Polisi awapa wanafunzi silaha na kupiga nayo picha, ni dalili za matumizi ya sigara kubwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi awapa wanafunzi silaha na kupiga nayo picha, ni dalili za matumizi ya sigara kubwa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kwitega, Sep 22, 2012.

 1. k

  kwitega Senior Member

  #1
  Sep 22, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakuu,

  Nimeshangazwa na kitendo cha askari mmoja jijini Mwanza mwenye cheo cha Konstebo kuwapa wanafunzi bunduki kisha kupiga picha wakiwa wamebeba silaha hiyo kwa kupokezana huku wengine wakiwa wameishika mithili ya askari walioko kwenye mafunzo ya kulenga shabaha.

  Kitendo hicho kilitokea juzi kwenye shule ya msingi Tambukareli iliyoko kata ya Butimba jijini Mwanza mara baada ya wanafunzi hao kumaliza mitihani yao ya darasa la saba.

  Binafsi nimeziona picha hizo huku askari huyo akiwa amesimama pembeni huku akiwa amelegeza macho hali ambayo kwa haraka haraka unaweza kusema huenda alikuwa ametumia sigara kubwa. Ninavyofahamu mimi, askari haruhusiwi kutoa silaha kwa mtu awaye yote.

  Wakuu, kumekuwapo matukio mengi ya Polisi kutumia silaha ovyo na kusababisha mauaji ya raia wasio na hatia. Je, kitendo cha askari kutoa silaha kwa wanafunzi na kupiga nayo picha, yaweza kuwa moja ya uthibitisho kuwa baadhi yao wanatumia sigara kubwa na kuna umuhimu wa kupimwa akili kabla ya kuajiriwa kwenye vyombo vyetu vya ulinzi na usalama? Tujadiri kwa hoja.
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  hebu weka na picha basi tuone tukio kamili.
   
 3. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #3
  Sep 22, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Ngoja tusubili taarifa ya kamisaa kisha tutaangalia adhabu ya kumpa huyo police,nadhani tutamfungia mwaka1 asiguse bunduki.
   
 4. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #4
  Sep 22, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,236
  Likes Received: 2,916
  Trophy Points: 280
  Mkuu uwezekano wa picha zenyewe km upo weka tujionee wenyewe pia tuje na michango isiyoegemea upande wowote kupitia picha.
   
 5. S

  Same ORG JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 323
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nitarudi
   
 6. Mkulima wa Kuku

  Mkulima wa Kuku JF-Expert Member

  #6
  Sep 22, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Hawezi kuwajibika, kwani ametenda kosa gani? Yeye alikuwa anatekeleza sheria ya utii bila shuruti hivyo hawezi kujiuzulu ng'o! Mmeelewa? Kuna swali la ziada kwangu mimi kamanda Kamu....?
   
 7. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #7
  Sep 22, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Majungu ni janga la kitaifa.
   
 8. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #8
  Sep 23, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  si zilinunuliwa kwa kodi ya wazazi wao? acheni watoto waenjoy jasho la wazazi wao
   
 9. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #9
  Sep 23, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  "Hilo sio kosa la Kamuhanda kujiuzulu".....kosa la kujiuzulu ni lipi?maana kuua au kutoa uhai wa mtu.....sidhani kama lina mjadala!
   
 10. K

  Kijunjwe Senior Member

  #10
  Sep 23, 2012
  Joined: Mar 3, 2007
  Messages: 182
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  "Tunajenga hamasa kwa vijana kujiunga na vyombo vya usalama na ulinzi"
   
 11. Autorun

  Autorun JF-Expert Member

  #11
  Sep 23, 2012
  Joined: Mar 21, 2008
  Messages: 556
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Wataanza kuwavisha na mabomu muda si mrefu
   
 12. Luno G

  Luno G JF-Expert Member

  #12
  Sep 23, 2012
  Joined: Sep 22, 2012
  Messages: 1,883
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  Ukivuta kile kitu bila kusema Bangi nibangue akili yangu niachie umekwisha
   
 13. m

  mkupuo JF-Expert Member

  #13
  Sep 23, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Huyo polisi nadhani hakuwahi kuhudhuria mafunzo ya upolisi pale chuoni moshi bali aliletewa cheti cha kuhitimu mafunzo nyumbani kwa sababu ni mtoto wa afande Kamu.......! Kwani si unaona mwenyewe akili zake ni kama za babake?
   
 14. m

  mwitu JF-Expert Member

  #14
  Sep 23, 2012
  Joined: Jun 22, 2012
  Messages: 857
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  acha ujinga weka picha
   
 15. Root

  Root JF-Expert Member

  #15
  Sep 23, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,122
  Likes Received: 12,837
  Trophy Points: 280
  hebu ushahidi kidogo tuamini na sisi
   
 16. K

  Kiduku JF-Expert Member

  #16
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 480
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hao ndio polisisiem, mtajibeba na ukimfatafata anakulipua kamanda atasema umepigwa na kitu chenye ncha kali
   
 17. P

  Pipitamu Member

  #17
  Sep 24, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "huyo ameishia darasa la nne but siku zao zinahesabiwa,tuweke picha mkuu"
   
 18. M

  Mchaga HD Member

  #18
  Sep 24, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 80
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wametokelezeaaa
   
Loading...