funguo malaya na vielelezo vingine
Watuhumiwa hao walikiri kuhusika na wizi na kuonyesha magari mawili

Pia watu 6 wamekamatwa na vielelezo mbalimbali ikiwemo radio na sabufa

Pia mtuhumiwa mmoja anayefahmika kama mister K kwatuhuma za matukio mbalimbali, moja ikiwa ni kutishia kwa kutumia bastola mlizi na kuiba vitu mbalimbali kama Tv na fedha
Mzee Said Omary ni mganga wa jadi? Maana wengi kabla ya matukio lazima wakaroge
 
Back
Top Bottom