Polisi: Aliyeuawa Singida akidaiwa kuwa Kiongozi wa CHADEMA, alikuwa dereva Bodaboda na sio Kiongozi wa CHADEMA

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,442
3,353
Jeshi la Polisi mkoani Singida limesema dereva wa bodaboda, Alex Jonas (40) aliyeuawa na watu wasiofahamika alikuwa siyo kiongozi wa Chadema.

Jonas ambaye ni mkazi wa Majengo mjini Manyoni mkoani Singida mwili wake ulikutwa umepigwa na kitu chenye ncha kali Februari 25, 2020.

Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi Februari 27, 2020 ofisini kwake Kamanda wa Polisi, Sweetbert Njewike amesema dereva huyo ameuawa Februari 25 mwaka huu nyakati za usiku.

Amesema kijana huyo ambaye kituo chake cha kazi kilikuwa Mwembeni mjini Manyoni bado haijafahamika siku ya tukio, aliondoka muda gani.

Kamanda Njewike amesema mwili wa marehemu uliokotwa mbungani mbali na barabara, ukiwa umechomwa chomwa sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo kichwani na miguuni.

“Wakati mwili wa Alex ukiokotwa mbungani, pikipiki yake iliokotwa kandakando ya barabara iendayo Dodoma. Baada ya mwili kukaguliwa alikutwa na vitu vyote isipokuwa simu. Chanzo cha mauaji hayo bado hakijafahamika, upelelezi unaendelea,” amesema.

Amesema hadi sasa hakuna mtu anayeshikiliwa kuhusiana na mauaji hayo ya kikatili na wameanzisha msako mkali.

“Tunaomba mwananchi yeyote mwenye taarifa sahihi juu ya tukio hilo atoe kwenye kituo chochote cha polisi kilicho karibu au mamlaka zingine ili watu\mtu aliyehusika aweze kukamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria,” amesema.

Kuhusu marehemu kuwa kiongozi wa Chadema wilayani Manyoni, Njewike amesema hilo wamelisikia lakini walipofanya utafiti imebainika kuwa alikuwa ni dereva wa bodaboda tu na sio kiongozi wa Chadema.

Wakati Kamanda Njewike akisema kuwa Alex hakuwa kiongozi wa Chadema, Mwenyekiti CCM Halmashauri ya Itigi, Alli Minja akizungumza na Mwananchi amesema marehemu Alex alikuwa mwenyekiti Chadema Wilaya ya Manyoni.

“Binafsi nasikitika kwamba sitohudhuria mazishi yake kutokana na kukosa usafiri. Alex alikuwa Chadema wa aina yake,” amesema na kuongeza;

“Alikuwa na utamaduni wa kuhudhuria vikao vya mabaraza ya madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni na kwetu huku Itigi. Kwenye suala la miradi ya maendeleo, ulikuwa huwezi kujua kama ni wa upinzani. Alikuwa anatoa ushirikiano wa hali ya juu. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi,” amesema Minja.

Akizungumza leo na Mwananchi, mmoja wa viongozi wa Chadema Kanda ya Kati, Idd Kizota amesema wapo katika maandalizi ya mazishi ambayo yatafanyika wilayani humo Jumamosi, Machi 1, 2020.

Zaidi, soma: https://www.jamiiforums.com/threads...oani-humo-hakuwa-kiongozi-wa-chadema.1696081/

https://www.jamiiforums.com/threads...jonas-auawa-kwa-kukatwakatwa-mapanga.1695330/
 
Kwani bodaboda hawezi kuwa kiongozi, au bodaboda kukatwa mapanga kwa polisi wanaona kwaida tu.
 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Itigi anamtambua marehemu,

Kamanda wa Polisi hamtambui marehemu,

Kama alikuwa anahudhuria VIKAO vya Halmashauri za Manyoni na Itigi,

ni dhahiri kuwa DC wa Manyoni anamtambua, OCD Manyoni anamtambua, Mkurugenzi Manyoni anamtambua, Mkurugenzi Itigi anamtambua.

Huyo Kamanda wa Polisi anayesema marehemu siyo Kiongozi wa Chadema anakusudia Nini?
 
Ilikuwaje mwenyekiti CCM aseme hivyo?Au alikuwa anamuwinda na bahati mbaya wauaji wakakosea njia?
 
Hivi ukiwa dereva wa boda boda huwezi kuw akiongozi wa Chadema?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ujinga huu unalidhalilisha jeshi la polisi. Raia wanahaki ya kikatiba kuwa katika vyama vingine. Polisi ni watumishi wa raia. Kwa polisi kudhania wajibu wao ni kwa chama tawala pekee wanawatenga na raia na kuifanya kazi yao kuwa hatari kama askari vitani. Ujinga huu utaligharimu jeshi na hata kuvunjwa katika siku zijazo
 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Itigi anamtambua marehemu,

Kamanda wa Polisi hamtambui marehemu,

Kama alikuwa anahudhuria VIKAO vya Halmashauri za Manyoni na Itigi,

ni dhahiri kuwa DC wa Manyoni anamtambua, OCD Manyoni anamtambua, Mkurugenzi Manyoni anamtambua, Mkurugenzi Itigi anamtambua.

Huyo Kamanda wa Polisi anayesema marehemu siyo Kiongozi wa Chadema anakusudia Nini?
- KumbukiziMTAFUTANO.jpg
 
Kwamba wewe ndio Unalazimisha awe Kiongozi wa Hiyo Saccosa sindio
Wacha upuuzi

Maneno hayo muulize M/kiti wa Halmashauri ya Itigi.

Kamanda anapata wapi UJASIRI wa kusema siyo kiongozi bali ni dereva wa bodaboda?

WENYE MAMLAKA SHIRIKIANENI KATIKA KUTOA TAARIFA ZINAZOGUSA UHAI WA BINADAMU (MTANZANIA) BILA KUJALI CHAMA CHAKE.
 
Back
Top Bottom