Polisi atimuliwa kwenye nyumba kwa kuuza mihogo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi atimuliwa kwenye nyumba kwa kuuza mihogo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Yo Yo, Dec 18, 2008.

 1. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Wakuu hii habari imenipa huzuni kweli......muangalie askrai huyu na mshahara wake wa elfu 70 kaamua kujikimu na biashara ya mihogo nayo wameona atafaidi sana wakamtimua kambini........
  Nimetokea kumchukia Jk na serikalki yake mpaka basi
  [​IMG]
  Na blog ya Mroki
  Mods mnaweza kuiamisha kama si mahala pake ila nina hasira na mkwere
   

  Attached Files:

  • 1.JPG
   1.JPG
   File size:
   106.6 KB
   Views:
   163
 2. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #2
  Dec 18, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Imeniuma hii kitu kweli nikiangalia samani za mvuja jasho huyu kutwa anang'atwa na mbu akilinda mageti ya mkwere na wenzie leo hii na mshahara wake kiduchu kaamua kuongeza kipato anafukuzwa kama mbwa.Malipo ni hapa hapa duniani
   
 3. K

  Koba JF-Expert Member

  #3
  Dec 18, 2008
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ...inatia huruma sana lakini sheria lazima zifuatwe,lakini mkuu hapo kwenye picha ni story tosha hebu angalia rangi ya huo ukuta,milango na bati,yard iliyojaa vumbi,ndoo nyingi nyingi za maji,poor quality furniture,sijui lile nalo ni banda la kuku au choo and above all jamaa alivyochoka...uongozi mbovu na ufisadi haya ndio matokeo yake ya kuuza mihogo na picha ya umaskini mtupu!
   
 4. Lusajo

  Lusajo JF-Expert Member

  #4
  Dec 18, 2008
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 451
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Ingawa wanaouza madini yetu kwa bei ya kutupa wanaachwa kwenye nyumba badala ya kulazwa keko. Jamaa alikuwa anajiongezea kipato, sasa wanataka akaibe? Duh!! inatia huruma sanaa. (Halafu tunategemea hawa watu watulinde!)
   
 5. BiMkubwa

  BiMkubwa JF-Expert Member

  #5
  Dec 18, 2008
  Joined: Jan 9, 2007
  Messages: 530
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Siamini!! I just cannot believe it! There must be some other reason than just selling mihogo??? There is more to it than meets the eye.......... If admiistrators can stoop this low basi watu wengi wanaoafanya biashara ndogo ndogo na huku wanaishi katika nyumba za mashirika na makampuni basi wangefukuzwa wengi. Kutokana na picha nahisi hapo ni Kilwa road. Kumbukumbu zangu za kilwa road ni kwamba hizi nyumba ni ndogo na maeneo yao ni padogo sana kwa kusema mtu ukalima mihogo na ukauza. Iwapo kama huyu askari anatoa mihogo up country, hiyo stoo ataipata wapi pa kutunza mihogo ya kuuza? Familia nyingi za pale Kilwa road zinategemea wanafunzi wakitoka shuleni na utakuta kila nyumba hapo njiani kuna meza ndogo mbele yake yenye bidhaa mbalimbali. Kama kweli amefukuzwa kwa sababu ya kuuza mihogo, yawezekana alijenga kibanda barabarani na alikaidi amri ya kuibomoa, otherwise I do not get it.
  Pole ziendee familia yake. Na kabla hatujatoa maneno kibao kuikashifu serikali hebu tujiulize kuhusu sheria ya kujijengea vibanda ovyo ovyo njiani. Maana nimeona watu wanapelekana mahakamani kwa sababu fulani kajenga genge mbele ya nyumba ya mtu.
   
 6. BantuGirl

  BantuGirl Senior Member

  #6
  Dec 18, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 157
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Bi mkubwa amini tu ndo maisha ya askari wetu, huwa mara nyingi hawaruhusiwi kuuza kitu bila ya kibali maalumu...... Jamani huyo baba anatia huruma masikini ukute hapo hata pesa ya kupangishia nyumba hana... Eee Mungu angalia maisha haya
   
 7. BiMkubwa

  BiMkubwa JF-Expert Member

  #7
  Dec 18, 2008
  Joined: Jan 9, 2007
  Messages: 530
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Ni kweli anatia huruma sana hasa ukizingatia ana familia. Ila kama kuna vibali vinatolewa kwa nini hakuhakikisha ana kibali? Au kuna mtu amemfitini? Kweli inatia huruma sana. Where there is a will there is a way, pray he gets a way out soon
   
 8. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #8
  Dec 18, 2008
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Sijui unaongelea nini.
  Lakini hali ya huyu jamaa pengine ni njema kuliko Watanzania wengi sana.
  Zile nyumba zilizo kuwa za za serikali kule Oysterbay zilikuwa zikitia huruma kwa uchafu na uchakavu huku ndani wakikaa maofisa waandamizi wa serikali.

