Polisi afukuzwa kazi kwa kumbaka mtuhumiwa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,868
30,337
KWA UFUPI
Kamanda Athumani alisema kuwa mbali ya kufukuzwa kazi askari huyo tayari amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mbozi ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.
JESHI la Polisi mkoani Mbeya limemfukuza kazi askari wake Enock Daffa (22) kwa tuhuma za kufanya mapenzi na mtuhumiwa wa kike mwenye umri wa miaka 25 katika Kituo cha Polisi cha Mji mdogo wa Tunduma, Wilaya ya Momba, mkoani hapa.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Athuman Diwani, askari huyo alitenda kosa hilo Novemba 21,2012 na kwamba mtuhumiwa aliyefanya naye mapenzi alikuwa akikabiliwa na kosa la wizi.

Kamanda Athumani alisema kuwa mbali ya kufukuzwa kazi askari huyo tayari amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mbozi ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.
Aidha alisema kuwa hali kama hiyo haitaweza kuvumiliwa na Jeshi la Polisi na kwamba atakayebainika kufanya tukio kama hilo adhabu yake itakuwa ni kufukuzwa kazi.

Kamanda huyo alitoa wito kwa askari polisi kufanya kazi kwa kufuata sheria na kanuni za Jeshi la Polisi kama mwongozo unavyowaagiza ili kulinda maadili ya Jeshi la Polisi ambacho ndicho chombo kinachotumika na wananchi katika kuzisimamia sheria.

Akizungumzia tukio hilo, baba mzazi wa askari huyo alisema kuwa kitendo alichofaya mtoto wake si cha kiungwana ambacho pia kimetia fedheha familia yake pia kwa jeshi la Polisi ambalo limepewa dhamana ya kutunza usalama wa raia na mali zake.

Wakati huohuo, katika kijiji cha Malangali Barabara ya Mbeya-Iringa, Wilaya ya Mbarali gari aina ya Nissan Patrol lilimgonga mtembea kwa miguu na kusababisha kifo chake papo hapo.

Alisema kuwa mwili wa marehemu bado haujafamika na mwili umehifadhiwa katika Hospitali ya Chimala Mission na kwamba juhudi za kuutambua mwili wa marehemu na mahali anapotoka zinaendelea.Polisi afukuzwa kazi kwa kumbaka mtuhumiwa - Kitaifa - mwananchi.co.tz
 

Songoro

JF-Expert Member
May 27, 2009
4,124
1,012
Hakuna ubakaji kuna kitendo cha ngono kwano wote walikubaliana ndo maana kafukuzwa badala ya kushtakiwa kwa ubakaji mtuhumiwa nae afukuzwe mahabusu si katenda yaliyokinyume na sheria za mahabusu!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom