Atasema "sio mtoto wangu lakini ananiita Baba"Joel Bendera atakuja kukana kama kaka yake Wassira!
dah! hii kali jamaa alitaka kujiandikia historia ya kuwa mjumbe wa kwanza wa nec moro kupitia jeshi la polisi
Ndio ujue siasa ni ajira inayolipa tz ndio maana watu wanauwana wakiangia huko.
Wapo wengi kana TIBAIGANA, OMARY MAHITA wote hawa wameishawahi kuingia kwenye mchakato wa kugombea ubunge bahati nzuri walikosa.
Inawezekana, asingejiamini kiasi cha kuandika jina la mtu bila sababu.Labda ni mtoto wa nyumba ndogo ya Joel Bendera. Bendera ni mwanamichezo na kada wa CCM, sifa tosha kumiliki nyumba nyingi. Mkuu weka picha yake tuwafananishe na J Bendera
Hilo tunalijua na ndo maana hatuna imani na jeshi la Polisi, Hizo kadi zao na uanachama wataukana ifikapo 2016 pale chama wanachokiabudu kitakapokuwa out of system kwani nafikiri nguvu ya Umma ndiyo kiboko yao.Mnashangaa nini hapo? Mbona makamanda wa polisi nchi nzima ni wanachama hai wa CCM? Huwezi kuteuliwa kuwa kamanda wa police mkoa au hata wilaya Tanzania kama wewe sio mwanachama hai wa chama tawala. Mwema pale alipo anakadi ya chama tawala, ni moja ya sifa ya kuwa IGP! Hivyo kujidanganya kuwa polisi hawana vyama ni kupoteza muda bure!
Hivi inapo fikia hatua ya kila mtu kutaka kukimbilia kwenye siasa, hii inatoa picha gani kuhusu TAIFA letu in general? wanatafuta umaharufi/kujulikana au utajiri wa haraka haraka - ni TAIFA gani duniani limepiga hatua ya maendeleo kwa kuendekeza mambo ya SIASA?
Mimi naona hatuko justified kumlahumu askali wa watu, naye anajaribu bahati yake - maanake mambo ya siasa yanaonekana kama mchezo wa kamari - PATA,POTEA. God help US.