  Ofisi nyingi za serikali nazo ziko nyanya kishenzi, zina vumbi la tangu nchi ipate uhuru.

  Sheria Tanzania zinavunjwa/zimevunjwa kwa muda mrefu sana kiasi kwamba wanaofuata sheria wanaonekana ni wavurugaji wa taratibu na waleta kero.
  Na wale wasiofuata sheria wanaingizwa kwenye Bondage ya kutoa rushwa au kukumbana na mikasa kama hii alopata afande.

  Kifupi kufuata au kutofuata sheria Tanzania hakukupi nafuu yeyote, hata shetani na jeshi lake wanadai ni ngumu sana kufanya kazi yao vizuri katika mazingira kama yale ya Tanzania.

  Ukifuata sheria utaadhibiwa kwa kujifanya unajua sana taratatibu, ukivunja sheria utaadhibiwa kwa kuvunja sheria.
  Tanzania mtu unatakiwa kuishi kadri maisha yanavyokuja au yanavyokwenda.
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Dec 18, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Bimkubwa, where have you been? You always go away for a long time before you show up again. Au kwa vile Raj Patel (lol) hayupo siku hizi...
   
 10. share

  share JF-Expert Member

  #10
  Dec 18, 2008
  Joined: Nov 22, 2008
  Messages: 2,294
  Likes Received: 2,277
  Trophy Points: 280
  Naona benchi hapo kama la kanisani! Vipi tena polisi huyu! ni mzee wa kanisa au mkuu wa kigango! akaamua kulihifadhi benchi nyumbani kwake? Au kalifisadi mahali fulani kwenye mawindo yake! Askari wetu hawakawii kubeba mali ikikaa urefu wa kamba yake ya kutanua!!!!
   
 11. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #11
  Dec 19, 2008
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Naona huruma lakini kuna swali muhimu tujiulize...

  Kama askari alikabidhiwa jukumu la kuzuia uvunjaji wa sheria na taratibu halali zikiwemo zile za makazi ya serikali/jumuiya/etc na akawa mstari wa mbele kuzivunja tufanyanye? Tunaweza kuona kuuza mihogo ni kitu kidogo ukitilia maanani kuwa kamshahara kenyewe kadogo lakini nadhani kuna umuhimu wa hatua kama hizi kuchukuliwa. Tukumbuke kuwa kuna mengi maovu yanayofanywa katika kambi zetu za polisi na majeshi. Ni lazima kuanzia mahala fulani na yaweza kuwa bahati mbaya kwamba kwake huyu ndio amengukia kuwa mfano wa mwanzo.

  Vilevile kuna tabia ya baadhi ya watu kutumia kuuza maandazi, mihogo na vinginevyo kama cover ya miashara haramu za gongo na madawa ya kulevya. Makambi yetu ya polisi na jeshi yanaongoza katika hilo.

  Nadhani wakati tunafurahia mifano ya kushunghulikiwa mafisadi wakubwa na tuwe tayari kula uchungu wa kushughulikiwa na viufisadi vyetu vidogovidogo....

  Huu ni mtihani mkubwa kwetu sote..

  Tanzanianjema
   
 12. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #12
  Dec 19, 2008
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Huyo kauza mihogo tu kambini katimuliwa. Mkapa kauza mashirika yetu ya umma mengi tu na kujiuzia kiwira mbona hajatimuliwa bali analindwa kwa gharama za walala hoi?.

  Yanayotokea uturuki yatatokea Tanzania muda si mrefu kama serikali yetu haitachukua hatua madhubuti.
   
 13. Kiungani

  Kiungani JF-Expert Member

  #13
  Dec 19, 2008
  Joined: Feb 2, 2007
  Messages: 274
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Share, hilo siyo bench la kanisani. Ni tendegu za kitanda (kichwa na za pembeni).

  Hapa cha kujiuliza, je itakuwaje huyu jamaa akiamua kushirikiana na wakora/vibaka kuliko kuuza mihogo?
   
 14. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #14
  Dec 19, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Sheria msumeno....
   
 15. share

  share JF-Expert Member

  #15
  Dec 19, 2008
  Joined: Nov 22, 2008
  Messages: 2,294
  Likes Received: 2,277
  Trophy Points: 280
  Nakubali hivyohivyo mkuu Kiungani kwa kuwa hilo nililosema benchi lipo pamoja na accessories za kitanda. Ila bado napata taabu ya kuunganisha mambo ya kiseremala. Pengine mwenzangu mtaalamu kwa hilo. Nashukuru mkuu.
   
 16. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #16
  Dec 19, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  ujasiriamali mwiko jeshini!!!!
   
 17. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #17
  Dec 19, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mkuu hilo siyo bench la kanisani ni tendegu la kitanda upande wa mbele.
  Naamini sisi kama JF Sauti Huru kwenye nchi huru kama Tanzania tunawajibika kumuokoa huyu jamaa kwa kupiga kelele hadi anatendewa haki.
   
Loading...