Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 749
- 1,797
Kijana Richard Peter Lombo (29) ameuawa na polisi wilayani Arumeru kwa kupigwa Risasi kifuani akiwa ndani ya Kituo cha Polisi Usariva Mkoani Arusha baada ya kufikishwa hapo akituhumiwa kwa uhalifu.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Longinus Tibishubwamu akizungumzia tukio hilo kwa Njia ya simu amesema kuwa kijana huyo alikuwa kibaka na alitaka kuchukua silaha ya askari lakini katika mvutano huo ukasababisha risasi kufwatuka jambo ambalo kaka yake Issa Juma amesema kuwa ameshuhudia askari akimfyatulia ndugu yake huyo risasi ya kifuani na kufariki papo hapo.
Ndugu wa kijana huyo wakiwemo wazazi wake wamemtaka waziri wa mambo ya ndani ,Kangi Lugola kuja mkoani hapa kufuatialia tukio hilo kwani kinachoelezwa na kaimu kamanda in uongo mtupu na unalenga kuipotosha jamii.
Familia imegoma kuuzika mwili wa kijana wao uliipo Mochware wakilalamikia unyama uliofanywa na askari hao wasiofuata na kuzingatia maadili ya Kazi yao kwa kufanya mauaji ndani ya kituo hicho cha Polisi bila woga na kudanganya kuwa alitaka kuwapora silaha