Polisi akamatwa kwa kumbaka denti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi akamatwa kwa kumbaka denti

Discussion in 'Celebrities Forum' started by MziziMkavu, Jul 4, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 4, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,612
  Trophy Points: 280
  uwazi [​IMG] Imedaiwa kuwa askari huyo alikuwa akimfuatilia mwanafunzi huyo siku nyingi na wakati mwingine askari wenzake ndio waliokuwa wakimzuia kumwita mwanafunzi huyo katika ofisi za jeshi la polisi.

  Hata hivyo, alisema kuwa siku ya tukio askari huyo alimwita mwanafunzi huyo ambaye baba yake ni afisa mgambo katika wilaya moja ya mkoa wa Iringa kwa lengo la kutaka kumtuma.

  Shuhuda huyo aliongeza kuwa baada ya mwanafunzi huyo kufika katika nyumba aliyokuwa akiishi mtuhumiwa ndipo alipomfungia ndani ya chumba chake na kuanza kumbaka hadi asubuhi alipomruhusu kurudi kwao.

  "Huyu jamaa ni askari mwenzetu lakini vitendo vyake vinaonyesha kulidhalilisha jeshi la polisi kwani hii ni mara ya pili anabaka┬ůkuna kesi nyingine inamkabili ya kubaka lakini kuna dalili za kuizima,"alisema shuhuda huyo.

  Kwa mjibu wa shuhuda huyo agizo la kumweka ndani askari huyo lilitolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Bw. Advoacate Nyombi.

  Kamanda Nyombi akiongea juzi kwa njia ya simu na gazeti hili, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba askari huyo atashitakiwa kijeshi baada ya taratibu za mashitaka kukamilika. Global Publishers - Tanzania Newspapers
   
Loading...