Polisi amtetea mtuhumiwa kortini, aliyeshtakiwa kwa kughushi

mawazomgala

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
342
212
KESI ya kughushi inayomkabili mfanyabiashara,Hans Aingaya Macha imechukua sura mpya,baada ya askari Johanes Mgendi mwenye namba E 2982 kutoa ushahidi katika upande wa mtuhumiwa kwenye kesi hiyo.

Mgendi ambaye ni mtaalamu wa maandishi Makao Makuu ya Polisi mjini Dar es Salaam,alitoa ushahidi katika kesi hiyo, iliopo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu chini ya Hakimu Devotha Kisoka.

Askari huyo, alidai nyaraka alizochunguza amebaini miandiko inafanana na kuomba mahakama ipokee ushahidi wake, katika kesi hiyo inayomkabili mfanyabiashara huyo mahakamani hapo.

"Haya ni maoni yangu, nililetewa jalada la uchunguzi na askari wa Kituo Kikuu cha Polisi kuchunguza suala hilo na kutoa maoni hayo,''alidai askari huyo na kumfanya wakili wa serikali, Nasoro Katuga kutikisa kichwa.

Hata hivyo, Katuga alimuuliza swali askari huyo kuwa mbona uchunguzi wa suala hilo,ulishafanywa na mkuu wako wa idara ya uchunguzi, Amaan Renatus Saad na kuonyesha saini zimegushiwa, ambaye alikuwa Mkuu wa Kitendo cha Uchunguzi wa Maandishi Makao Makuu ya Polisi nchini.

"Mbali ya nyaraka hizi kufanyiwa uchunguzi nchini, pia Jeshi la Polisi Kenya lilifanya uchunguzi na kubaini mtuhumiwa amegushi nyaraka, huoni unakwenda kinyume na wachunguzi wenzako waliokuzidi ujunzi akiwemo Mkuu wako wa kazi,ambaye ametoa ushahidi na kuonyesha nyaraka zimegushiwa, huoni unapingana na maoni ya bosi wako,?''aliulizwa swali Katuga kwa askari huyo.

Swali hilo, lilimfanya askari huyo aliyekuja mahakamani kumtetea Macha kudai kuwa Polisi hakuna ukubwa huku akisisitiza kuwa yale ni maoni yake yeye na hayahusiani na Amaan,ambaye tayari alishatoa ushahidi kwa upande wa serikali.

Hakimu wa mahakama hiyo, alihairisha kesi hiyo hadi Januari 22, mwakani kwa ajili ya kutoa hukumu katika kesi hiyo ya kugushi inayomkabili mfanyabiashara huyo.

Macha anashitakiwa kwa kosa la kugushi hati, mkataba wa mauziano na kuwasilisha hati ya umilikishaji miliki kwa Msajili wa Hati.
 
hana kazi huyo askari ngoja achunguzwe, hao ndio wanaolishusha hadhi na umuhimu wa Jeshi la Polisi
 
Naona Mangi Kama kawa, kamtia mtu ndimu...ogopa Sana hawa watu,huyu afande kwa jinsi jeshi la lilivyo mbona kaikanyaga na atajuuuta.
 
Mapolisi ndiyo kazi yao, kwani ana tofauti gani na hao wanaomba rushwa katika barrier za barabarani? Ama wanaojifanya mahakimu?
 
Naona Mangi Kama kawa, kamtia mtu ndimu...ogopa Sana hawa watu,huyu afande kwa jinsi jeshi la lilivyo mbona kaikanyaga na atajuuuta.
 
KESI ya kughushi inayomkabili mfanyabiashara,Hans Aingaya Macha imechukua sura mpya,baada ya askari Johanes Mgendi mwenye namba E 2982 kutoa ushahidi katika upande wa mtuhumiwa kwenye kesi hiyo
 
Huo ndio mfumo wa nchi hii kwani bila cho chote hupati kitu iwe Mahakmani, TAKUKURU au ofisi yo yote ya Serikali.
Nchi hii imejengwa katika msingi wa rushwa.
 
Back
Top Bottom