Polisi aliyetinga klab na bangi atimliwa kazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi aliyetinga klab na bangi atimliwa kazi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Apr 4, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 4, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Rehema Matowo, Moshi
  POLISI mkoani Kilimanjaro imemfukuza kazi askari wake G 8415 PC Deogratius Chamwa (22), aliyeingia disko na misokoto ya bangi na kumpiga mlinzi wa ukumbi wa Pub Alberto.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Absolom Mwakyoma, alithibitisha kufukuzwa kwa askari huyo na kwamba, hatua hiyo inatokana na kufanya shambulio na kukutwa na misokoto mitatu ya bangi, makosa ambayo ni ya jinai.

  Mwakyoma alisema polisi huyo alifanya fujo akiwa disko kwenye ukumbi wa Pub Alberto Machi 24, mwaka huu saa 6:00 usiku.

  Alisema askari huyo alimshambulia mlinzi wa pub hiyo kwa kumng’ata mkononi na kutoa lugha ya matusi, alipokamatwa alifanyiwa upekuzi na kukutwa na misokoto mitatu ya bangi.

  “Baada ya tukio hilo alifikishwa kwenye mahakama ya kijeshi na kukutwa na kosa la jinai, kutokana na makosa hayo hatuna budi kumfukuza kazi na baada ya hapo atapelekwa mahakamani kujibu shtaka linalomkabili,” alisema Mwakyoma.

  Hivi karibuni kumekuwa na matukio ya utovu wa nidhamu yanayofanywa na polisi, hili likiwa ni tukio la pili kutokea ndani ya miezi miwili baada ya askari mwingine kuacha lindo na kuingia disko kwenye ukumbi huohuo akiwa na silaha. Pia, polisi huyo alifukuzwa kazi.

  Kamanda Mwakyoma alisema polisi aliyefukuzwa kazi jana ni wa 18 tangu mwaka jana kwa makosa mbalimbali ikiwamo utovu wa nidhamu.

  Alisema huo ni utaratibu wa polisi ambayo ina kamati ya maadili inayokaa na kutathmini utendaji wa askari na kwamba, pale askari anapopotosha anawajibishwa ikiwamo kushushwa cheo, kufukuzwa kazi au kubadilishwa kitengo.Alisema hawafurahi kumfukuza kazi askari, lakini pale anapovuka kiwango cha makosa jeshi hali jinsi ya kumsaidia zaidi ya kumfukuza.

  Polisi aliyetinga klab na bangi atimliwa kazi
   
 2. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mmmmmhh!

  Ama kweli kweli KUNGURU hafugiki!

  Atajashangaa uraiani na roho yake!
  Anafikiri huu msoto raia waliyonayo anafikiri tunafaidi siyo!

  Asiyesikia la MAMAYE,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,!!!!
   
 3. Thomas Odera

  Thomas Odera Verified User

  #3
  Apr 4, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 644
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Ukitaka kujua ya kuwa polisi ni wateja wakubwa wa bangi na madawa ya kulevya fuatilia mienendo yao na pia mirungi ndio haswa nenda stand ya magari ya nairobi na namanga hapo Arusha ujionee. Hongera jeshi kwa hilo ila asije akawa ni mtoto wa maskini halafu wa wakubwa anahamishwa
   
 4. j

  jmnamba Senior Member

  #4
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 140
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Gazeti la Uhuru - Ile habari ya Askari aliekutwa na misokoto mitatu kama sikikosei ya kitu cha arusha (sigara kali kuliko zote) afukuzwa kazi baada ya shitaka lake kufikia tamati katika mahakama za kijeshi (polisi).
   
 5. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #5
  Apr 4, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Nojuavyo geshi letu la polisi lina asilimia kubwa ya waathirika wa hiyo makitu......... Watafukuza wangapi?, mi naona wangetafuta mbinu mbadala ya kuwafunza kuepuka mambo hayo la sivyo fukuzafukuza zingemkumba hata zombe.
   
