Polisi ,crazy! kreizi!

Nonda

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
13,358
4,304
Mkuu,

Kuna maiti ya mzee aliyookotwa kijijini kwetu ikiwa na majeraha ya kukatwa katwa. Ni kijiji kidogo cha watu kama 400 kwa hiyo watu wanajuana wote.


Walipelekwa polisi wapelelezi kufuatilia, sasa wakawa wanawahoji wanakijiji ili kupata taarifa.

Walifika nyumbani kwa mzee mmoja wakamsalimia na mazungumzo yao yakawa hivi :-


Mwanakijiji: Karibuni vijana


Polisi: Mzee hapa kijijini pameokotwa maiti, je wewe umesikia?


Mwanakijiji: Ndiyo nimesikia. Imeokotwa wapi?


Polisi: Sasa mzee wewe umezisikia wapi hizi habari?


Mwanakijiji aliwatazama wale Polisi wawili, halafu akawauliza ",nyie vijana vipi? Sasa hivi mumeniambia kuwa imeokotwa maiti hapa kijijini. Na mukaniuliza nimesikia nikawajibu ndio. Nimewasikia nyie mukisema hivyo. Vijana wa leo hamuna kumbu kumbu hata kidogo."


Mzee wa watu anaendelea kuwashangaa na kuwaona machizi.


Polisi nao wakapigwa na mshangao, wao waliona wamepata mtu ambaye atawapa lead lakini wakaishia kuambiwa vijana wa leo hawana kumbukumbu nzuri,wanasema kitu baada ya dakika moja wameshasahau nini walisema.

Wakaona kuwa mzee ni chizi, wakajiondokea.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom