Polisi chapeni kazi, wananchi tuko nyuma yenu

wiseboy.

JF-Expert Member
Aug 11, 2014
2,932
4,542
Nawashangaa sana watu wanaowaandama polisi kwa kuchapa kazi ipasavyo. Hali huko Rufiji, Kibiti, Mchukwi na Pwani kwa ujumla si nzuri hata kidogo.

Hili suala si la vyama ni la kitaifa kabisa. Polisi wanapokusimamisha na wewe ni raia mwema tu, unakimbia ili iweje? Yaani unawezaje kukimbia,? unakimbia ili iweje? Tena ktk eneo lenye mstari mwekundu? Ni lazima polisi watumie risasi tu hakuna namna.

Kwanza naona kama serikali haipo serious na hili jambo, yaani mtu anaua polisi 8 kabisa? I wish I could be a TISS director, ningewanyosha hawa magaidi uchwara hakyanani tena.

Tuacheni ujinga kabisa, tena ilitakiwa eneo lote la Pwani itangazwe hali ya hatari kwa muda wa miezi hata mitatu, saa 12 jioni ndo mwisho wa kutembea kiumbe chochote kilicho hai, vinginevyo ni risasi tu.

Watu mnakuja kulaumu polisi tu, hamlaumu hayo mashetani yanayoua watu hovyo. Nasema polisi chapeni kazi wananchi tupo nyuma yenu.

Na hao magaidi uchwara si kwamba eti polisi waliwakosea, kwani wameua watu wangapi? Natamani kusikia polisi wameua magaidi mia.
 
Hili jambo linahitaji sana hekima, akili ya kulipizana visasi haifai hapa kwa kila upande. Hata mbuyu ulianza kama mchicha. Ubabe kwa kila upande haifai hata kidogo na hakuna atakaye shinda.

I wish I could be IGP
 
Sawa, wachape kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na weledi LAKINI wakichapa kazi kwa UBABE, KIBURI, KUJIONA SANA, KISASI haya mauaji hatutokoma kuyasikia masikioni mwetu.

WAFANYE KAZI KWA UADILIFU
 
Back
Top Bottom