 6. O

  OMEGA JF-Expert Member

  #6
  Apr 4, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 671
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 60
  Kufukuzwa tu haitoshi kwani kupatikana na Bhangi-cannabis sativa ni kosa la jinai,apelekwe mahakamani.
   
 7. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #7
  Apr 4, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Amefukuzwa kazi?
  Kwa sasa anaish gereza lipi?
   
 8. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #8
  Apr 4, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Yote 9! 10 na yule Askari aliyeingia na SMG Club?? hawa ndio vijana wa Saidi Mwema, natumaini haya mafunzo wanayapata pale CCP Moshi.
   
 9. j

  jmnamba Senior Member

  #9
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 140
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tatizo sijui turudi nyuma issue ya mishahara kuwa midogo ndio mpaka hupelekea kuzuka hili na lile kwa jamii tunayoitegemea mfano polisi na issue ya bangi/rushwa/nk nk Polisi ni wito au wanajiunga kwa kulingana na soko la ajira kuwa gumu!?
   
 10. i pad3

  i pad3 JF-Expert Member

  #10
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,520
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Polisi aliyetinga klab na bangi atimliwa kazi
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Tuesday, 03 April 2012 21:32 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  Rehema Matowo, Moshi
  POLISI mkoani Kilimanjaro imemfukuza kazi askari wake G 8415 PC Deogratius Chamwa (22), aliyeingia disko na misokoto ya bangi na kumpiga mlinzi wa ukumbi wa Pub Alberto.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Absolom Mwakyoma, alithibitisha kufukuzwa kwa askari huyo na kwamba, hatua hiyo inatokana na kufanya shambulio na kukutwa na misokoto mitatu ya bangi, makosa ambayo ni ya jinai.

  Mwakyoma alisema polisi huyo alifanya fujo akiwa disko kwenye ukumbi wa Pub Alberto Machi 24, mwaka huu saa 6:00 usiku.
  Alisema askari huyo alimshambulia mlinzi wa pub hiyo kwa kumng’ata mkononi na kutoa lugha ya matusi, alipokamatwa alifanyiwa upekuzi na kukutwa na misokoto mitatu ya bangi.

  “Baada ya tukio hilo alifikishwa kwenye mahakama ya kijeshi na kukutwa na kosa la jinai, kutokana na makosa hayo hatuna budi kumfukuza kazi na baada ya hapo atapelekwa mahakamani kujibu shtaka linalomkabili,” alisema Mwakyoma.

  Hivi karibuni kumekuwa na matukio ya utovu wa nidhamu yanayofanywa na polisi, hili likiwa ni tukio la pili kutokea ndani ya miezi miwili baada ya askari mwingine kuacha lindo na kuingia disko kwenye ukumbi huohuo akiwa na silaha. Pia, polisi huyo alifukuzwa kazi.

  Kamanda Mwakyoma alisema polisi aliyefukuzwa kazi jana ni wa 18 tangu mwaka jana kwa makosa mbalimbali ikiwamo utovu wa nidhamu.

  Alisema huo ni utaratibu wa polisi ambayo ina kamati ya maadili inayokaa na kutathmini utendaji wa askari na kwamba, pale askari anapopotosha anawajibishwa ikiwamo kushushwa cheo, kufukuzwa kazi au kubadilishwa kitengo.Alisema hawafurahi kumfukuza kazi askari, lakini pale anapovuka kiwango cha makosa jeshi hali jinsi ya kumsaidia zaidi ya kumfukuza
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 11. M

  Marytina JF-Expert Member

  #11
  Apr 4, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  ukumbi wa PUB ALBERTO una majini utaingia utake usitake
   
 12. l

  laboratory Member

  #12
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tunapaita jumba la dhambi au kanisani lzma uendeee;;;(alberto)
   
