Polisi Arusha: Ufafanuzi kuhusiana na tukio la waandishi wawili wa habari wa Global TV na Tripple A kukamatwa

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
Ufafanuzi kuhusiana na tukio la waandishi wawili wa habari wa Global TV na Tripple A Radio mkoani Arusha

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo akiongea na vyombo vya habari leo February 26, amesema kuwa Tarehe 24.02.2022 muda wa saa 4:00 asubuhi huko maeneo ya Sakina katika Halmashuri ya Jiji la Arusha askari wa jeshi la akiba (mgambo) waliwakamata Ester Jackson (38) na Isaya Mollel (20) wote wakazi wa Ngaramtoni wakiwa na Bhangi misokoto 1755 na kuwafikisha katika kituo kidogo cha Polisi Sakina.

Kamanda Masejo ameendelea kusema kuwa Baada ya tukio hilo, baadhi ya watu waliwasiliana na waandishi wa habari kuhusiana na tukio la kukamatwa kwa watuhumiwa hao ambapo walifika eneo la tukio na kuanza kufanya mahojiano na baadhi ya wananchi ambao walishuhudia tukio hilo.

Wakati waandishi hao wakiendelea kuwahoji watu katika eneo la Raskazoni, askari mgambo hao walipita katika eneo hilo ambapo nadaiwa waandishi hao
waliwasimamisha kwa lengo la kuwahoji, kitendo hicho pamoja na kupigwa picha kiliibua mzozo kati ya waandishi hao na mgambo.

Amesema Waliendelea kuvutana kuanzia eneo la Raskazoni hadi eneo la Sakina kilipo kituo cha Polisi na kusababisha vurugu eneo hilo

ACP MASEJO amewaambia waandishi kuwa askari polisi waliokuwa zamu katika kituo hicho waliomba msaada kutoka kituo cha Polisi kati (Central), kutokana na idadi ya watu kuanza kuongezeka katika kituo hicho, ndipo Mkuu wa kituo cha Polisi Kati alifika kituoni hapo na kuwachukua waandishi hao wa habari pamoja na mgambo kwa ajili ya mahojiano, ambapo waliachiwa baada ya kuhojiwa.

Kamanda Masejo ameendelea aliendelea kusema Baada ya kupata maelezo ya watu mbalimbali walioshuhudia kuanzia chanzo cha mzozo huo, tutapeleka jalada kwa Mwendesha Mashtaka wa Serikali kwa maamuzi ya kisheria.

Mwisho ACP Masejo amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha litaendelea kuhakikisha wananchi wakiwepo waandishi wa habari wanaendelea kufanya shughuli zao katika mazingira ya amani, utulivu na usalama kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi.

Pia, soma:

1). ' IGP Sirro, angalia Polisi wako wa Arusha Wanavyo lazimisha Rushwa kwa Kushirikiana na Mgambo
 
POLISI subirini majibu ya zile kamati za mtwara na kilindi! reshuffle ni kubwa mtatikisika sana hamtaamini!
maisha ya kuonea yanaanzia kwa ma OCD! wengi waganga njaa kwa kukosa weledi! unategemea mtaji wa maisha kwa kubambika makosa
 
Hakuna alichojibu cha maana askari wake wamechukua 90000 nae kawalinda,kazi ya police kwa tz ni laana yani wao wako juu ya sheria...toka lini mgambo akafanya kazi ya kusimamisha wao ni kuwahoji...mimi akiingia anga zangu mgambo namfurahisha atajua hajui
 
Afrika raha sana.

Matukio yetu kwenye bara hili kila siku ni vituko, yaani ukisoma au kuwepo eneo la tukio unabaki kucheka tu mwenye maamuzi na asiye na maamuzi kila mtu ana hofu au ujuaji.

👉🏾 I'm still earning human characters.
 
Hivi kisheria nani mwenye uwezo to arrest a suspect?maana naona ni vurugu tu tunazo,Maine yangu ni police tu ndio wapewe mamlaka hayo, uhamiaji (only kitengo cha law enforcement)majeshi mengine yote ni lazima yaite police kama kutakua na arresting hivyo hivyo kwa raia.
 
Back
Top Bottom