chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 19,685
- 22,694
Shahidi wa kwanza katika kesi ya kuzuia polisi kutekeleza majukumu yao na kushambulia inayomkabili Naibu Waziri wa Fedha wa zamani, Adam Malima amesema alilazimika kupiga risasi hewani ili kuwatambulisha wananchi kuwa yeye ni askari aliyepata mafunzo Chuo cha Moshi.
Shahidi huyo, H 7818 PC Abdul wa Kituo Kikuu cha Polisi alieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa lengo lilikuwa ni kujinusuru na watu waliotaka kumvamia wakati wa kumkamata Malima. Mbali ya Malima, katika kesi hiyo mshtakiwa mwingine ni Ramadhan Mohammed anayekabiliwa na kosa la kuzuia polisi kutekeleza majukumu yao na kushambulia.
Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage, shahidi huyo alidai anakumbuka Mei 15 alikuwa na jukumu la operesheni iliyohusisha Kampuni ya Priscane Business.
Alidai walikwenda maeneo ya Masaki Kinondoni Dar es Salaam, akiambatana na Konstebo Edger na Msimamizi wa Kampuni ya Priscane, Joseph Mwita.
Aliendelea kuwa baada ya kumkamata Malima na vurugu kutokea eneo la Double Tree Msasani, wananchi walianza kumsogelea na kulazimika kupiga risasi tatu hewani ili wamtambue kuwa yeye ni polisi aliyepitia mafunzo Chuo cha Polisi Moshi.
Baada ya kumaliza ushahidi wake, Hakimu Mwijage aliahirisha kesi hadi Oktoba 3, itakapoendelea. Malima anawatetewa na Wakili Peter Kibatala.
Chanzo : Mwananchi