 13. RasJah

  RasJah JF-Expert Member

  #13
  Apr 4, 2012
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 697
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  huyo polisi nae alizidisha ugangwe bana.. misokoto yote ile ilikuwa apulize na nani au ndo usela mavi wacha akapigwe na jua la mtaani anyoloke vizr
   
 14. hengo

  hengo JF-Expert Member

  #14
  Apr 4, 2012
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 403
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kufukuzwa kazi, maana kinachofuata ni kupelekwa mahakamani.Hivi vitu vya waarusha bwana kimewaasili wengi mm nashauri serikali ianzishe kampeni ya kupima watu walioathirika na madawa ya kulevya, maana hili Taifa tunakoelekea litajaa mateja tu hadi ngazi za juu za uongozi kwa sababu mpaka sasa wapo wanaokula kitu Malijuana at the Top rank.hii ni tishio kwa ustawi wa Taifa
   
 15. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #15
  Apr 4, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,727
  Likes Received: 1,634
  Trophy Points: 280
  safi sana waje pia na Namanga Oyseterbay Police wanalewa chakali wakiwa kwenye lindo.
   
 16. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #16
  Apr 4, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [h=2]Polisi aliyetinga disko na bangi afukuzwa kazi[/h]
  [​IMG]


  Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Absalom Mwakyoma


  Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro, limemfukuza kazi askari wake, Deogratius Chang'a, kwa kosa la kuingia ukumbi wa disco wa Pub Alberto wa mjini hapa na kufanya vurugu, kuumiza watu na kukutwa na misokoto mitatu na nusu ya bangi.

  Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Absalom Mwakyoma, alithibitisha jana kufukuzwa kazi kwa askari huyo na kueleza kuwa ni baada ya Mahakama ya kijeshi kumkuta na hatia na kuamuru afukuzwe kazi kwa fedheha.

  Alisema kuwa kosa la kwanza la askari huyo ni kufanya fujo katika ukumbi huo na kumjeruhi mmoja wa wafanyakazi wa ukumbi huo kwa kumng'ata meno na kosa la pili ni kukutwa na misokoto ya bangimfukoni.

  "Mnamo Machi 24, mwaka huu, saa 6:05 usiku, katika kituo cha Polisi Kati Moshi Mjini, askari huyo alipekuliwa na kukutwa na bangi, kitendo ambacho ni kinyume na mwenendo mwema wa Jeshi la Polisi
  Tanzania. Amepatikana na hatia kwa makosa yote mawili, Kamati ya Maadili ya Polisi ilipendekeza afukuzwe kazi kwa fedheha, hivyo tumemfukuza kazi kuanzia Aprili 3, mwaka huu," alisema.

  Askari huyo alimjeruhi mlinzi wa pub hiyo, Rajab Hamad, kwa kumng'ata meno mkononi, kutoa matusi na kuwapiga ngumi watu mbalimbali bila sababu, kitendo ambacho ni kinyume na mwenendo mwema wa Jeshi la Polisi nchini.
  Baada ya tukio hilo, Jeshi hilo lilieleza kuwa askari huyo akiwa amevalia kiraia alifika katika ukumbi huo kwa lengo la kucheza miziki na kwamba alikuwa akinywa pombe, lakini baada ya muda alianza kufanya vurugu.
  Walinzi wa ukumbi huo walipojulishwa juu ya vurugu hizo, walifika na kuanza kukabiliana naye na ndipo alipomjeruhi mmoja kwenye mkono na mmiliki wa ukumbi huo, Christopher Shayo, alipoingilia kusuluhosha, alipigwa ngumi ya usoni.  CHANZO: NIPASHE
   
 17. s

  sugi JF-Expert Member

  #17
  Apr 4, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  hicho ni"KIDHIBITI"ni haki yake kuwa nacho kama polisi,ili kuwawekea watu anaowashika na kwa matumizi yake anapokwenda kutawanya watu maandamanoni;kaonewa tu
   
Loading...