Polisi auawa Musoma na mtuhumiwa wa ujambazi

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
KamandawaPolisiPICHA-300x224.jpg

POLISI mkoani Mara, Ephraim Lazaro (G- 1379), ameuawa kwa kupigwa risasi na mtu anayedaiwa kuwa ni jambazi aliyekuwa ametoroka kutoka mahakamani zaidi ya mwezi mmoja uliopita na kufuatiliwa baada ya kupata taarifa zake mahali alipokuwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Jafar Mohamed, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 7.00 mchana katika Kata ya Buruma wilayani Butiama ambako askari walikwenda eneo hilo kumfuatilia mtuhumiwa.

Alisema askari wake alipigwa risasi na jambazi huyo aliyefahamika kwa jina la Mbogo James, maarufu kwa jina la China.

Alisema jambazi huyo alikamatwa akiwa na wenzake wawili.

Alisema mtuhumiwa alikuwa akitafutwa baada ya kutoroka mahakamani akiwa anakabiliwa na kesi ya mauaji na unyang’anyi wa kutumia silaha iliyokuwa ikimkabili.

“Tulipata taarifa za mtuhumiwa huyu na askari wetu walikwenda kumfuatilia eneo husika.

“Kwa bahati mbaya kabla hawajamfikia kumkamata alikuwa na silaha na alifyatua na kumpata askari wetu ambaye alifariki dunia muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini.

“Jambazi huyu aliuawa akitaka kufanya jaribio la kutoroka na wenzake wawili walifanikiwa kukimbia.

Chanzo: Mtanzania
 
View attachment 649467

Acheni utani, jambazi hawezi kutoroka mahakamani, alitoroshwa.
 
Daaahhhh kuna maelezo nmeishia kuyaandika nakufuta zaidi ya Mara NNE .

Niseme tu duniani hapa hamna haki.
 
Acheni utani, jambazi hawezi kutoroka mahakamani, alitoroshwa.
Jumatano ya Juma lililopita kuna jamaa aliruka kwenye gari la Polisi mitaa ya Barakuda Segerea,askari walikuwa wamejisahau,wanastuka jamaa ameshatua chini akakimbilia ubavuni mwa daladala ambako kulikuwa Na watu wengi.Askari wakabaki wameduwaa wakashindwa hata kumlenga risasi maana jamaa aliviringika kikomandoo katikati ya watu akatimka zake mbio Na kutokomea mtaani.Gari la Polisi hata halikusimama.
 
Yaani ulitaka hilo gari lisimame ili wote waishie?? Tumia busara kidogo mkuu. Dereva huyo alikuwa na uelewa mzuri wa kazi yake. Aliyetoroka atapatikana tu.
 
Na mie nilielewa hivyo maana gari lingesimama wengine wangesepa

Tumbo ndio Linalotembea,Miguu ni Mikongojo tu.
 
yap, aliuawa katika jaribio lingine la kutoroka. sasa sijui alikuwa anakimbia wakampiga risasi, walimkamata kwanza na kumpiga au alipigwa risasi akijaribu kutoroka lakini alikufa katika harakati za kumpeleka hospitali kuokoa maisha yake...tuelewe nini hapo sasa, habari haijakamilika, hasa ile sentence nzuri tuliyoizoea.
 
watuhumiwa wa kesi za mauaji hasa majambazi makatili waende mahakani wakiwa na chain miguuni hizo pingu za mikononi peke yake hazisaidii kitu kwa hao makatiri...RIP askari wetu.
 
lakini akiwa mahakamani hatakiwi kufungwa kwa vyovyote, sasa pale ndio yeye huwa anaruka na kutoroka, anajichanganya na watu, polisi wanaogopa kurusha risasi itapiga raia waliokuja kusikiliza kesi na yeye anatumia raia kama shield ndio anatokomea hivyo. na wana mbio balaa. nilshashuhudia kwa watu kama wawili wakitoroka mchana kweupe, ni raisi tu, timing. afu ni mpango tu, unakumbuka yule wa kisutu aliyejaribu kuruka fense akapigwa risasi, kuna noah ilikuwa inamsubiri kule nyuma angeruka tu ule ukuta kuna noah ilikuwa inamkimbiza akatokomee mbali huko. jambazi mmoja akiwa ndani, jua kuna wenzie kama 20 hivi huku nje wananafuta namna ya kumtoa mwenzao kwa namna yeyote ile, kwa pesa, kwa vyovyote vile.
 
Hute matatizo yapo mengi nikitaka nielezee mahakama kuu inatakiwa iwe na dock ambayo mtuhumiwa anatoka na kukaa hapo dock na si kama zilivyo hizo mahakama zipo kama kikao cha sherehe jaribu kuangalia Mahakama za Nchi zilizoendelea utaelewa nachomaanisha watuhumiwa huwa wanatoroshwa bara barani wakitoka mahakamani linavamiwa lile gari na majambazi wenzao huku wakiwa na siraha nzito kama wanaiba kumbe wanamtorosha jambazi mwenzao na si kutoka kiboya hivyo harafu niseme eti sawa...
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom